ali kiba akicheza na mashabiki wake washingon dc
cinderella akipagawisha wadau
palikuwa hapatoshi
kama kawa
Mwanamuziki maarufu kutoka Tanzania Alikiba, ameanza tour yake ya Marekani kwa kishindo baada ya kuwaburidisha mamia ya washabiki wake kwa takriban masaa mawili huko Washington D.C.

Hakuna aliyehudhuria hii show asiyekubali kama kijana amekubalika na ana kipaji. Alikiba ataendelea shows zake kama ipasavyo

09/06 Minneapolis Mn,
09/13 Houston Tx,
09/20 Atlanta Ga,
09/27 Wichita Ks,
10/04 New Jersey.
10/11 Baltimore Md,
10/18 Kansas City Ks,
10/25 Dallas Tx
na show ya mwisho 11/01 Boston Ma....
usingoje kusimuliwa hakikisha unajionea mwenyewe,
Alikiba is the best thing out of East Africa right now.

Kwa maelezo zaidi nenda
alikibausa.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. MBONA WAKO BARAZANI KWA MTU, AU HUU NDIYO UKUMBI MKUBWA ZAIDI HUKO MAREKANI? WAMAREKANI WEUPE MBONA HAWAONEKANI? AU KWENYE KAMERA HAWAWEZI KUONEKANA SHAURI YA WEUPE WAO! KWANINI TUNAPENDA KUTUKUZA SANA KITU HATA KAMA HAKIJA KIDHI? KWANI BILA KUTUMIA NENO KUPAGAWISHA HABARI HII ISINGEKUWA NZURI?

    ReplyDelete
  2. inachefua tu mavazi kwa kina dada!!sijui kuvaa uchi ndo kupendeza!mi sielewi kwa kweli!!

    ReplyDelete
  3. Samahani naomba kuwauliza nyie wa USA.

    Ina maana washabiki wote wamepanda jukwaani? au ndio mambo ya DC kwenda na wakati stage siku hizi hazina mpango?

    mmmh kama hapo ndio DC ukumbi uko hivyo je kwangine hali ikoje?

    mmmh...

    Haya ali kiba hongera kwa "BONGE LA SHOW" ulilofanya.....lol..

    ReplyDelete
  4. Edwin Ndaki.
    I see your point on the performance stage and crowd but with all due respect, you cannot mock Ali Kiba kwa kusema "bonge la show" wakati yeye ni msanii.
    He is/was not the promoter or organiser for that particular event.
    Yeye kaenda kufanya kazi yake to the best of his ability with what was offered to him.
    So i dont see why you should mock him in a statement like that. You could probably direct your concerns to the promoters/organisers.

    As for the promoters, c'mon now !!!!
    The lights are ALL ON, there seems to be no order or barriers for crowd control. Mbona hivi jamani ??? i thot ya'll said US was going to host the best Ali Kiba show ???
    As for Ali K, do your thang man and make that paper.

    ReplyDelete
  5. kwani huo ni ukumbi au parking ya magari ? halafu ndo nini kucheza na mavikombe ya plastiki mkonono? mi nilifikiri wenzetu wako juu kumbe ushuzi mtupu ? bora huku kwenye vyumbi

    kwekweli hiyo ni parking ya magari nachoka mie

    ReplyDelete
  6. Show si stage jamani.Kwangu mimi naona kujimix na wageni ilikuwa fresh zaidi. Tukubali kijan akipaji anacho....tusaidiane kuikuza Tanzania tusirudishane nyuma..Ally Kiba JUUUUUU..naona an ashow nyingi hapo USA...

    ReplyDelete
  7. Apo yupo on stage!!!! anapagawisha!! dah unyamwezini kweli noma.....

    ReplyDelete
  8. Mwenzenu huwa najua ulaya kuna mavazi mazuri kumbe uchuro tu! Yaani aliyependeza ni huyo anayeiba .. Ali Kiba

    ReplyDelete
  9. astaghfirullah............
    hivi huyu ali kiba hajui kama huu ni mwezi mtukufu!!!!!!!!!!!!!!loh Dunia imekwaisha hakuweza kufanya tour miezi yote aje afanye mwezi huu hasara kubwa na wwengine hapo mnajifanya waislamu kweli i don't know............

    ReplyDelete
  10. We Ali Kiba we, Mwogope Mungu, mwezi mtukufu huu we bado unaimba msiki tu, kwani kwa kuwa bongo celebrity hata dini yako umesahau..Haya we!

    ReplyDelete
  11. Kwa ukweli Ali ujaitendea haki NAFSI yako tufanye maovu yote lakini huu ni wakati wa KUTUBIA Mbaya zaidi dada zangu mmevaa mbovu.
    starehe haina Mwisho ila Kunawakati Inabidi Mwenyezi Mungu naye apatiwe nafasi ya kushukuriwa.

    ReplyDelete
  12. Huyo aliyevaa jeans ya blue na sharti ya draft la blue.....ni mvulana msichana?

    Mnatusema siye huku na nguo zetu joto, tukivaa boots ohhhh joto ...sasa hii si summer jamani huko kweenu na ni usiku mbona kajirundika hivyo....nakumbuka kuna mtu alitoa comment kwenye picha ya party bongo juzi tu akiulizia hivi huku hatuna dress code kwenye clubs na nyie huko je ...dress code hazikuwako au ....???????

    ReplyDelete
  13. HUKO DC HAKUNA GYM?

    ReplyDelete
  14. Hizo ndio show zao zinavykuwa woooote wakija these two side of atlantic. usitegemee watapelekwa millenium dom au...hello no kwenye vibar vya wabongo havina hata stage...two hrs hao wanakipa alafu mna-published back home oh! it was...njoo ulaya uone damn! kama prez anakuja uoni news on telly itakuwa bongo flava na ukumbi wabongo wenyewe wanaokaa huku full beef wataweza kweli kuorganise event ya maana katika ukumbi wa maana? kama akili nyembamba, na mawazo will be the same na hela pia nyembamba
    tunashidwa hata kuona mifano ya the like of Akon, Two face and other...
    full michosho

    ReplyDelete
  15. astaaaaakafululaaaah yaani mwezi wote huu.........we ally, we ally mswalie mtume mdogo wangu, yaani hata aibu huna.

    sasa hapo utatu-convisi vipi wasilam wenzio kuwa hukugusa pombe, ana huku-ikurbia zina?!!!

    ReplyDelete
  16. Hivi kama kitu huna huakika nao au hukijui unapata hasara gani kuuliza? Au mmesahau kwamba kuuliza si ujinga? Naona watu wamekurupuka kwa kuanza kukandia tuu mara hiki mara kile.
    Hio siku ilikuwa ni siku ya party ya wabongo na hall lilochukuliwa ni kutoa nafasi kwa watanzania watakaokuja kutoka kila pande.ali kiba aliongezewa ka ku spice up the event sio na ndio wakati wake wa kuwaburidsha watu ikabidi nafasi hiandaliwe hili haweze kuburidisha na baada ya hapo wataendelea na sherehe yao kama kawaida.kwahio mambo ya kulaumu ukumbi futeni kabisa ukumbi ni mzuri na huwa unatumika mara nyingi tu.
    wale wanaolalamika kuhusu mavazi kila mtu anavaa kujiridhisha nafsi yake sio za watu.unayelalamika wanawake wako uchi nadhani hujui uchi nini.
    Unaelalamika watu kucheza huku wameshika vinywaji hawakusumbuka hakuna nafasi ya kumuekea kila mtu meza ya kuweka kinywaji chake hili haende kcheza hio ni kawaida huku na watu wana enjoy tu.
    Nasemaga kila siku tuacheni kuumiza roho zetu kwa kitu ambacho akikuhusu au akiingilii maisha yako kwa njia yoyote.
    Try ur best to make urself happy no one will do it 4 u.
    Asante kaka michuzi kwa nafasi hii.

    ReplyDelete
  17. Unajua watu tunawasifia tu ooh wanajaza ukumbi hizo kumbi wanazojaza mmeziona?me naona hii ni kama party ya familia tu,jamani watu wanapiga show me naona tuwe tunasifia show wanazofanya nyumbani huko Tz na si huku ughaibuni,hizo wanazoziita kumbi haziingizi hata watu 1000 ni watz tu ndio wanaojaa,me naona wanapewa moyo tu lakini ahhhh wapiiii,they still have a long way to go whether u like it or not!

    ReplyDelete
  18. Jamani majuu kuna kumbi nzuri ila na bei zenyewe zimechangamka, tatizo waandaaji wanataka kupata faida kubwa kwa hiyo wanachagua vijikumbi viduchu visivyo hata na stage ambavyo ni cheap(na kiingilio kinakuwa kikubwa), matokeo yake show haziwi nzuri na mahudhurio yanakuwa hafifu maana watu tushajichokea kuliwa hela zetu kila siku....

    ReplyDelete
  19. KWELI DC NI CAPITAL CITY/DAR ES SALAAM MAANA MACELEBRITY WOTE WA BONGO LAZIMA WAANZIE DC..MNAJITAHIDI KEEP IT UP..!! KAZI NZURI DC...UKUMBI BOMBA TUU TULIENJOY.

    ReplyDelete
  20. Acheni kuhate ...haters hamkosi cha kusema...let them rest pliz

    ReplyDelete
  21. anony wa 3:46pm,nadhani huyo KIBA yupo USA na sio Ulaya kama ulivyosema.kuhusu mavazi nadhani labda wengi choka mbaya hahaha..just kidding..lkn kwani ungependa wavae mavazi gani?kuhusu ukumbi hao waandaaji nao Choka Mbaya vile vile..nadhani hapo itakuwa Bar za Uswahilini.wamesogea viti na meza alafu ndo vile tena..hahaha

    hao waandaaji nadhani ndo wale wale walioharibu Columbus Old Skul few months ago.

    ReplyDelete
  22. Tatizo la DC sio wasanii. Ni waandaaji. Yaani watu wanajipinda kutoa kila walichonacho, lakini maandalizi yanawakwamisha. Alikuja Bonny Luv wakamweka Safari. Haikunoga watu wakasema weeee basi wakaona wamtafutie penye hadhi wakampeleka Gallery. Sasa pale kukawa na sherehe 3. Kwanza "Bachela-Pati" ya wahindi pili "Besdei" ya mnugu kisha wakawepo kina sie wazee wa Old Skool. Halafu sasa ukumbi mmoja. Matokeo yake hakuna aliyepata alichotaka. Maana akiingia Bonny kina sie haoooo ukumbini, then wanakuja wahindi na wanugu kulalamika. Si wanataka nyimbo zao za kisasa? Sasa jamaa japo alifanya makamuzi akaonekana zoba na mtu wa zamani mbele ya wasiojua kilichokuwa kinaendelea. Sasa sijui hata kama Bonny mwenyewe alijua kuwa anaenda kwenye mchanganyiko wa watoto namna ile. Sasa ona Ali naye yawezekana alikamua ila maandalizi ndio hovyo.
    Ila ndo ujasiriamali huo, kuwekeza kidogo upate faida kubwa.
    Sema Ramadhani imeanza sijui Mungu na Dola nani mkubwa Kiba. Chunga roho

    ReplyDelete
  23. Eti ALI KIBA ateka Marekani!! mnacheza, sema awateka watanzaia waishio Marekani, hivi hapo unaona sura ya Mmarekani? nyie nyote hapo ni watanzania ambao hamna uwezo wa kuingia shows kama za wamerekani na wakija wabongo mnawalalia kwa viingilio njiwa mnajaza ukumbi, eti ndo ameteka Marekani, kwanza nani anamjuwa Ali Kiba kama si nyinyi watanzania pekee, msilete za kuleta, kwanza hakuna hata mtu anajuwa kuwa kuna mwanamuziki toka Tanzania kaja. Msitudanganye.

    ReplyDelete
  24. WEWE EDWIN NDAKI VUUTA BANGI KWA KIPIMO..HUYU MWIMBAJI HANA UWEZO WA KUINGIZA MASHABIKI WATAKAOLIPA JUMLA YA "$30,000.00 KWA USIKU MMOJA" KWANZA WABONGO WAMEJITAHIDI KUFIKA, NA WALA HATUMJUI KIASI HICHO, TUNAJARIBU KUDUMISHA WASANII NA KUWAUNGA MKONO WASHKAJI.

    ReplyDelete
  25. HIKI NI KIASI NILICHO PATA WASHABIKI WANGU WALIOWEZA KUINGIA NI 98 WANAUME WALIWEZA KUTOA DOLLAR 100 NA WANAWAKE WALITOA DOLLAR 80 VINYWAJI HEINKEN DOLLAR 5 NA BUDLIGHT DOLLAR 3 PER BOTTLE, HARD LIQUAL WAS 7 BUCKS, KUMBE NILIFANIKIWA KUINGIZA KARIBU DOLLAR 72,198.52 BAADA YA MAKATO NA TAX. I WAS TOLD HERE IN USA I HAVE TO PAY TAXES.NATUMAINI ZIARA ZANGU KWENYE MIJI MINGINE KAMA BOSTON, MINESOTA,KANSAS CITY AND NEW YORK ITALETA NEEMA KAMA HII YA DC. ASANTENI WADAU WOTE KWA MOYO MKUNJUFU

    ReplyDelete
  26. HUYU aliyejiita ALI KIBA si ALI KIBA mwimbaji labda mwingine...msanii hasemi mambo kama hayo kuwa alilipisha watu dola 100. Kama ulikuwepo ungejua walilipa kiasi gani...mfagilieni dogo..walijaa watu wa umri tofauti na WALIFURAHISHWA mambo ya steji, sebuleni , jikoni jua zaidi kuhusu mambo ya shoo kabla hujaanza kubwabwaja...Tanzania ni yetu tuisadie kupata jina tukiishia kupigana madongo TUTAFIKA? Majirani zetu siku zote WAKO JUU ikifika kwetu LAZIMA KUMALIZANA ....Wake up Mtanzania...Dogo fanya mavituz na ninaona watu wameanza kujiit ajina lako!!!!

    ReplyDelete
  27. Ali kiba anapendwa na wakenya kuliko wabongo na sio kwamba sio mkali jamaa mkali sema bongo watu hawapendi kussuport mtu kisa wivu.utasikia nani akasikiliza bongo fleva akati dollar 20 naenda club na enjoy vizuri tu.wabongo kubalini sio wote tunaweza kua nakipaji kama mwenzako kajaliwa muunge mkono kama huwezi nyamaza sio unatoka na maneno ya kukandia bila sababu.
    Kwa state zingine show ilikuwa nzuri na jitokezeni kwa wingi kumuunga mkono ali kiba .

    ReplyDelete
  28. mmh ni kweli haka ka ukumbi ni hovyo hamna kama wewe ni urefu wa over 6ft basi utagusa ceiling. Pia hamna stage wala nini!! Ni papo very local. Hivi WABONGO organizers mnashindwa kupanga mambo yakawa mambo! Afadhali sikuenda baada ya uchafu wa OHIO bado nina sufffer from that trauma!!

    ReplyDelete
  29. waislamu bwana!
    hamjui jamaa hiyo ni kazi yake na ndio imemleta ughaibuni, isitoshe anapiga wikiendi tu yaani siku nne ndani ya mwezi si atazilipa mwezi ukiisha.
    basi na nyie acheni kazi zenu sababu ni mwezi mtukufu au kazi zenu hazina connection yeyote na maovu?
    acheni kuonyesheana vidole wakati nyie wenyewe bado mna mapungufu ya kurekebisha

    ReplyDelete
  30. Ama kweli tutaishia kufa na roho zenye chuki na umaskini. Watu wamehangaika Ally kafika Marekani. Wanaishia kuitwa si wabunifu na kukandia sehemu. Inabidi tuangalie mambo fulani fulani. Ni kazi gani waliyoipata kuhakikisha anakwenda na kuandaa show. Watanzania wamepelekewa Kijana ambaye anavuma si Afrika Mashariki tuu bali na kati na hata magharibi na sehemu nyingien nyingi anasikika. Sisi tunaonyoshea vidole watu tukae tujiulize kwanza kabla ya kunyoshea vidole. Ungekuwa wewe ungeweza? Na kama ungeweza kwa nini hujafanya mpaka leo? Watu walioenda kwenye show hao ndiyo wangetoa maelezo kitu gani kilipungua na kama kilipungua tutumie nini kiendelezwe si lawama tuu. Ally alikuwa na option ya kukaa kwake au kwenda kwingine au kufanya kitu kingine...ameenda huko hamna hata "hongera" inaishia kulaumu. Haya mambo ya Ukumbi ukumbi andikeni point za maaana...vitu kama kuangalia jinsi gani na sisi tutaweza kuiendeleza nchi yetu si ndani tuu hata nje ya Tanzania. Wenzetu wakija hapa tunawashangilia tunajisahau kuwa na sisi tuna wasanii wetu. Inatia huruma kuona comments nyingi humu ni kulaumu...tukubali kijana ana kipaji tumshangilie tumsaidie aendelee na sisi tuige na tufuate njia wanazotumia watu katika kujiendeleza...maendeleo si lele mama ukadhani ukilala halafu uamke utayakuta yanakusubiri mlangoni lazima ujitume...

    ReplyDelete
  31. DINI ni imani kamaa akifunga mwezi wooooote utampa pesa za futarii, ramadhani iko oman, weee unaye funga unauhakika gani nakufunga kwako na Mungu??? Dini ni imani usimseme mtu usimlazimishe mtu kuna dada zenu wameolewa na hao mnao waita makafiri nmafriji zimejaa nguruwe baba zao kutwa wako misikitini bongo wanajua fika na wanapokea pesa kutoka kwa wakwe zao na wakaa kimyaaaaaaaa na wakatumiawa pesa na hao makafiri wazipikia futarii, Tuko na waarabu huku ulaya wanapika pizza na wanachanganya na nguruwe kweupe peee pee na warabu orignal na sio wakuchovywa wanasema mzungu bila nguruwe hajala waliambiwa warudi kwao vita vimeisha walienda kulia makanisani na kutokula wakawaonea huruma DINI NI IMANI ISHI NA UNAVYOWEZA

    ReplyDelete
  32. HOngera Ali Kiba nasikia vitu vyako lakni sikuweza kuhudhuria hii show ya DC nitaangalia state nyingine utakazo burudisha. Sasa nyie vichaa wengine. Mlitegemea kwa dollar $10-$20 muwekwe kwenye ukumbi wa maana itawezekana vipi? Nafasi ya kupata ukumbi wa maana ipo ila kazi ni kuwa watanzania mtakubali kutozwa mpaka $100 nyie kufidia gharama za ukumbi ndiyo haya mambo kila siku organizers tunalaumiwa tunakula pesa sijuhi vijicent. Nani ale hizo dollar kumi kumi zenu? Zitamfikisha wapi? Tuache roho za kiuchoyo na ndogo na kukata tamaa bali tuwe na malengo ya juu na tupendane na kusupportiana. We are definitely our own enemies.

    ReplyDelete
  33. haaaaaa hapo marekani ama tunataniana nyie waandishi...kama sebuleni vilee.....

    ReplyDelete
  34. jamani hizo ni picha tu, NA WABONGO NI HIVI, SEMENI MNAYOSEMA MAREKANI hauwezi kuilinganisha na TZ kimaendeleo, hizo kumbi sio mbaya kama mnavyodhani, ila ni kweli za bei rahisi na zinakidhi bajeti zao ukitaka kumbi na mengineyo utapata. MAREKANI ni MAREKANI, Semeeeeeeeeeeeeeeeeeeni we ila huko kwa wenzetu ndo dunani.
    Najua mtasema ila huo ndo UKWELI.NA ALIKIBA NINA IMANI ANAINJOI Au vp dogo?

    ReplyDelete
  35. Naona kuwa watu wanaogopa "UKWELI" wanataka "KUPONGEZWA" hata wanapochemka.

    Asilimia 95 ya maoni hapa sijaona yanayomponda Ali KIBA.

    Binafsi nikiwa mmoja wanaopenda kuona sanaa ya tanzania inafika mbali lazima niongee ninapoona "HUWEZI KUMWAGA UGALI..MI NISIMWAGE MBOGA"..

    Nyie mnao watetea waandaaji au kama ndio waandaaji lazima mkubali kujifunza.

    Mnao wajibu wa kuandaa mazingira mazuri ya "show" ili kuvutia si tu watanzania bali na watu wengine na ndio kuutangaza muziki wetu.

    Kama mnakosa stage..mnaonaje mchukue japo "meza kama NNE ili iwe stage?...lol.. au mnaofia ukumbi sio mrefu ..msanii anaweza kugusa dari.

    Msiamini mneendeleza muziki wa bongo kwa kuandaa show zenye kiwango cha chini.

    Mwanzo Mgumu..chukueni faida kidogo..fanyeni mambo makubwa kwanza.

    Kuhusu Ali Kiba najua kijana anakipaji na ninafikiri hata yeye mwenye kwa mwaliko huo unamsaidia kujifunza mawili matatu.

    Kila la kheri waandaaji ila LAZIMA mkubali kuwekeza ili show zenu ziwe na TIJA na kuwavutia watu wengi zaidi.

    Ni bora muweke kiingilio 50usd mpate wato 250 kuliko watu 400 karibu kila anayetoka anasema "katu siendi tena show za wabongo"

    Ni hayo tu..

    Tutafika tu

    N.B
    Kuna makosa kibao ya uandishi kwenye maoni yangu maana nipo "fasta"

    ReplyDelete
  36. WALIINGIE WANAUME 98, NA WANAWAKE 80 JUMLA 178 HAWA HATA WANGELIPA $100 KILA MMOJA NI $17,800. SASA HIZI $72,000. AMEZITOWA WAPI? SHULE NI MUHIMU JAMA HATA MAHESABU NJIWA YANATUSHINDA

    ReplyDelete
  37. Kwa wale ambao hamjatembea nchi za ughaibuni, when local musician visit a country like US where you have tons of well known and struggling musicians, your success will come from your fellow country folks and there is no difference with Ali Kiba, unknown Jamaican musician or unknown Spanish musician, etc. These local musicians may be big may be huge in the motherland when they land here they are just regular folks. So Ali Kiba entertained the Tz crowds and he is very talented fela but people can only pay $20.00 max bro...I attended Jay Z show and I paid 40 bucks...whadday think...This is US, unless you have a Hollywood smell you ain't nothing..Better recognize

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...