mwenyekiti wa simba mzee hassan dalali akiwatuliza wanachama na wapenzi wa simba wenye hasira ambao waliandamana leo na kurusha bakora mtaa wa msimbazi kufuatia hatua za kinidhamu kuchukuliwa kwa baadhi ya wachezaji na benchi la ufundi.
Habari kamili ni kwamba uongozi wa klabu ya soka ya Simba imewafukuza na kuwasimamisha wachezaji na makocha wa timu hiyo kutokana na tuhuma mbalimbali.
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Hassan Dalali maarufu kama ‘Field Marshal’ alisema leo mbele ya wanachama wa klabu hiyo katika makao makuu ya Simba yaliyopo mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam kuwa hatua hiyo ilifikiwa na kamati za utendaji, ufundi na mashindano baada ya kuwahoji wachezaji wote wa timu na benchi la ufundi mmoja baada ya mwingine juu ya tuhuma mbalimbali zilizopelekea timu kuwa na mwenendo mbovu kwenye ligi.
Dalali alisema katika hicho kilichofanyika juzi kamati hizo zilifikia uamuzi wa kuwatimua kwenye klabu hiyo kiungo mkabaji kutoka nchini Kenya Edwin Mukenya na kipa wake namba moja Amani Simba pia katika mkumbo huo wa kufukuzwa yumo Kocha Msaidizi wa timu hiyo Jamhuri Kihwelo 'Julio' na kocha wa magolikipa Iddi Pazi ‘Father’.
Aidha Dalali alisema wachezaji Mussa Hassan Mgosi na Henry Joseph wamesimamishwa kwa muda.Wachezaji Ulimboka Mwakingwe ambaye ni nahodha msaidizi wa kikosi cha Simba na kiungo mchezeshaji Mohamed Banka wamepewa karipio.
Kwa mujibu wa Dalali, uamuzi huo pia umezingatia mapendekezo ya kocha mkuu Krasmiri Benzinki na kufuatia uamuzi huo benchi la ufundi la Simba litakuwa chini ya Benzinki ambaye sasa atasaidiwa na mlinzi wa zamani wa klabu hiyo Amri Said.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...