Mambo Michu,

Hiyo pick-up siyo kama imepaki ila imezuiliwa kuondoka baada ya dereva wake kujitia ukichwa maji kwa kutaka kulazimisha kupita wakati mtaa umefungwa, bahati mbaya alisahau kama nyuma amebeba bomba refu linalozidi urefu wa turubali.

Ile kushtuka hamadi! bomba likachana turubali na kuliburuza hatua chache mpaka anafunga breki tayari alishasababisha madhara! bomba za stendi ya turubali zilipinda na bomba moja ikakwaruza gari ndogo iliyopaki pembeni kulia bahati haikuvunja kioo! na gari yake nayo ilipata michubuko kidogo. Dereva(aliyesimama mwenye jinzi na raba nyeusi) alisalimika kichapo baada ya kuomba radhi lakini alilazimika kugharamia hasara aliyosababisha.

Tukio hili lilitokea jana baada ya swala ijumaa katika mtaa wa Mafia jirani kabisa na msikiti wa Manyema, turubali hilo liliwekwa kwa ajili ya shughuli ya kisomo cha Bi Mboni Mtambo mwanamama alwatan mitaa ya Kariakoo aliyefariki mwezi uliopita.

MR. AHMED VIRIYALA
Creative Director,
CUTE DESIGN.
Cell: 0754 296085
Tel: 2181218
or
0732 921445
Website:
www.cutedesign.co.tz
We are dealing with:
Advertising Agency, Publishing, illustrations,cartoons, Graphics Designing and Printing of everything from Billboards to brochures, Annual Book Report, magazines, t-shirts, wheel covers and etc.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...