Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akimsalimia mmoja wa watoto wakati alipotembelea kituo cha watoto yaitma na wasiojiweza cha Nyumba ya Amani na Furaha cha Mburahati jijini Dar jana


Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na wazee wakati alipotembelea kituo cha kulea watoto yatima na wasiojiweza cha Nyumba ya Amani na Furaha cha Mburahati jijini Dar jana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hiki kijiji mbona ndo leo nakiskia. Heby tumuvuzishie shughuhuli zake ili nasi huko mitaani kwetu tukimit na watu wenye matatizo kama haya tuwaelekeze.

    ReplyDelete
  2. Hivyo ndivyo itakiavyo kuwa, hii ni sehemu ya Kanisa Katoliki kama sikosei, ni sehemu ya kuwatunza wazee na watoto yatima n ya siku nyingi sana toka hata kabla ya uhuru. Serikali pia inatakiwa iwe na vituo kama hivyo si Dar tu bali nchi nzima chini ya Wizara ya Ustawi wa JamiI. Watoto yatima na wazee wanatakiwa kulelewa na serikali ndo maana watu wanalipa kodi si kwa ajili ya mishahara ya watendaji wa serikali na semina zao tu bali kwa mswala ya jamii pia! Serikali lazima ichukuwe hiyo kama changamoto kwao, pamoja na dini zingine na madhehebu mbalimbali zinaweza kufanya hivyo na wapatiwe ruzuku na serikali na iwe kila mkoa si Dar tu, kuwe pia na Vyuo/College zinazofundisha na kutowa nondozz juu ya kulea yatima na wazee wahitimu waajiliwe kwenye sekta hiyo, pia watu binafsi wanaweza kuanzisha biashara ya kulea yatima na wazee na watu wakufanya bishara hizo ni lazima wawe wamesomea maswala haya ya malezi na malipo ya biashara yao yafanywe na serikali sio clients wao kwa vile hilo ni swala la jamii, pia kuwe na wakaguzi watakao kuwa wanagaguwa standards, mfanyabishara akizembea hizo standards ashitakiwe na kufungwa pamoja na faini na kunyang'anywa leseni. Mambo kama hayo hufanyika sehemu sana na ndo kawaida kwa baadhi ya nchi hapa duniani.

    ReplyDelete
  3. Kaka Michuzi,

    Hii ni kati yangu mimi na wewe.

    Hivi Umeshawahi kukitembelea kituo hiki siku ambayo sio jumamosi, jumapili na wala sio siku ya wageni au sikukuu? hebu jaribu siku moja ujifanye wewe ni mtu tu wa kawaida na usiulambe pamba wala usiende na kamera, halafu ukaone ni jinsi gani watoto na wanaolelewa katika kituo hicho jinsi wanavyopata taabu ni tofauti na unavyoona au kusikia kwamba kituo hicho kinawalea vizuri. Naomba tu uifanye hii kazi kwa muda wako halafu utajionea mwenyewe, kwa maana hao watoto ni YATIMA MARA MBILI, kwa lugha nyingine HAWANA UNAFUU WOWOTE na hakuna AMANI WALA FURAHA. Mama Theresa kaondoka na AMANI YAKE.

    Mwenyezi Mungu Awasaidie.

    ReplyDelete
  4. Nadhani kiko kwenye 'rada' kwa muda mrefu tu, ila nadhani hawapendi attention na kuna utaratibu maalumu wa kutembelea hicho kituo. Jina maarufu au linalotumiwa zaidi ni 'Mother Teresa' na huwezi kupotea.

    ReplyDelete
  5. Hicho kijiji kipo toka miaka ya 70 kama sikosei. Ni ya Mother Theresa hasa. Naye alikuwa hana makuu.

    ReplyDelete
  6. Mchukueni na Mzee Matonya basi. yeye si kama mnavyomzushia baadhi yenu eti ana ng'ombe na tajiri wa kupindukia. Ni mzee, kipofu na masikini. Acheni kumtania hana tu wa kumsemea shida zake. Mkuu wa kituo mlete umhifadhi hapa tafadhali.

    ReplyDelete
  7. BIG UP to those who cares for those in needy.
    They do not do it for "show", so anon 6.55 be careful with what you are saying.
    Kama umeona hakuna AMANI WALA FURAHA, unaonaje kama ukichangia kuweka hiyo AMANI NA FURAHA.
    Hata MOther TEREZA kabla hajatutoka walisema anaendekeza umaskini badala ya kusaidia watu kuacha umaskini. Hiyo siyo kazi ya hao masista, their duty is to love and see CHRIST in others to the extent they can.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...