Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo (Jumatano, Oktoba Mosi, 2008) ametuma rambirambi, na kutoa mkono wa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimusa, na wana-tabora wote kufuatia vifo vya watoto 19 vilivyotokea jioni ya leo katika ukumbi wa Jengo la NSSF lililoko mitaa ya Shule na Jamhuri mjini Tabora.

Katika rambirambi zake, Rais Kikwete amesema kuwa amepokea kwa mshituko mkubwa habari za vifo vya watoto hao, na pia amehuzunishwa na kusikitishwa mno na msiba huo wa watoto hao wenye umri kati ya miaka mitano na 12, ambao wamepoteza maisha kwa kutokana na msongo wa pumzi na kukosa hewa.

Rais amesema kuwa mawazo yake yote yapo na wazazi na familia za watoto hao ambao wamepoteza maisha wakati wakicheza disco la watoto katika kusherehekea Sikukuu ya Idd Et Fitr.

“Nimepokea kwa mshituko mkubwa, huzuni nyingi na masikitiko yasiyokuwa na kifani habari za vifo vya watoto hao wasiokuwa na hatia, ambao walikuwa wanasherehekea Sikukuu ya Idd El Fitr kama tulivyokuwa tunafanya sisi sote leo,” amesema Rais katika rambirambi hizo na kuongeza:

“Mawazo yangu yote yako kwa wazazi na wana-familia wa watoto hao katika kipindi hiki kigumu cha huzuni, majonzi na msiba mkubwa. Tunawaombea kwa Mwenyeji Mungu waweze kuwa na uvumilivu na kupitia katika kipindi hiki kigumu sana.”

Rais Kikwete amesema kuwa ni matarajio yake kuwa vyombo vya sheria vitachunguza kikamilifu na ipasavyo vifo vya watoto hao na kuchukua hatua zinazostahili.

Rais pia amemtuma Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo, Profesa Juma Kapuya kuiwakilisha Serikali katika msiba huo mkubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. sue those people to their last dime man....Poleni na inasikitisha na inakuaje watoto wa miaka mitano wakachezeshwe disco na watoto wa miaka 12 humo humo?

    jamani aibu ...ni nchi zingine hao watu wangefilisiwa kishenzi ...kumbukeni kule new england wale watu walivyoungua kwenye night club....sheria na sheria tu


    watoto wote hao kisa kukosa hewa. alikusanya shilling ngapi siku hiyo? Huu mchezo wakutokuwa na regulations zozote ndio haya......mpaka jambo litokee baya ndio uchunguzi unafanyika....tooo late roho za watu zimeshaondoka hapo. wekeni sheria kwenye mambo membi tu na muhakikishe inafuatiliwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...