Idadi ya watoto waliokufa katika maafa makubwa kuliyo yote kuwahi kutokea katika sikukuu ya Iddi El Fitr nchini huko Tabora imefikia 20, baada ya kufariki leo mmoja kati ya watoto 19 kufariki dunia jana kwa kukosa hewa katika ukumbi wa Disco wa Bubbles.
Akithibitisha hayo leo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimusa, alisema kwamba watoto waliokufa wanakisiwa kuwa na umri wa kati ya miaka 7 na 18 na walikuwa katika 'Disko Toto' iliyokuwa imeanza majira ya saa nane mchana.
Amesema kwamba wahanga hao walikumbwa na maafa hayo wakiwa wanasheherekea sikukuu ya Idd El Fitr kati ya saa 11.30 hadi 12.15.
``Nilipoenda katika ukumbi majira ya saa 12 ndipo tukaanza kuondoa miili katika ukumbi. Walikuwapo waliokuwa wamezimia pia,`` alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Alisema kwamba kati ya waliofariki wanane ni wavulana na 11 ni wasichana.
Mwinyimusa alisema tayari maiti 16 zimetambuliwa na ndugu zao na watatu bado hawajatambuliwa.
Maiti wote wamehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Tabora. Alisema miongoni mwa maiti ambazo hazijatambuliwa, wawili ni wasichana na mvulana mmoja.
Mkuu wa Mkoa alisema watoto 16 wamelazwa katika hospitali ya mkoa, watatu kati yao hali zao ni mbaya. Alisema baada ya kuitisha kikao cha kamati ya Ulinzi na Usalam cha Mkoa, ameunda kamati ya kuchunguza tukio baya kuliko yote kuwahi kuukumba mkoa huo, ikijumuisha Polisi, Usalama wa Taifa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Tanesco.
Rais Jakaya Kikwete amekwisha kutuma salama za pole na amemteua Waziri wa Kazi, Ajira Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, ambaye ni mbunge wa Urambo Magharibi, kuwakilisha serikali katika msiba huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. 20 wafa katika dosko toto tabora....Balozi Mithupu, dosko au disko??
    Nawapa pole wafiwa wote, Allah awape imani kwenye wakati mgumu kama huu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...