naam! tupo juu, hawa wadau wametuwekea google sio tu ya kimatumbi bali pia mahususi kwa bongo. tatizo linakuja kwenye ulaji. wao wana ile kitu inaitwa 'adsense' ambapo ukiomba wanakuwekea matangazo kwenye globu ama tovuti yako ambapo wadau wakibofya hesabu zinaingia kwenye akaunti yako utayowapa. ila hadi sasa globu ama tovuti zinazotumia lugha ya kiswahili hawaitambui kwa kile wanachodai kwamba lugha hiyo, ambayo wameanza kuitumia kwenye google, haimo kwenye orodha ya 'adsense'. hii imekaaje wadau?



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Taratibu nafikiri hata adsense inayotambua maneno ya kiswahi itakuja. Lakini kuna tovuti ngapi za kiswahili ambazo zinatangwazwa au zinajitangaza kupita google? kama hakuna ina maana google hawezi kupoteza muda na fedha zao kuweka adsense ya kiswahili.

    Hata hivyo mimi nalilia google map. Ni lini google map ya Tanzania itakuwepo inayoonyesha mitaa na address za makazi kama ilivyo kwa US?

    Utaona google pia wametoa product nyingine ambayo inaitwa street view. Hii ni bomba ile mbaya hasa kwa watu wa real estates maana unapoafuta nyumba unaiona kabisa na unaweza kuzunguka mitaa ukiwa umekaa tu kwenye PC yako.

    Wabongo bado tuna safari ndefu kuelekea kwenye technolojia.

    ReplyDelete
  2. Kwenye google map tatizo sio lao ni la nchi yetu kuwa na majina na vitu viinavyoeleweka

    SA na Nigeria mbona ramani zao zipo?

    Hivi unaweza kutumia GPS bongo....si utaishia baharini kweli.....na kama barabara ni hapo downtown too how about the suburbs of Dar es Salaam city usiende mazenze kwanaza....nenda kimara, sinza, masaki, msasani , mbezi etc hamna majina ya mitaa....mabarabara yapo tu no numbers or whatsoever.....

    We mpaka leo mtu anatangaza jina la duka lake anasema liko karibu na mahali fulani...kwa nini asitoe tu number na jina la barabara na kama barabara yenyewe ni ndogo au haijulikani sana ndio amention at least libarabara likubwa linalojulikana....let say off of Pugu road.....kila siku karibu na rose garden, karibu na shoprite.....ulimwengu wa ssa utatuacha tu hivi hivi

    ReplyDelete
  3. nyie watu mnasikitisha sana,mmekalia kutoa kasoro badala ya kutafuta solution.sa tukianza kujidharau wenyewe wengine watufanyeje?
    toeni maoni nini kifanyika ili kupata hizo post code ndani ya bongo nyinyi ndo taifa linawategemea kwani mko nje ya nchi tayari kwahiyo mjifunze vitu vipya mvilete nyumbani kwa ajili ya maendeleo.
    ahsanteni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...