pamoja na mambo mengine, mbunge huyu machachari alielezea masikitiko yake na ya wadau wengi juu ya hali dhaifu ya matumizi ya teknohama nchini kiasi kwamba hata karibu tovuti zote za umma hazina uendeshaji na uamgalizi wa kifanisi kwa kukosa watu wa kuziendesha na kusimamia na kuzifanya zidode kwa muda mrefu bila ya kusuguliwa (kuwa up dated).
mh. ndassa pia aliibuka kuwa mbunge wa kwanza kueleza jinsi teknolojia ya globu za wadau binafsi zinavyokuwa mstari wa mbele katika kutafuta na kutoa habari za mara kwa mara tofauti na tovuti hizo za wizara na mashirikia ya umma.
kwa niaba ya wadau wote, globu hii ya jamii inatoa pongezi za dhati kwa msimamo wa mh. ndassa ambaye ameweza kuzitamka bungeni globu zote zinazoendeleza libeneke, ikiwamo hii, na kutaka hatua za haraka zichukuliwe ili mitandao ya umma ziige mfano huu wa kupasha habari mara kwa mara.
ni matumaini ya kila mdau kwamba ujumbe mzito wa mh. ndassa utazingatiwa na tutaanza kuona matunda yake kwa mitandao nyeti serikalini na kwenye mashirika ya umma ikisuguliwa kila mara, kama si kila siku.
ahsante mh. ndassa na hongera kwa ushupavu wako wa kupasha ukweli
UNAJUA KWA MAKISIO YANGU ZAIDI YA ASILIMIA 70 YA WASOMI WA TAZANIA WANAAMINI KUWA KITENDO CHA KUWA KWENYE INTERNET KINATOKANA NA KUTOKUWA NA KAZI YA KUFANYA. UKITIZAMA MAONI YALIYOKUWA YANATOLEWA WAKATI TANZANIA INATOA PONGEZI KWA MANDELA KUTINIZA MIAKA 90, WASOMI HAO AMBAO WAKO BIZE WALIDAI WATANZANIA HAWANA KAZI ZA KUFANYA WANAPOTEZA MUUDA KWA KUTOA HIZO PONGEZI.
ReplyDeleteKichwa cha habari kingekuwa ivi "Mh Ndasa aipa shavu blog ya Mithupu mjengoni".....watu wapo busy kutembelea blog ya michuzi, Michuzi ni mwandishi wa habari mmoja maarufu mjini...watu wanatembelea blog yake kuliko web za serikali coz Mithupu ana uptodate kila wakati
ReplyDeleteNakubaliana na wewe Tumaini, back in da days when net iliingia niliwahi kuwa cristised na boss wangu kwamba naganda sana kwenye pc sina kazi IoI imagine she was HR nilipewa msg na deparmental boss na nilipokea kwa masikitiko sana ingawa by then si wengi walijua hii kwa Technology ila mpaka leo Bado matumizi ya Internet sio yenyewe kwa wabongo wengi ndani ya bong na hata nje ya bongo as well sijui wanaogopa mimi sielewi kwa kweli but Ukiishi huku wanapojua kutumia mitandao utajua nini maana yake you just select, click unatoa details after few seconds unasikia jamaa yuko mlangoni kwako. Sasa hii inatakiwa kupewa somo watu wote kama unavyomwambia mtoto apige mswaki asubuhi ni lazima.Kungekuwa na policy kila sector ya serikali lazima iwe na tovuti inayokwenda na wakati wafanyakazi wawe na e-mails sio za yahoo wala hot..za the same org. company watever database ya maana ku-keep data na archival...a good info. system ya communication within and outta org. sio memo za katarasi kila siku wakati mnalalamika miti inaisha na mazingira yanaharibika lazima wafanyakazi wawe-active kucheki e-mails na kureply every time sio kwa wiki maa moja IoI Hatutafika ila hapa naona kama unampigia mbuzi gitaa... am out
ReplyDeleteLondoner