wawakilishi wetu kwenye michezo ya olimpiki huko beijing, china, wakiwa katika gwaride la ufunguzi jana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Imejitahidi kuwa hapo hongera.Ila kuna suala la mavazi, je walishindwa kuvaa kitu cha kuonyesha uafrika?nimeona nchi nyingi tu za afrika zimefanya hivyo,sasa kuvaa just a t-shirt kwakweli siamini kama walishindwa kuvaa japo hata mashati ya vikoi kama si vitenge, etc Viko vitu vingi vya kuvaa vya kiafrika kama si ki-tanzania basi!Sijui lini tutakuwa serious kuitangaza nchi yetu!?!?

    Mdau

    ReplyDelete
  2. Mdau wa hapo juu suala siyo kuwepo suala ni kushiriki kikamilifu tuache mambo ya kuji -please kwani nchi kama Zimbabwe iliyoko taabani(inaongoza kwa hyper inflation in human being history) inapata medal sisi tunaopandisha uchumi eti kwa asilimia 5 kila olympic games tunashiriki hakuna kitu miaka zaidi ya 30 bila medali halafu unasema eti hongera kwa kuwepo suala siyo kuwepo ni kushirika na kushinada kwani siye tuna tofauti gani na kenya jirani zetu wa karibu ambao most of them wanatoka kwetu umasaini...
    Ukija suala la representative siye ndiyo tulio kuwa wa mwisho katika gwaride la ufunguzi...suala siyo vazi la kiafrika nchi nyingi zilivaa safi na siyo mambo ya vitenge who told you that vitenge is our traditinally dressing...???nchi nyingi za africa zilivaa mavazi safi bright colour ,kofia nzuri ,viatu safi sare, siyo mambo ya bongo, hao wana michezo wenyewe wamechoka ile mbaya ukiweka na mavazi basi ilikuwa ni kasheshe..jamani yaani nchi inakosa fungu la kuandaa wawakirishi wa olympic kiasi kwamba mtu unaona aibu kumwambia mke wako au jirani zako angalia national team yetu ya olympic eti aahaa sie ni nchi maskini ,Tanzania siyo maskini kuliko Mali ,Burkinafasso au Tongo..halafu mtu anaweka heading eti watanzania wamelemeta...jamani kweli sie ni kichwa cha mwenda wazimu kila mtu anajifunzia kunyoa.kwetu.
    MKELEKETWA ..
    MDAU WA KARAGWE.

    ReplyDelete
  3. huyo mzimbabwe ni mwelsh. hata zim hakujui. huyo wa Togo ni mfaransa we pantoni na togo wapi nawapi? . ila what they have in common ni ??? DUAL NATIONALITY ambayo sisi hatuna.

    ReplyDelete
  4. mimi nimeangalia michezo mingine nikajiuliza kwanini bongo hatukuzi vipaji hivyo? Kuna michezo mingi wala haaitavi vifaa au mambo mengi ya kusema kuwa hatuna uwezo...Jamani beach volley ball kweli tunashindwa kushiriki? Diving...moto hiyo na maporomoko kila siku tulikua tunadive tukiwa wadogo kweli hatuwezi kukuza vipaji hivyo? Yaani kuna michezo mingi tu na sio kwa ajili ya jina ni kwa ajili ya ajira. Nimeona watu wengi walioshiriki wakashinda shinda Sidney na Athens sasa hivi wanajishindia maisha USA. Kwa hiyo kushiriki sio kukuza jina la nchi tu bali pia kama mtu akijituma ndio njia ya kuchomoka....Na ukichomoka basi ni kama tunaexport ujuzi nje ya nchi na huyo mtu ataleta maendeleo nchini kwetu.

    ReplyDelete
  5. nami naunga mkono wangeshona hata mavazi ya vitenge ingekuwa poa...nilikuwa naangali na wazungu wakaniuliza vipi bongo hamana vazi la kitaifa kama nchi nyingine za Afrika?nikashindwa nini cha kujibu.....
    man_lion

    ReplyDelete
  6. yeah, mavazi yao sucks big time. hawakuwaona wenzao wa-nigeria na ma-babangida yao?

    ReplyDelete
  7. mimi niliwaona wa tz waliowakilisha hawakuwa hata na furaha wao binafsi, tofauti na nchi zingine walikuwa wakipungia mikono na kuonyesha furaha yao.

    pia ma rais wa nchi zingine walikuepo kusapoti nchi zao ila viongozi wa kiafrika wanajikosesha raha hata wao kwani kama uko proud na nchi yako mbona hutokei kama wengine???

    unajuwa some time tuna ji full wenyewe kwa uongozi mbaya. raia wamekonda kama wanakula simenti uliona wapi na nchi ya tz ndiyo inaongoza kwa rutuba lakini wapi, inasikitisha sana

    huwa inaniuma natamani hata kulia ila basi tu waacheni waikongorowe nchi hiyo mpaka mwisho

    ReplyDelete
  8. Siku hizi Wabongo "tumeendelea sana" hatutaki mtu atwambie mambo ya vitenge au vikoi, sijui khanga, ooh baibui au suti za kaunda. Ni suti ya ulaya na tai mpaka misibani bila kusahau T-shirts na blue jeans kwenye gwaride la Olimpiki!!! Mungu atupe nini? debe la kunguni? Msitake kuturudisha nyuma. Tulichelewa kidogo ngoja nasi tufaidi matunda ya waliostaarabika.

    ReplyDelete
  9. niikua naangalia opening ceremony walipofika bongo ikabidi nishike mdomo kwa butwaa, nani huyo aliyewaandaa jamani hata formal dressing imekua issue!

    ReplyDelete
  10. mungu ibariki tanzania hawa jamaa wamedhalilishwa vibaya sana na taifa hili yaani hata hao viongozi hawaoni kama hawa jamaa wanakwenda kusimama mbele ya dunia kuiwakilisha tanzania au ni watu ambao hajastaarabika kuelewa kwamba ilibidi tuonyeshe our best to the world

    ReplyDelete
  11. i am curious to know ni officilas wangapi waliokwenda na wachezaji wetu huko beijing. bila shaka idadi yao itakuwa imezidi wachezaji wetu. ni mpaka lini tanzania tutakuwa tunafikiria matumbo yetu badala ya kuwa na uzalendo? hizo nguo wachezaji wetu walizofaa siku ya ufunguzi zinatia aibu. siyo siri sisi hatuna vazi lakitaifa, lakini hiyo siyo issue, walitakiwa kuwa smart tu na siyo kuvaa vi t-shirt kama wacheza mpira wa miguu. wachina wenyewe wana vazi la kitaifa lakini wenyewe walivaa blazer nzuri na walipendeza kweli kweli. anyways i wish the team well and i hope watarudi na at least a ka bronze!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...