Hi Wadau wa globu ya jamii,
Mwanaharakati, msanii na mwanamuziki wa ki-Tanzania, Ras Nas au Nasibu Mwanukuzi amewasha moto wa kiutu-uzima kwenye fani ya muziki Norway kwa kuwa msanii mwa-Africa wa kwanza nchini humo kupata nyota tano kwenye marudio ya albamu yake “Dar-es-Salaam” toka gazeti kubwa la Dagsavisen.
Hii inadhibitisha kwamba wabongo nao tupo!
Ukitaka kuangalia shoo live ya Ras Nas unaweza kubonyeza Youtube: http://www.youtube.com/user/rasnas55
(hapa kuna video tatu: 1.River Nile 2. Dar-es-Salaam na 3. Guantanamo) Asanteni,
Kongoi Productions


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...