habari zimeingia sasa hivi toka helsinki zinasema fc bongo imeunda kamati teule ya kuchunguza sababu zilizopelekea timu yao na mashabiki kulishwa pilau dume huko sweden walipoenda kucheza na kilimanjaro fc siku kadhaa zilizopita. picha hiyo hapo juu inayotoka kwa kaka mjengwa inasemekana ni mojawapo ya vizibiti vya tuhuma hizo nzito
tume hiyo, inayoongozwa na mwenyekiti mtimkubwa, inaanza kazi yake kesho jumapili na imepewa siku 10 iwe imekamilisha. hadidu rejea za kamati hiyo ni kama ifuatavyo.
1. ni kweli pilau walilopewa fc bongo kule stockholm siku ya gemu halikuwa na nyama?
2. kama ni kweli pilau halikuwa na nyama, ni kwa nini na kwa sababu gani
3. kama kilimanjaro fc walishindwa kununua nyama pengine kwa hali ya uchumi, hata kababu ziliwashinda?
4. endapo ikigundulika kwamba kilimanjaro fc waliwanyima nyama wageni na kuzila wao wenyewe kivyao, fc bongo warivenji siku kilimanjaro wakienda kucheza finland?
5. je kunyimwa nyama na kulishwa pilau dume kuna uhusiano wowote na kufungwa kwa fc bongo bao 4-3?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. jamani, huku ulaya ukiingia dukani ukakuta chakula kimeandikwa "pilau rice" hicho ndo chakula walichopewa wadau, kwamba hamna nyama huko. Sasa inaelekea wadau lugha ilikuwa mgogoro.

    Lakini what's the big deal? kama waliona mwenyeji wao hajawapa chakula wanachotaka kwa nini wasinunue chippy si ziko kila kona?

    Na hizo nyama kama zingekuwepo, zingebadili vipi kiwango chao cha uchezaji?

    ReplyDelete
  2. Ebana Washikaji Wa Filand Mbona Mnatutoa Nishai Watu Wa Sweden?? Inawezekana Kweli Inawezekana Mwenyeketi Wa Kili FC Akabania Maana Nae Hajatulia.Tunawaomba Radhi Na Muuchune Yaishe Tatizo Ndio Hilo Mwenyeketi Wetu Mbabe

    ReplyDelete
  3. swala la 5 ndio la msingi kuna uhusiano gani kati ya pilau na 4-3,walikosa maji ya kunywa sio nyama,ila walipewa huduma nzuri hasa wale wasichana walikuja nao tuliwahudumia vizuri tu,,kili stars + bongo fc = TZ pa1

    ReplyDelete
  4. Hahaahah Majungu ya Watanzania yanaanza sasa duh wote si wa nchi moja jamani kwanini fitna na majungu? au jokes hizi kama wenzenu wazungu sijui mnajuwah uko mnasema Vegiterian pengine hawali nyama kwahiyo wamewapa chakula chao cha asili ya kwao ukija kwetu huku uzaramoni utapewa ugali wa muhogo au wali na kisamvu cha kunde huwezi nenda hotel. yamekwisha. tuwacheni kidogo majungu kama utani powa.

    ReplyDelete
  5. Pilau lilikua tamu sana jamani. me hata sikukumbuka nyama. ila tu maji ya kunawa na ya kunywa ndo lawama yangu.

    ReplyDelete
  6. Mimi ile mechi nilikuwepo, kiukweli Kilimanjaro FC walicheza vizuri, tena yule mfungaji wao mahiri alikuwa ni mwiba kwa Bongo FC. Kuhusu chakula, pilau ilikuwa na nyama za kutosha tu na ile nyama ilikuwa na taste nzuri sana, na wali mweupe na mchuzi wenye nyama vyote vilikuwepo aliyetaka kuongeza ilikuwa ruksa! Mimi siegemei upande wowote ila natoa fact kwa sababu siishi Sweden wala Finland, nilikuwa Sweden kimatembezi tu!

    ReplyDelete
  7. Afadhali hao kilimanjaro wametupa pilau, Jamaa wa Tampere wametupa vibawa viwili viwili vya kuku na viazi vipande viwili, walipokuja kwetu tuliwashibisha na marosti hevi wakala na kuvimbiwa.

    ReplyDelete
  8. Mbona hao jamaa wa Finland wanazungumzia sana msosi.Inakuwa kama wapo kwenye kambi ya wakimbizi Darfur.Mmefungwa na Kili Stars na hata mngepewa nyama kilo mia tau bado mngefungwa .Mmefungwa pamoja na refa kuwa wa kwenu bado kelele nyingi tu.Next time njooni na chakula chenu.

    ReplyDelete
  9. Nanyi Fc Bongo kwa misosi, siku nyingine mkisema timu nzima ni watu 25 mpaka 30 hii ni pamoja na viongozi nyinyi mnaleta washiriki wa Olympic watu 80 ndio maana mnapewa nyama kidogo mnataka wawahudumie mpaka washabiki wenu duh. Mdau Sweden

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...