Rais wa Comoros Mh. Ahmed Abdallah Mohamed Sambi leo asubuhi anatarajiwa kulihutubia Bunge, kwa mujibu wa Spika Mh. Samwel Sitta.


Mh. Sambi, ambaye ataambatana na mwenyeji wake JK, atalihutubia Bunge mara tu bada ya kipindi cha maswali na majibu milango ya saa nne unusu.


Rais huyo wa Comoros anatarajiwa, pamoja na mambo mengine, kutoa shukurani zake na za wananchi wake kwa Tanzania kwa kuongoza jeshi la Umoja wa Afrika katika mapambano yaliyofanikisha kuung'oa utawala wa kanali Mohammed Bacar katika visiwa vya Anjuani mapema mwaka huu.


Baada ya mgeni huyu kuondoka, Bunge litaendelea kujadili hotuba ya bajeti ya makadirio ya Wizara ya Fedha na Mpingo ambapo Waziri Mustafa Mkullo kuhitimisha baadaye jioni.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Huyu MEMBE anasema Tanzania itajiunga na IOC (JUMUIYA YA NCHI ZA KIISLAMU), na akasema Tanzania itafaidika na mafuta kwa bei nafuu, lakini watu wanataka kujuwa IOC ni nini na madhumuni yake nini, yaani ilianzishwa kwa sababu zipi? ni kwa ajili ya mafuta raisi tu au kuna mambo mengine, mara nyingi nchi kabla ya kujiunga na jumuiya yoyote lazima wananchi waelezwe kwa uwazi hicho kitu wanachojiunga nacho ni nini na kina faida gani kwa section yote ya wananchi husika, I MEAN THE BENEFIT ACROSS THE WHOLE SOCIETY. Kama vile tulivyojiunga na UN, AU, SADC nakadhalika, nadhani kila mtu anajuwa umuhimu wake wa kijiunga na jumuiya hizi nilizotelea mfano. Hivyo ni jukumu la BENARD MEMBE kutueleza wananchi kinagaubaga ni nini IOC na madhumuni yake ni nini kwa kupitia vyombo vya habari vyote kiwazi na watu wakaelewe, UMASIKINI USITUFANYE TUJIUNGE NA JUMUIYA SIMPLY BECAUSE TUTAPATA MAFUTA KARIBU NA BURE, our country is a non-religion, sasa kujiunga na jumuiya inayohusisha dini naona kuna walakini hapo hata kama hiyo jumuiya ina manufaa 100% kwa watanzania wa dini zote! kunaweza kukatokea tatizo la kisheria hapo mbeleni na tukaulizwa kwani nyinyi hamna wanasheria na hawajuwi kazi zao, kama vile Rais alivyosema bungeni kuwa siku zote tufuate sheria tusijejiingiza mkenge.

    ReplyDelete
  2. Hadi Laha--wangazija bungeni!!!!!

    ReplyDelete
  3. Hata mimi nakuunga mkono kuwa haiwezekani membe atupeleke kama kondoo au kama alivyofanya mkapa kuweka mikataba ya kuiibia nchi,isiyonaukweli.

    tena ikiwezekana swala hilo lipingiwe kampeni watu wapige kula. nchi si ya wachache bali ni ya wana nchi wote. kunamsemo unasema bule aghali sioni umuhimu wa kuleta uroho wa mafuta na kujiunga na nchi za kiislam hilo taifa si la udini.

    ReplyDelete
  4. Pia tupige kura siku ya kupumzika iwe Jumapili au siku nyingine iili haki itendeke.Kwanini iwe Jumapili tu????

    ReplyDelete
  5. MUNGU WANGU, kale kanyama kanakoitwa udini bado kako hai. Mbona nchi nyingi za kiafrika za kisekyula zimejiunga OIC kwa sababu za kiuchumi tuu. Hapa udini utatufikisha mbali pabaya.

    Maana hawa matajiri wa kiarabu wanatoa mikopo isiyo na riba/interest tofauti na nchi za magharibi ambazo hutukamua hasa.

    Haya maswala kama watu walienda sunday school wakaiva au madarasa si uwanja wake huu. We unafikiri wataalamu ni wajinga au nchi nyengine kama DRC ni wajinga kuwa OIC?

    Unazungumza kura, hii siyo siasa ni uchumi hivyo wataaalamu ndio wanahusika zaidi.

    Haya maswala ya kuwa extremist hayafai, kuamua mambo kwenye nchi ya kisekyula kwa misingi ya kidini. (Namaanisha hatuwezi kuancha kuinyonya OIC eti kwa sababu kuna hisia za kibinafsi za dini ya kikristo). Mbona serikali ikikopa kwenye mashirika ya kikristo waislam hawasemi? Cha msingi ni manufaa kwa nchi nzima.

    Hapa watu watapata mikopo ya kufanya biashara na kujisomesha elimu ya juu.

    ACHENI UDINI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...