oktoba 5, 2006: Kepteni George Mazula akiwapokea watoto wake uwanja wa ndege wa Dar walipowasili na miili ya marehemu Walter Mazula na Vonetha Nkya waliouwawa kikatili huko Detroit, Marekani. Kwa kumbukumbu hii ya kusikitisha bofya hapa na hapa

MAZISHI YA ALIYEKUWA RUBANI MKUU WA ATC KEPTENI GEORGE MAZULA YANATARAJIWA KUFANYIKA SIKU YA JUMATANO KATIKA MAKABURI YA KINONDONI, DAR.
KWA MUJIBU WA TAARIFA ZA FAMILIA, SHUGHULI ZITAANZAIA NYUMBANI KWA MAREHEMU MIKOCHENI MAJIRA YA SAA TANO. MISA ITAFANYIKA KATIKA KANISA LA MTAKATIFU MARTHA LILILOPO JIRANI NA NYUMBANI KWA MAREHEMU.
BAADA YA MISA MWILI WA MAREHEMU UTAHAMISHIWA VIWANJA VYA LEADERS CLUB KINONDONI MAJIRA YA SAA NANE KWA AJILI YA HESHIMA ZA MWISHO, AMBAPO BAADA YA HAPO MWILI UTAPELEKWA MAKABURINI KWA MAZISHI.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Pole sana Aunt Harrieth.. Tunamuomba Mwenyezi Mungu akupe nguvu na akufariji ktk kipindi hiki kigumu sana cha msiba..
    Bwana alitoa na Bwana ametwaa.. jina lake litukuzwe.
    Mungu ailaze mahali pema peponi, roho ya Uncle George.. Amin
    Checkingo's..

    ReplyDelete
  2. samahani kaka michuzi sasa mbona kichwa cha habari kinasema kuwa kapteni kuzikwa halafu unasema picha yupo anapokea miili ya watoto wake, je nini mimi ndie kiswahili kimenishinda atazikwaje ilhali yu hai? au mwenzetu unaona ya mbeleni?

    ReplyDelete
  3. Pumzika Kepteni Mazula,mungu amekupenda zaidi.Umeondoka mapema wakati website ya aliyekuwa mwajiri wako inamaliza mwaka sasa bila/haiwezi kufunguka.Inasikitisha.

    ReplyDelete
  4. AKIWAPOKEA WATOTO WAKE OKTOBA 5, 2006 ANONY WA PILI SOMA VIZURI TENA HAPO JUU!!!!

    ReplyDelete
  5. Hivi ni lazima apelekwe Leaders Club? Kwani nyumbani kwake hapatoshi au hana ndugu anayeweza kutoa nyumba yake? Haijalishi watu watakuwa wengi kiasi gani, kwa kweli sijui... lakini mimi binafsi SIJAIPENDA Mazula kuagwa "CLUB".

    ReplyDelete
  6. Anony wa pili ukisoma maelezo mwanzo wa sentensi unasema october 5, 2006. sasa huelewi nini? kwani 2006 si alikua mzima!

    ReplyDelete
  7. Uwanja wa Leaders una nafasikubwa na kwakuwa inategemewa kuwa na watu wengi kuja kumuaga Marehemu ndio maana wamechagua hapo.Ni sawa tu na kumuaga mtu muhumbili. Kuna ufinyu wa parking nyumbani na eneoni dogo kulinganisha idadi ya waombolezaji watarajiwa na pia ni karibu na makaburi ya Kinondoni watakaomuaga leaders wanayoosha kwa miguu hadi Makaburini ndio maana wameamua hivyo na si vinginevyo. Ndugu wakaribu kabisa watamuagia nyumbani as usual

    ReplyDelete
  8. Wacha aagwe leaders siku hizi waombolezaji nao wamekuwa kwapu kwapu hawataki vurugu. wataibiana waombolezaji mpaka wataingia kwa wafiwa

    ReplyDelete
  9. Uncle Michu,

    Hiyo picha hapo juu inanisikitisha sana, kwanza sikujua kwamba Kepten mazula amefariki, pili kwenye picha yupo na Uncle Isaack kwagilwa (aliye vaa shati la Kitenge la Brown) ambae nae alifariki Ghafla mwanzoni mwaka huu, hawa wawili ni marafiki wa karibu mno mno. Kwakweli nangependa ni wape pole wafiwa wa familia zote mbili (Mazula's & Kwagilwa's) kwasababu najua kifo cha George kitakuwa kimetonesha kidonda cha kifo cha Isaack na cha Walter pia.
    MUNGU AWALAZE MAHALI PEMA, WAKAPUMZIKE MILELE.
    AMEN.

    ReplyDelete
  10. Rest In Peace Captain George Mazula.We will miss you! Jamani George Mazula alikuwa mcheshi,mtu wa watu... Ni kilio gani Dar hii utaenda umkose Captain... Captain alikuwa hachagui misiba ya matajiri wala ya walala hoi yote alihudhuria. Tulimpenda Captain George Mazula lakini MUNGU amempenda zaidi. RAHA YA MILELE UMPE CAPTAIN GEORGE MAZULA EEH BWANA... NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE... APUMZIKE KWA AMANI. AMINA. Poleni sana kwa msiba huu mzito Harriet na watoto na wenzangu wote tulioguswa na msiba huu.

    ReplyDelete
  11. R.I.P George we are really going to miss U!! Harrieth we pray, that GOD will give you the strength at this trying time.

    TC - The wings of Kilimanjaro

    ReplyDelete
  12. R.I.P George we are really going to miss U!! Harrieth we pray, that GOD will give you the strength at this trying time.

    TC - The wings of Kilimanjaro

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...