CHAMA CHA MAPINDUZI

Shina la Reading

MKUTANO WA WANACHAMA WA SHINA LA READING

Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Wanachama Wote - C C M - Reading
Wakereketwa Wote - C C M - Reading
Wapenzi Na Wana-Mapinduzi Wote

Tarehe: 31/08/2008 Saa: 7 Mchana – Saa: 11 Alasiri

WAPI:
UKUMBI WA: 79 (Kijiweni)
79 LONDON ROAD
READING
RG1 5BY

Kwa ufafanuzi zaidi, tafadhali wasiliana na:

MAIRA MIGIRE - 07799212095
Katibu wa CCM Shina la Reading

Watanzania Wote Mnakaribishwa

Tafadhali Wataarifu na Wengine

Kiingilio - BURE!!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Ndugu zangu samahani, mbona matawi ya chama tawala yameibukia sana hapo ukerewe!!!!! KULIKONI?? Mnatutia shaka na kutukwaza baadhi yetu tulio ughaibuni. Inamaana Japani, Australia, hata mali au Bukinabe ama kokote kule ughaibuni hakuna wabongo??? Mbona sijaona mikutano ya chama tawala na kufungua matawi??? hebu tupeni siri na utamu wa matawi haya, labda mwapata ruzuku yoyote? Ama kweli mwataka kutuambia nyie wenzetu wa ukerewe kweli kweli chama kipo damuni. Samahani wadau wa Blog yetu ya jamii, naomba msaada juu ya jambo hili. Kusema kweli linanikwaza!!!

    ReplyDelete
  2. HUYU HAJUI CHOCHOTE KILE ,ILA MATAWI YAPO MENGI TU HATA UGANGA ,INDIA ,KWA WEWE WASILAINA NA MAKAO MAKUU UPEWE SOMO.HAKUNA PESA ILA TUNASAIDIANA NA PIA KUPASHANA HABARI ZA NYUMBANI.

    ReplyDelete
  3. Sina uhakika lakini nahisi si sheria na kinyume cha sheria ya nchi kuanzisha tawi la chama nje ya nchi, nadhani hata katiba ya nchi nahisi imeeleza hili na hata katika ya CCM pia imeeleza hivi, pia tume ya uchaguzi miongozo yake imeeleza hili pia, kwa hiyo si sahihi kuanzisha shughuli za kisiasa nje ya nchi, pia nahisi wanavunja sheria za UINGEREZA pia sidhani kama zinaruhusu kuanzisha tawi la chama cha siasa hapa UK. eBU FANYENI UCHUNGUZI WA HAYA NA HII NI CHALLENGE KWENU BE SO CAREFULLY. msije mkawa mnachafua integrity ya chama chenu/chetu

    ReplyDelete
  4. pia mjiunge na umoja wa nchi za kiislam

    ReplyDelete
  5. Njaa ni kitu kibaya sana........

    ReplyDelete
  6. katiba ya CCM inaruhusu kuwa na matawi ya nje ya nchi, haya matawi yanayofunguliwa nje ya nchi hayako kinyume cha sheria. kama unataka kuhakikisha soma katiba ya CCM

    ReplyDelete
  7. Kweli wabongo hatuna deal, nyumbani hatuna deal na tukiwa ugenini hatuna deal vile vile. Ukerewe leo tumekosa la kufanya tunahangaika kufungua tu matawi ya CCM. Mimi nilifikiri tumekuja huku kupanua mawazo na kusimama imara kuikosoa CCM ambayo haina mwelekeo zaidi kuwaibia walalahoi.
    Kweli njaa ni mbaya saana ila njaa ya mawazo ndo mbaya kuliko zote

    ReplyDelete
  8. HIVI UKEREWE SIKU HIZI SHUGHULI ZA ZA MABOX ZILIISHA NINI? MBONA NAONA WATU WANAFUNGUA MATAWI YA CCM KILA KUKICHA

    PAMOJA NA UFISADI CCM INAOFANYA BADO WATU MNAZIDI KUPANUA WIZI TU!!!
    AU NDO MISEMO YAO WAKEREWE "IF YOU CAN'T BEAT THEM, JOIN THEM"

    MDAU, US

    ReplyDelete
  9. misikubaliani na hii kitu kabisa,kwanza kibaya kuliko yote wengi wa wanachama hasa wa matawi ya uk walijiripua ili kuweza kuishi huku.Sasa kama mliweza kuikana nchi ili mjikimu na shida zenu,tutawaamini vipi kuwa viongozi wetu wa baadaye na nyinyi si ndio mafisadi wenyewe au niwaitaje?waoga wamaisha mkirudi nyumbani ndo mnafikiri mtapata madaraka kiraisi mnakera sana kwakweli!sikumoja ntawastua wajomba kwenye vikao vyenu tuone kama kweli nyinyi ni watanzania halisi nyi endeleeni tu!!!!!

    ReplyDelete
  10. CCM should be careful about this and thing again. Hivi na Chadema, CUF etc etc wakianza kufungua matawi nje ya nchi si ndio kuanza kukuza magaidi?

    Sijui siku wapinzani nao wakiibuka na vyama vyao nje ya nchi mtawakataza au mtawalaumu nani?

    Hivi vyama nje ya nchi nani anavisponsor au nobody cares about that. Siku wapinzani watakapoanza kufungua matawi na kuwa sponsored na magaidi watu watajiuliza kwanini hatukuona this one is coming. Kila siku mikutano ni nani anwapa hela za kufanya hiyo mikutano. I hope sio hela iliyotengwa kwa mambo ya embassy.

    Nawaonea huruma watoto na vizi vijao...


    halafu huyo anayesema sijui vipo vyma india na uganda vingi tu mbona USA hamna na wakati USA inaongoza kuwa na raia wengi wa tanzania nje ya nchi? Ina maana huku hamna wakereketwa?

    ReplyDelete
  11. Wazo la anonym. wa 6.45 la kuwastua wajomba wawaingilie kwenye vikao naliunga kwa asilinia 100%. Mimi binafsi nipo Bongo kwa vakesheni ya two weeks, kisha narejea huko Ukerewe, na sio siri naishi hapo hapo wanapotaka kufanyia vikao vyao. Nitajua nini la kufanya,siwatishii, ila mnatutia aibu watu wa Ukerewe, huku nyumbani watu hawatuelewi hata chembe. sisemi mengi, ila mtasikia habari yao.

    ReplyDelete
  12. Matawi ya CCM hayapo USA kwasababu wadau wa USA wana akili kushinda wa UK.

    USA tuna bash za watanzania hata siku nyingine tusheherekea uhuru wa jirani zetu Kenya kuliko hao wa UK wanaoshabikia ukoma

    ReplyDelete
  13. Bora wa UK wanaenda kwenye CCM nyie wa USA mnauwana kwenye bash zenu hizo

    ReplyDelete
  14. Hihihi Job True True!!! Yaani Nyie Hamjastukia Picha Bado?Matawi Ya CCM Yanaundwa Katika Nchi Ambazo Vigogo Wamepeleka Watoto Wao Kusoma.Na Hii Ni Kuwaanda Watoto Wao Ili Wakirudi Moja Kwa Moja Bungeni Na Wizara.Hakuna Mtaji Mzuri Kama Siasa Tena Ya Bongo.Mbona Matawi Hayo Yako India.USA na UK? Huwezi Kuta Uchafu Huo Kwa Wazungu Wa Roho Kama Italy,Holland,Sacandnavia Sababu Hakuna Watoto Wa Vigogo...Hihihi Job True True..Ni Mdau Wenu Mpindisha Shilingi

    ReplyDelete
  15. NJAA TUPU, KAMA ALIVYOSEMA ANON MMOJA HAPO HAKUNA KITU KIBAYA KAMA NJAA YA MAWAZO. UK HAWANA CHOCHOTE WAJUACHO KWAHIYO WANAKIMBILIA CCM. (CHUKUA CHAKO MAPEMA) HOPING ONE DAY NAWAO WATAPATA CHAO MAPEMA. NYIE MMETOKA NJE YA NCHI BADALA YA KUJIEMDELEZA NA MAMBO YA MAANA MNAFUNGUA SHINA LA CCM KWANINI MSIFUNGUE UMOJA WA WATANZANIA KAMA KWELI MNAPENDA NCHI NA UMOJA. SOTE TU WATANZANIA BALI SOTE SI WANA CCM. NA HIYO EMBASSY SI YA CCM NI KWA WATANZINIA. KESHO NA KESHOKUTWA CCM IKITOKA MADARAKANI I WONDER KAMA HAYO MATAWI YA CCM YATAENDLEA KUWEPO.

    ReplyDelete
  16. kweli kabisa nawaunga mkono anons. Hao wanachama wengine wamejiita wakimbizi ili wapate status za kukaa Uingereza na wengine status zao hazieleweki. nina uhakika officers wa home office wangependa saaaana kukutana na watu wa aina hiyo. Je ni vipi kama mtu akiwatonya BBC news kwamba kuna watu ambao wanajiita wakimbizi au wana asylum status lakini pia ni wanachama wa CCM na wanahudhuria mikutano yao kwenye branches za CCM hapa UK? oh dear! I can even see the headlines.

    ReplyDelete
  17. 1.kama kweli nyie ni viongozi safi na si wasaliti wa nchi tunaomba kujua status ya huyo katibu mkuu wenu.asije kuwa katoka (burundi,ruanda,congo,somalia e.t.c)
    2.inabidi bunge litunge sheria kudhibiti hawa watu wanaojilipua na kuingia kwenye siasa.
    maana watu kama hawa tayari inaonesha jinsi gani wasivyokuwa na uzalendo na nchi.

    ReplyDelete
  18. Please huko Ukerewe naomba mfanye kweli mkigundua siku za hivi vikao muwaitie uhamiaji. manaweza hata kusema kuna magaidi wanakutana mahali ili ipate uzito unaostahili. Na ni magaidi kweli kwani wanaua nchi, ulishasikia bei za umeme zilivyopanda? Na bado wanataka kupandisha tena kwasababu ya wajanja wachache ambao bado hawako jela?

    ReplyDelete
  19. USA KUMEJAA MABISHOO NA MASISDA DUU, SIASA YA TANZANIA WATAIJULIA WAPI.!!!!!

    ENDELEENI MAWASOMI WA UK KUENDELEZA LIBENEKE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...