CHAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA MAREKANI AMBALO MAKAO YAKE MAKUU YAPO MJINI HOUSTON TEXAS KWA KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHA MAPINDUZI SHINA LA MISSOURI KITAFUNGUA RASMI SHINA LAKE LA KWANZA NCHINI MAREKANI KATIKA JIMBO LA MISSOURI HAPO SIKU YA JUMAMOSI YA TAREHE 13/9/2008. WANACHAMA WOTE WA CHAMA CHA MAPINDUZI, WAKEREKETWA, PAMOJA NA WANAMAPINDUZI WOTE POPOTE HAPA MAREKANI NA NJE YA MAREKANI MNAALIKWA RASMI KATIKA SHUGHULI ZA UZINDUZI HUO.SHUGHULI YA UZINDUZI ITAONGOZWA NA MWENYEKITI WA TAWI LA CCM MAREKANI NDUGU MICHAEL NDEJEMBI AMBAYE ATAAMBATANA NA VIONGOZI WENGINE WA TAWI NA WANACHAMA KUTOKA HOUSTON TEXAS PAMOJA NA MWENYEKITI WA SHINA LA MISSOURI NDUGU DEOGRATIS RUTABANA VIONGOZI WENGINE WA SHINA LA MISSOURI.
SIKU YA UZINDUZI: TAREHE 13/09/2008
MAHALI: JIMBO LA MISSOURI
UKUMBI: COVES CLUB HOUSE 5417 NW.85TH
MTAA: KANSAS CITY MO 64154
KADI ZA CHAMA CHA MAPINDUZI ZITAKUWEPO UKUMBINI TAFADHALI WANACHAMA MJE NA PICHA (PASSPORT SIZE). KWA MASWALI YOYOTE KUHUSU UZINDUZI HUO, TAFADHALI WASILIANA NA MWENYEKITI WA CCM MISSOURI NDUGU DEOGRATIS RUTABANA SIMU 816-812-5495 AU KENNEDY MALLYA SIMU 816-255-4944.
KUMBUKA: KIINGILIO KITAKUWA BURE NA KUTAKUWA NA VINYWAJI


Tulikuwa tunayaona UK na uko Marekani mmeanza kujiunga na chama cha mafisadi CCM au na na nyie mmesaidiana nao kuwawekea pesa zao uko au mnawafanyia deals za kuimaliza nchi yetu?
ReplyDeleteAH, ndo hivyo!! Hao ndio ndugu zetu tunaowatarajia na kuwategemea ya kuwa wameona mbali.Halafu wanadiriki kusema kutakuwa na vinywaji bure, bila ya kujali itikadi za kidini ya kuwa huu ni mwezi mtukufu. Haya, kwa kuwa mungu alishawapiga laana ya kuutukuza ufisadi kwenu nyie ndugu zetu endeleeni. Mungu ni mkubwa ipo siku atawapeni MAONO.
ReplyDeleteEhee, na nyie mmeanza!!!
ReplyDeleteEhee, na nyie mmeanza!!!
ReplyDelete2010 ITAKUWA JOB TRUE TRUE.... HAKIKISHENI VIKADI VYENU VYA IMMIGRATION VIKO SAWA KABLA HAMJAANZA KURUDI BONGO KUCHUKUA HIZO FOMU ZA KUGOMBEA UBUNGE ILI MAFISADI WENZENU WAKIWASHINDA KWENYE UCHAGUZI MSIBAKI KUGOMBANIA VIBANDA KWENYE LILE GOROFA LA MACHINGA KUANZA KUUZA VI NIKE NA VI TIMBERLAND VYENU MTAKAVYOENDA NAVYO
ReplyDeleteJuzi juzi tuliposoma habari juu ya Waadventista wasabato masalia waliokuwa wamepiga kambi katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar wakisubiri kwa imani ya kunyakuliwa na kupeperushwa bila tiketi, pasipoti, viza, nk (sijui kwa nyungo) hadi ughaibuni kueneza neno la Bwana, watu wengi walishindwa kuelewa kinachoendelea vichwani mwa wabongo. Baadhi waliandika ninanukuu: "kweli dunia imeisha sasa ukichaa unakuja wa kila namna..."; "kuna sababu ya kuongeza mapambano dhidi ya malaria, no doubt hii ni malaria iliyopanda kichwani inapelekea ukichaa...". Kama hii sio malaria ya nchi za baridi iliyowapanda vijana wa kitanzania kichwani, basi ni mradi wa Makamba!!!!!
ReplyDeleteMmeanza na nyie huko tehetehetehetehetetetetet
ReplyDeleteTawi la kwanza na hilo la missour ni la ngapi?
Mwenyekiti wa CCM marekani alichaguliwa na nani kama tawi ndio linafunguliwa? Kwanza huko missouri sio marekani
Ndejembi hao hao watoto wa baba
Huston mmeona kuiba viwandani na kwenye mabank siku hizi soba sasa mnajipalailia njia ya kurudi bongo.
Tumewaona vijana wengi tu wamerudi bongo kutoka Huston sijui ni self deportation au ......Kimya kimya wako hapa...hata degree hawana....Fanyeni yaliyowapeleka huko sio mambo ya ajabu.
Hivyo vyama vitasaidia nini hapa bongo. Huko UK wamefanya nini toka wamefungua vyao....acheni uzembe....Njooni nyumbani mjiunge na vyama.
Blood sucker
Tumeanza sasa.
ReplyDeleteHaya yalikuwa UK sasa yameingia hapa marekani.
Watu wengine bwana, mmemaliza kila kitu bado hamtosheki sasa mmeanza siasa.
Mlikuja hapa marekani mkaona ndoa za makaratasi ndo suluhisho mkapata, then- bado mkaona wizi wa credit card ndo mapigo mkafanya, halafu mkaingilia hapo Houston wizi wa comp chip halafu
sasa hamuelewi cha kuendea mmeingilia sasa CCM.
Nendeni mkafanye mambo hayo huko Tanzania. Maana sheria za nchi hii zinasema wazi kabisa huwezi anzisha chama cha siasa ,kufungua shina, tawi, au kufanya mikutano katika ardhi yake bila ruhusa ya jimbo hilo au nchi kwa ujumla. Ninyi mnafanya kiholela kwa kuandikiana mail kitanzania tanzania na kusema kila mtu aje,katika kikao wakati hicho chama hakina usajili wowote hapa marekani.
Mtakapokutana hapo Missouri au tena Houston basi tutatoa taarifa kwa sehemu husika ili tupate uhalali wa hivi vikutano, vikusanyiko na vikao vya kishenzi shenzi.
Kama wewe ni CCM au unataka kuwa CCM hapa marekani ni sawa, ila wasiliana na CCM Tanzania na kamilisha mambo yako nao huko huko TZ na wakutumie kadi zako kivyako na sio kufungua shina au mashina hapa marekani bila kufuata sheria za nchi.
Toeni majina yenu wazi ili tuyawasilishe sehemu husika na kuyafanyia kazi.
lazima mfuate sheria za nchi hii na siyo kujiamulia bila kujali.
Kumbe waliweza kupeleka watoto wao hata marekani. Ndejembi si alikua kiongozi wa chama huyu?
ReplyDeleteTulizania mafisadi wanao wako UK tu kumbe na USA
KLH NEWS,hakikisha unaleta hii shuguli live and direct toka kwenye kikao
ReplyDeleteMsije mkaanza kutuletea umbeya na majungu kama ya UK huku. Lakini si shangai hizo sehemu zinazoazishwa hivyo vyama wanaoishi humo hawana tofauti na wa UK. Usaniiii na uswahiliiii mwingiiiii kariakoo ina afadhali....Maneneo na majungu sana tu vimeanza Huston/Missouri soon utasikia Maryland and then Ohio .....nani anataka kubet. Hizo state hata kama hujui umbeaya ukihamia humo utaujua tu.
ReplyDeleteHivi vitu tumevizoea kuvisikia kutoka UK, India, Urusi, Pakistani na Mozambiki, sasa leo mnavileta hadi huku marekani? Nawapatia anonymous tip watu wa ICE waje wapate vichwa kadhaa...
ReplyDeleteAdress si mshatoa tutandaza kipira cha INS tuone kama kuna atakebaki.
ReplyDeletetafuteni cha maana cha kufanya.
na huu si uongo kwani info zote mshatuma an sisi tunawapelekea INS hizohizo info.
anayetafuta safari ya bure bongo ajitokeze as a matter of fact washaanza utaratibu wa immigrants wanaotaka kurudi makwao bure lakini aliojitokeza ni mtu mmoja tu
Bila shaka wahusika hawajui utaratibu, kama mdau alivyosema hapo juu. Tangu lini uongozi bila uchaguzi?????Kweli CCM, ni mabavu tuu!!
ReplyDeleteUtaratibu gani umetumika kufungua Shina uko Missouri? Kwa nini isiwe Washington DC, au uko uko Houston? Ndio kusema sheria za Missouri zinaruhusu ufunguzi wa Mashina ya vyama vya kisiasa...
tehetehetehetehe
Ebwana eehh, All I can say is I aint no snitch but this time Im gonna make that phone call to INS.
ReplyDeleteBe ready for the trip we dont need this mess around here and we dont welcome there kind too. Your orry asses will be gone just like that.
Pelekeni uduwanzi huo kwingine ua mtaiona Kipawa taratibu na mgema juu ya mnazi
habari za kwa ujumla watanza nia wote popote mulipo kwa kweli nimekuwa nikiangalia mtandao huu na kila kukicha nimekuwa nikisikia matawi ya ccm yakifunguliwa nje ya nchi ( ughaibuni )hii mimi nashindwa kuelewa maana sijawahi kusikia chama cha democratic ama lipablic kuwa na matawi nje ya nchi zao ? sasa hii ni watu kujitafutia njia wakirudi nyumbani ama ni vipi ?
ReplyDeletetunajifunza kutoka wa watu walioendelea ndio tutapata nasi kuendelea . watanzania tuache hizi habari za ujanjaujanja wa kujitafutia umaarufu .
Huo upumbavu wenu na chama chenu cha mapumbavu,huko huko msije kabisa anga za huku new york,umeona wapi ujinga kama huo ,kwa nini musirudi bongo mkaleta upumbavu wenu,sasa hayo matawi ya nini?,munataka kutugawa na huku pia?,huku kuna umoja wa watanzania,sio tena ccm,cuf na vingine mutatugawa tena,hawa ccm,cuf,chadema acheni hayo.
ReplyDeleteWala msilalamike sanaaaaaaaaaaaaaaaaaa isije kuwa ni watoto wa mafisadi ndio wanaendesha hizo kampeni za kufungua matawi ya CCM kwani mimi binafsi nawajua wengi(watoto wa mawaziri wastaafu kwa ufisadi, watoto wa mbunge mmoja wa Kike nk), wapo huko USA na UK na ndio wao wanashiriki kufungua matawi hayo pamoja na vibaraka wao (Marafiki).
ReplyDeletekwahiyo sio ajabu matawi hayo yakafunguliwa kila kona kwani watoto wa mafisadi wapo kila kona za nchi mbalimbali wakitumia fedha za ufisadi na sithani walalahoi ambao wameangaika kupata safari wakajihusisha na mambo ya CCM au UVCCM kwani hata huo muda hawataweza kuupata kwa shift nyingi za kazi na overtime.
Kenge
Inaelekea watanzania asilimia kubwa wanaoenda USA wanajishughulisha na mambo ya ajabu kwa kutaka maisha ya haraka haraka, mwishowe mtachafua jina la Tanzania na kufanya wengine wanaotaka kwenda huko wapate vipingamizi kwa ajili ya tabia zenu, kwani tumesikia humu kuwa kuna wizi wa viwandani, wa comp chips, kuna umbea, na mara nyingi umbea uendana na tabia mbovu, tumesikia wizi wa credit cards katika mabenki, kwa kweli huo ni mwanzo mbaya wa kutangaza Tanzania vibaya na kuwapaka kasoro na matope watu wazuri wenye nia njema ya kutafuta maisha, hizi habari na kama zile za wanaigeria wanavyoogopwa UK, kwa si wote lakini wale wachache wamewaalibia wenzao wenye shida kweli ya kutafuta maisha, kama vile wa-Albania kwa wizi katika ATM za benki, tuwaombeni acheni hizi, tafuteni maisha mazuri kihalali.
ReplyDeleteUSHAURI WA BURE, KWA HILI LIFE LA HAPA LINAVYOENDA FAST,WATANZANIA WALIVYOFUNGUKA MACHO NA KUONA MAUOZO YANAYOENDELEA HUKO KWENYE NCHI YA WADANGANYIKA!!! LOL HIKI MNACHOKIITA TAWI SIJUI UMOJA KUFANYAJE MSISUMBUKE KUUANZISHA SABABU MTAWAPATA WADANGANYIKA(WAPUMBAVU TU) WENGINE WALIOSHINDWA KABISA KUBADILIKA MAWAZO KWENYE VICHWA VYAO PAMOJA NA MADUDU YOTE YANAYOENDELEA KWENYE NCHI WALIYOIKIMBIA.........I COULD'NT AGREE MORE WITH MY FELLOWS ANONYS MNATHIBITISHA JINSI GANI HAWA WATU WANATAFUTA MATUSI YA WAZI WAZI TUMECHOKAAAA TUMECHOKAAA TUMECHOKAA NA HIVI VIJIKITU MNATAKA KUVIANZISHA NDIO MNATUTIBUA KABISAA....SIIPENDI HII SENTENSI(CHAMA CHA MASHETANI)
ReplyDeleteMy friend are you planing to establish a CCM government in the United States? I thought being in the United States you will contribute towards the development of Tanzania by supporting opposition parties but when I read your add it seems to me that you are no More than those “WAFISADI” of CCM!!!!
ReplyDeleteNYINYI WAOSHA VINYWA HAMNA MADA MNACHOONGA SAAANA BILA KUJUA MNACHATAKA NI NINI OOHH HAMJA SAJIRI OOOHH HAPA MAREKANI HAWARUHUSU OHHOO MSITUREETEE HUKU MAREKANI WEWE KAMA NANI HUKO MAREKANI UKIANGALIA SANA HATA MAKARATASI YA KUISHI HUKO HUNA UNAJIFANYA ETI MSITULETEE HUKU MAREKANI KAMA KWENU VILE USHAMBA TU!! UNAJUAJE KAMA WATU WANAFANYA KIHOLELA? ULIZA UAMBIWE LA SIVYO UTAKUWA MPUMBAVU DAIMA WATU SIYO WAJINGA MPAKA UKIONA WANATANGAZA UJUE WAMEANZIA MBALI UNAFIKIRI WATU WAMELALA KAMA WEWE? ACHENI WATU WAFANYE VITU VYAO NYIE LALENI BAADAE MTAISHIA KUSEMA WAMEPEANA OOHH WATOTO WA WAKUBWA, SHAURI ZENU CHANGAMKIENI MAISHA WAKATI UNAKWENDA!!
ReplyDeleteHAMUITAKI CCM NA HUKO MLIKO HAMNA CHAMA CHOCHOTE KINACHOWATAMBUA!! HATA MNAPOISHI HAMTAMBULIKI MNAISHIJE, KABLA HUJASEMA OVYO UJISAWAZISHIE NAMNA YA KUISHI HUKO, NA KABLA HUJABIGIA DEBE VYAMA VYA WATU WASIOKUTAMBUA VYA OBAMA AU MCCAIN USHAMBA HUOOOO
Kweli watanzania wamelaaniwa!!! Nasema hivi sio kwa furaha bali uchungu. Mimi nilifikiri tulivyokuja nchi za watu tulikuja kujifunza yale mazuri ili tuzisaidie nchi zetu. Wale tulioko Marekani tumeona ni jinsi gani watu walivyo na uchungu na nchi, uwazi wa kila kitu na mfumo imara wa kila kitu unaofanya watanzania walio wengi wasitake kurudi kwao. Na tunaelewa wazi kwamba hii isingewezekana kama isingekuwa vyama imara vya siasa.
ReplyDeleteNa wote tunaelewa kabisa kwamba Tanzania haifai kwasababu ya uongozi mbovu(corruption). leo hii watu na nywele zao vichwani wanadhani CCM inafaa, au ndo hao hao hao wezi "mafisadi" SHAME ON U
Lazima niwapigie simu wajomba kuhusiana na huo mkutano mchafu wenu, kwa hiyo nawapa tahadhari kabisa kwa yeyote atakayekwenda kwenye huo mkutano wa Chama cha MAFISADI lazima mjue watu wa ICE watokee. Kama unajua huna karatasi ujue lazima wajomba watokee. TUTAONA.
ReplyDeleteMuanzilishi wa Tawi ni mtoto wa Sijui Mkuu wa something ndani ya CCM Mr Ndejembi, ndio maana unaona huo upuuzi wao hawajauleta Houston na wamepeleka Missouri.
ReplyDeleteAll this kids ambao wamekuja US few months ago ndio wanaleta huu wazimu. I think it doesn't worth kupigizana kelele, but i believe inside US you will see different approch compared to that of UK. Kama mnaweza kufanya analysis angalieni hawa wote walijipachika vyeo kwamba ndio viongozi, wote ni watoto wa so called CCM elites.
Thanks Ndejembi kwa kupeleka huo wazimu wa CCM in Missouri, sababu you know kabisa kwamba ungejaribu kufungua that non sense here in Houston, then ungeona hata kama maji watu wangekunywa na wewe glass moja.
CCM my********
Mdau wa Houston, Texas 77057
Unajua vyama vya kikomunisti au kisosholisti ni marufuku ktk nchi hii...sasa wanaokwenda kujiandikisha wajue na litakalowapata.........
ReplyDeleteNa mimi najitolea kuwapigia simu watu wa Immigration na tutasema hawa watu wengi wao hawana makaratasi na wanaanzisha tawi la Chama Cha Kikomunisti zenye mlengo wa siasa kali. Nawapigia simu washikaji wengine wa state mbalimbali nao wapige simu.
ReplyDeleteINS Contacts
ReplyDeleteIf you have a question about immigration procedures, or need clarification,or repeort any immigration issues dont hasitate to call our National Customer Service Center (NCSC) at:
1-800-375-5283 (TTY 1-800-767-1833)
Haya wadau namba ya wajomba ndio hiyo na tushawatwangia simu.
hakuna kiongozi yoyote wa bongo anayeweza kumpa makaratasi mwanaye.
wanaweza kuibia nchi lakini kwa hili tutafikishana mbali
Jamani wadau wa State mbalimbali tafadhali pigeni hiyo namba ya Immigration (ICE) kwa wingi ili hawa watu wa CCM wakamatwe na kurudishwa BONGO, hatutati ujinga. Mimi leo nimeongea na jamaa mmoja anafanya kazi ICE na amesema atalishughulikia hili suala. CCM iishie huko huko UK lakini sio hapa. Sijawahi kumchongea mtu arudishwe Bongo lakini kwa hili hawa watu lazima tuwakomeshe.
ReplyDeleteWenzenu huko kutoka nchi zingine wanazitumia fursa zilizoko huko kujiendeleza kielimu,kimichezo na hata kimitaji na kufungua milango wadogo zenu huku nyumbani wapate urahisi wa kuja huko kwa madhumuni hayohayo NYINYI WENZETU KILA KUKICHA MNAWAZA CCM MNAKULA CCM MNAKUNYA CCM,aibu gani hii!Hivi Tanzania ilipata medali ngapi za Gold kule Olympics Beijing? Hata medali ya Bati hatukupata.Angalieni visiwa vidogo kama vya Jamaica jinsi vilivyo itikisa Dunia.Huko Marekani tuna MaStaa wangapi wa Kitanzania katika medani yeyote ile? HAKUNA.Upumbavu Mtupu.Mwangalieni mwenzenu Obama hivi sasa makubwa anayoyafanya.Hivi mnafikiri kwa kufungua matawi ya CCM huko Nje huko Marekani Tanzania ndiyo itaneemeka zaidi? Wajinga kwelikweli.Lini tutaanza kuwasikia watanzania walioko Marekani na Ulaya wakitamba katika Riadha za Kimataifa,wakitamba katika Premiere League za Uingereza,Hispania,Itali,Ujerumani na kwengineko?Lini tutawasikia Madaktari Bingwa wa Kitanzania katika tiba za Moyo,Kansa,Ubongo nk.Lini tutawasikia Matajiri Mabilionea wa Kitanzania waliowekeza huko Marekani,Uingereza na kwengineko?ACHENI HUO UPUMBAVU WADOGO ZANGU,Tanzania sasa imebadilika.Kama hujarudi huku nyumbani siku nyingi nakushauri uchukue likizo fupi uje ushuhudie mabadiliko yaliyopo huku nyumbani hivi sasa angalau katika sekta ya kupashana habari.Watnzania siyo Wapumbavu tena wa kudanganywa kama watoto wadogo kama ilivyokuwa huko nyuma,mtu kupata passport ni ajabu?mtu kusafiri kwenda nchi zanje ni ajabu?Hakuna ujinga huo tena.Hivi sasa huku nyumbani siyo siri tena TUNAJUA JINSI BALOZI ZETU ZOTE HUKO NJE ZINAVYOFANYA KAZI.Wasiwadanganye.Atakudanganya mtu ooh Tanzania inajulikana kwelikweli ulimwenguni,ooh ina sifa kubwa kweli duniani,sifa kwa kitu gani?Hata medali ya shaba olimpiki hukupata sifa itoke wapi? Kwa siasa safi na uongozi bora wa CCM? ustakencheke!
ReplyDeleteAnonym. wa 4.08 AM, naona umechanganyikiwa kabisa. Kwa ufupi una MAONO YA KUKU " Chicken vision". Sikutukani na wala sina nia ya kukutukana, hata kidogo!! ila kichwani mifupa yote muhimu imebeba haja kubwa.Kama una nia ya kusuta au kusutwa, ndani ya blog hii hakuna mambo ka hayo. Kama umeletwa ughaibuni na hicho chama usitake kuwaambukiza upuuzi waTAnzania wenzako wenye nia na uchungu na nchi yao. Sio kama wewe, Guruguru mkubwa wee. ??@€&nzi** sana,Kama huna la kufanya huko wategemea kujikomba CCM ndo dawa, nakuambia umeisha. Pundamilia We.
ReplyDeleteHuyo mtoto wa Ndejembi ni nani na anatafuta umaarufu kupitia CCM hapa US. Thats the F***d up shit to come with to US. Take that bulshit to UK, Russia & India.
ReplyDeleteKama maisha yamemshinda si bora arudi bongo kuendeleza kilimo.
Cha muhimu ampigie simu baba yake awe tayari kupokea airport kwani simu zishapigwa na wajomba wanasubiri.
Na kwa wale washabiki uchwara wenye nia ya kwenda vilevile kaeni mkao wa kula kwani safari mmejitafutia wenyewe
ANONY WA JUU YANGU NAKUSUPPORT 100% HUYO MPUMBAVU ANONY ULIYEMTAJA ANADAI TUCHANGAMKE TUSILALE TUCHANGAMKIE MAISHA SASA SIJAMWELEWA VIZURI KUMBE ANAJUA FIKA YEYE NA WA*#&ZI WENZAKE KUCHANGAMIKIA MAISHA NA YAWE BORA BASI UANZISHE TAWI LA CCM MIMI NILIDHANI KUANZISHA MATAWI YA SASA YA CCM HAYAHUSISHI PROFIT ILA NI KUANGALIA JINSI GANI WATOTO WA MIAKA 50 IJAYO YA TZ WATAWEZAJE KUWA NAMAISHA BORA MAANA KWA JINSI NCHI ILIPOPELEKWA NA CCM LEO WEWE NA WOTE MKIANZISHA MATAWI YA CCM LEO KWA NIA NJEMA MPAKA MNAKUFA MATOKEO MAZURI HAMTAYAONA NI PROSECC AMBAYO INAHITAJI SAFARI NDEFU KUTOKANA NA UHARIBIFU MKUBWA ULIOFANYWA NA CCM KUANZIA KUHARIBU AKILI ZA WATU,KUUZA NCHI, KUIBA HATA HIVYO VIHELA VIWILI TULIVYONAVYO NDIO MAANA NASEMA HAMNA MNALOLIJUA SISI SI WAJINGA YAANI MNANIUZI!
ReplyDeletejamani ujinga gani mnatuletea huu eti tawi la ccm linafunguliwa huku tumewakimbia na ccm yenu na uraiya tumebadili lakini bado mnatufuatia huku tuliko na pesa yetu mnataka kuila waizi wakubwa .msituletee upumbavu wenu .
ReplyDeleteNyie laleni na upumbavu wenu baadae mtakapoamka na kuamua au kurudishwa nyumbani ndiyo mtakapoona kuwa mmepoteza muda mkubwa wa kubeba mabox bila ya kuitumia vizuri akili yako kwa maisha ya baadae na kuja kuisaidia nchi yako kama unaipenda kweli nchi yako fikilia jinsi utakavyoweza kuisaidia na hakuna jinsi nyengine zaidi ya wewe kujiunga nao hao ccm ili muwe wengi wenye mawazo mazuri mkabadirisha mambo miaka kumi au ishirini ijayo maana kwa taarifa zenu mtasema mpaka mtachoka kama mnawaachia watu haohao kwenye vyama bila ya nyinyi kujiunga basi ndiyo haohao watakaowaongoza hakuna ubishi, sasa baada ya kutukana au kuchomeana kwa polisi maana hiyo ndiyo tabia ya wabongo na sasa wamepata sababu ya ccm kujitangaza mambo waliyoyazoea na wanayofanya kila siku ya kubigiana simu polisi hamna aibu? haya mambo nilikuwa nayasikia tu wabongo nje wanapiga simu polisi au hata makazini kuchomeana(werehouse)A.K.A box-job, kama mtaendelea na mwendo huo hamtaendelea daima mtakaa na kuangalia watu tu, jaribuni kutumia akili zenu kuiendeleza nchi yenu siyo kuponda na kutukana na kuiga mambo yasiyofaa kwani wengi wenu mnaoandika matusi na ujinga humu ndiyo nyie mnaovaa majeans makubwa mikanda kwenye magoti na machupi nje kofia kubwa T-shirt ya size ya Yao Ming XXXXLL unaivaa wewe mbilikimo hahaha, na kujaribu kuzungumza SLANG au kuficha accent mnachekesha sana!! hao wamarekani mnaowahiga wanawacheka pia wanawaona vituko jinsi mnavyovaa na mkizungumza, mnahiga upumbavu mnajiona wajanja eti mfanane kama mmarekani mweusi!! mnachekwa!! kama wewe unataka kupata gold medal kwenye olimpic usisubiri mtoto wa ndejembi akufungulie gym na akufundishe jinsi ya kukimbia au kuogelea huko nje!!, kila mtu ana mawazo yake yeye amefikiria ccm wewe nenda gym kafanye mazoezi uende olimpic ukashinde medal pumbavu ngedere nyie.
ReplyDeleteAnon 1:32pm, ahsante saana kwa kumpa vidonge vyake anon 4:08AM. Niliwahi kusema kwamba njaa zote ni mbaya ila njaa ya mawazo ni mbaya zaidi. Pale vichwa vya watu vinapojaa panzi basi ujue hakuna kitakachofanyika. Hawa watu wamekuja ughaibuni si kujifunza mazuri yaliyoko huku ili kukosoa nchi zetu masikini bali wanaona ni bora wazidi kuendeleza ufisadi walio wengi wazidi kuteseka. Na mimi nimepiga tena simu kwa wajomba ili kuhakikisha hii kitu iko kwenye record zao. Uzuri naona kuna mtu alishawapa taarifa.
ReplyDeleteNa wewe Anon 4:08am need to watch ur wide mouth otherwise someone will fill it with s...t
THIS IS COMPLETELY BS
USA sio utani comment moja tu ndio inasupport huu ujinga.
ReplyDeleteMsituletee migawanyiko ya watu hapa. Kwanini msiende bongo mkajiunga na vyama huko au kama ni card kwanini msiombe huko bongo wakakuletea.
Hivi hao watu ambao hawajaenda Bongo miaka mia wataisaidiaje nchi kwa kufungua haya mashina ya CCM?
Malengo yenu ni nini kuwa na tawi la CCM nje ya nchi?
Yale ya UK yameisaidiaje nchi toka yaanze kufunguliwa. Ni mwaka sasa hivi lakini hatujaona report yeyote zaidi ya yule mama kuhutumia airport siku alivyofika bongo.
Afadhali ya Mashaka amepeleka mablanket
Badala ya kuona mbele manatazama giza.
We mwenyekiti nani kakuchagua kama shina ndio linafunguliwa? Ndejembi alikua Arusha kwenye serikali sasa wameona ulaji uko huko tuwarithishe watoto wetu.
Nyie CCM nyie dawa yenu ipo jikoni.
Sina moyo wa kunyanyua simu na kuwaambia hao watu wa uhamiaji. lakini ningezaliwa na roho hiyo guarantee ningewaambia kuna watu wanafanya mikutano ya vyama huko. Lakini nawasupport hao hapo juu msipokomeshwa mapema mtatuletea migawanyiko huku na siye hatutaki haya mambo.
Sisi watu wote hapa watanzania. mambo ya CCM, kesho CUF ndio mwanzo wa kuwa tugawanya huku.
Jamani mnakumbuka nili post hapo juu kuhusu suala la kuanzisha ilo tawi la ccm.Nimepata maelezo ya uhakika kwamba sheria inasemaje ktk nchi hii hasa kwa vyama vya kisosholisti na kikomunisti....NI MARUFUKU!jamani hayo mambo yanafaa ktk nchi zingine sio hapa US.Ila kama unataka tiketi ya bure kwenda bongo sawa.Simtishi mtu hii ni fact.
ReplyDeleteHata kama una makaratasi hapa siku hizi wakikuona unafanya kosa au kitu ambacho wanafikiri kitawaharibia usalama wao wanakurudisha kwenu na makaratasi yako. Naturalize citizen ni kama tu Green card siku hizi.
ReplyDeleteNa kama uko shuleni tena ndio hivyo 9/11 walioharibu ni wanafunzi sasa nyie na CCM mtarudishwa nyumbani hata elimu mlioifuata hamjaimaliza.
Hivi mnajua habari za huyu kijana waliye mkatalia asiingie tena huku? [Jina nalihifadhi] Alikua mwanafunzi na ilikua semester yake ya tatu. Lakini toka alivyokuja huku (yeye ni mtoto wa mfanya biashara) hakufanya kazi wala nini summer ya kwanza tu kaenda bongo. Amerudi tu mara mwenzi wa 12 tena kaenda bongo kwenye harusi sijui harusi ilikua ya nani ila mama yake alimtumia ticket. I am telling you that was it. Hakurudi na sababu waliyompa ni kuwa hayo masomo anayosoma viko vyuo vingi siku hizi bongo vinayatoa. So no needs of him to returning here. Mimi nilikwenda kuchukua vitu vyake alivyoacha hapo chumbani kwake manake aliondoka akijua atakaa week 2 hivi bongo. Mara mama yake huko anawaambia watu mwanangu ameamua kubaki tu huku manake anamiss nyumbani sana na pia haoni tofauti ya kusoma huko na huku bongo. nyoooo niulizeni ukweli ndio huo walifreeze na hawakuamini . walifikiri hela yao inaweza kuongea kila mahali.
Msichana mwingine kaoelewa kwa makaratasi sijui alizania ndio kesha yapata au hakujua au kiherehere. Kaenda kwenye harusi sasa wamempa miaka mitatu ndio ataruhusiwa kuingia huku.
USA they don't need a reason to deport you or deny you the entrance back with your documents nowadays.
Msicheze na Marekani mkazania ni kama UK ukideportiwa unaweza kubadili badili address ukahama hama kila siku maisha yanaendelea.
Hapa ni from the little room to the airport. Ukijiondoa mwenyewe ndio wanakupa siku 90 ufungashe virago vyako. Sasa nyie kama mmekuja juzi na pressure zenu take it easy na muwaombe wakubwa zenu muongozo.
Wacheni upumbavu hapa.
Hawa jamaa wanacheza hivi kwanini wameamua kufanya mkutano wao yaani siku mbili tu baada ya 9/11....kwa mtu aliyekaa Hapa marekani kwa muda fulani atajua kuwa wamarekani wanakuwa na mood gani hiyo wiki ya 9/11...sio kitu cha ajabu hata huyo atakaye wakodisha ukumbi akapiga simu kwa uhamiaji au kumwita sherrif....
ReplyDeleteKuna mshikaji amenipigia simu nije hapa kwa Michuzi nione wapumbavu wanaotaka kutuletea mambo ya CCM. Watanzania wote wenye akili timamu tulio hapa USA tuungane kuwamaliza hawa watu wa CCM. Niko kwenye Mwezi Mtukufu na dini yangu inanifundisha upendo kwa kila mtu lakini kwa hili sina cha upendo wala amani na mungu atanisamehe. NITAPIGA SIMU UHAMIAJI ZAIDI YA MARA 10.
ReplyDeleteHaki hata mimi nafanya research ya eligibility ya ku-ran foreign political party in US na kama nikipata documentation nawachongea hamna kikao
ReplyDeleteIsiwe maneno tu bali tunahitaji pia documentation. Please do your homework/research
ReplyDeleteSample:
18 U.S.C 951
951. Agents of foreign governments
(a) Whoever, other than a diplomatic or consular officer or attache, acts in the United States as an agent of a foreign government without prior notification to the Attorney General if required in subsection (b), shall be fined under this title or imprisoned not more than ten years, or both.
(b) The Attorney General shall promulgate rules and regulations establishing requirements for notification.
(c) The Attorney General shall, upon receipt, promptly transmit one copy of each notification statement filed under this section to the Secretary of State for such comment and use as the Secretary of State may determine to be appropriate from the point of view of the foreign relations of the United States. Failure of the Attorney General to do so shall not be a bar to prosecution under this section.
(d) For purposes of this section, the term "agent of a foreign government" means an individual who agrees to operate within the United States subject to the direction or control of a foreign government or official, except that such term does not include--
(1) a duly accredited diplomatic or consular officer of a foreign government, who is so recognized by the Department of State;
(2) any officially and publicly acknowledged and sponsored official or representative of a foreign government;
(3) any officially and publicly acknowledged and sponsored member of the staff of, or employee of, an officer, official, or representative described in paragraph (1) or (2), who is not a United States citizen; or
(4) any person engaged in a legal commercial transaction.
(e) Notwithstanding paragraph (d)(4), any person engaged in a legal commercial transaction shall be considered to be an agent of a foreign government for purposes of this section if--
(1) such person agrees to operate within the United States subject to the direction or control of a foreign government or official; and
(2) such person--
(A) is an agent of Cuba or any other country that the President determines (and so reports to the Congress) poses a threat to the national security interest of the United States for purposes of this section, unless the Attorney General, after consultation with the Secretary of State, determines and so reports to the Congress that the national security or foreign policy interests of the United States require that the provisions of this section do not apply in specific circumstances to agents of such country;* or
(B) has been convicted of, or has entered a plea of nolo contendere with respect to, any offense under section 792 through 799, 831, or 2381 of this title or under section 11 of the Export Administration Act of 1979, except that the provisions of this subsection shall not apply to a person described in this clause for a period of more than five years beginning on the date of the conviction or the date of entry of the plea of nolo contendere, as the case may be.
Pia angalia hii documentation nyingine niliyokutana nayo
http://www.usdoj.gov/opa/pr/2007/December/07_nsd_992.html
Jamani naomba niseme wabongo mlioko marekani mmenikuna! Inaonyesha wazi mlivyokuwa na uwezo wa kufikiri mbali.
ReplyDeleteKuna kitu kimoja watanza walioko ughaibuni hawajakifahamu, CCM style yake ya utawala ni ile ya kikoloni ya "Watenge Uwatawale". Na wanajua wazi nyinyi mlioko nje ndo mmekuwa na upeo wa kuona kinachoendelea huku nyumbani sio sahihi, kwa hiyo wanachofanya ni kujaribu kuwagawa nyinyi kwa sababu wanajua wakifanya hivyo hakutakuwa na ule moto wa mabadiliko ambao umeanza kuwashwa katika tovuti na vyombo vingine toka kwa watanzania wa ughaibuni. Mkikubali wafungue tawi huko maana yake ni kuwa wale msioshabikia siasa za CCM mtaanza kuwa diss wenzenu matokeo yake mtakuwa hamuelewani kama ilivyo kwa hao wenzetu walioko UK.
Aise keep it up guys..mmenifanya nibadili mawazo yangu, nilikuwa nishaanza kusema walioko nje wote ni watu wa majungu!
Pamoja.
Isaac
Kweli bwege bwege tu nikiwaita mafala mtakasilika,sasa nyie wote mmekomaa kuusema ubovu ccm na kumsema bwana ndejembi, mnajua nia yake ni nini? mnadhani kila mtoto wa kiongozi ni mtoto wa fisadi? huyo ndejembi( ndejembi the father) umeshawahi kumsikia kutajwa kwenye any kashfa? msikatishe tamaa viongozi vijana wenye uchungu na wanaojari kuiokoa nchi (huyu bwana ndejembi junior ) ni nape mnauye mwingine ndani ya
ReplyDeleteccm. Bwana NDEJEMBI JR usikate tamaa, hao wanaosema hawana hoja na ni watu wabwatukaji wasio na msaada na nchi yao.
Jamani hawa watu sio wajinga, hawakukurupuka. hili la kuanzishwa ccm hapa marekani nililisikia toka bongo walipokwenda kupata ufafanuzi juu kuanzisha tawi hilo ktk moja ya ofisi za wahusika MSIJIDANGANYE, KINA NDEJEMBI SIO MANDONDOCHA, na binafsi ninaunga mkono, tena kwa mikono yooooote miwili. kip it up boy!!
ReplyDeleteHivi hao wajinga wanaielewa ITIKADI ya Chama. Ni kweli halmashauri ya chama ambayo inakutana huko Dodoma inautambua ufunguzi huo wa shina Missouri Marekani???
ReplyDeleteNyie mnaojifanya kumetetea huyo Ndejembi wenu basi mwambie na wapambe wake wakutane siku hiyo kwenye hiyo address iliyowekwa hapo juu. Nawahakikishia mtaona kitakachotokea. Tumeshafanya background checks ya Michael Ndejembi na Deogratias Rutabana na tunazo social security numbers zao na details nyingine zote. Hili suala tunalichukua umuhimu wa hali ya juu na tutahakikisha hawa watu na wapambe wao wanakuwa arrested and then deported. Vyama vya kisoshalisti na kikomunisti vinavyochochea UFISADI na RUSHWA havitakiwi nchi hii.
ReplyDeleteHii ni WARNING kama mnabisha basi watu wa CCM kutateni na tusije kulaumiana baadae. Tumewatadharisha mapema kuhusiana na hili suala.
michuzi na wewe fisadi tu kwani kila mafisadi wanakokwenda na wewe haukosekani, ndege wenye manyoa yanayofanana huruka pamoja,ninachojua mimi kama mafisadi hawataki uchungulie ufisadi wasingekuwa wanakuchukuwa wewe kila waendako inaonyesha kuwa huna cha kuchungulia kwani kama ni timu na wewe uko kwenye first eleven, ndiyo maana baadhi ya maoni yanayoikashifu ccm na hawa wehu wanaoanzisha hilo tawi huyaweki humu kwenye blog yako, najua huu ujumbe hutauweka lakini tunauhakika utausoma
ReplyDeletehiyo misemo ya nyerere bado mnayo tu, wewe alikuambia nani kuwa kuna watu wanaojenga nchi ya tanzania,yeyote unaemuona anapiga kelele ni kwamba ajapewa dili la ufisadi akipata tu kimyaaaa. kwani naona kila anaetoa maoni anadai kuwa watu wa ughaibuni fanyeni mambo ya maana huko ili msaidie tanzania.raisi wako mwenyewe hajengi nchi anachofanya yeye ni kujijenga mwenyewe na mafisadi wenzake kila siku yuko marekani sasa sijui nae keshapata shift ya kubeba box au?. mwenye nchi mlishamfukia siku nyingi kilichobaki sasa ni kudanganyika tu
ReplyDeleteMbega
Office za Kansas INS ni
ReplyDelete9747 NW Conant Avenue
Kansas City, MO 64153
nilijaribu kuwapigia simu lakini sikuweza mpata mhusika labda na nyie wengine mjaribu pia. Mimi nitajaribu tenaa baadye kidogo na kesho siku nzima.
Namba nilizopata ni
(816)-584-1054 ext229(duty officer)
(816)-505-4712 opt. 0 halafu ulizia
naomba tupige simu kwa wingi ili tuweze kumtetea yule mwananchi anayeumia kule vijijini na sehemu mbali mbali tanzania. Wengi wetu hatujaweza kufanya mambo makubwa kama ni kununua mablanketi, madawa au madawati. Lakini hili dogo tu la kupiga simu tunaweza kulifanya.
Kuwepo na haki kuhakikisha waliokula hela za EPA wanafikishwa mahakamani na hatimaye jela. Wananchi wanaumia na Tanesco wahusika wafikishwe mahakamani na hatimaye jela. haki itendeke kwa wafanyabiashara watatu waliouwawa na polisi. Heko kwa akina Nape na Nchimbi. Mungu ibariki Tanzania
wadau msikonde sisi tuko hapa kansas city na huyu Deogratius tunajua anakokaa 39 & Baltimore st na huyo kennedy anakaa kwenye moja ya kitongoji cha hapa kc kinaitwa lee summit, tutawakolimba halafu taarifa zao tutampa fisadi mwenzao michuzi awafahamisheni
ReplyDeleteNyie chongeni tu nchi inaliwa na kwa upumbavu wenu mnadiliki hata kuwakatisha tamaa wenye moyo. Sasa wewe unadai una green card sasa kinachokuwasha nini? kuwalaumu kina ndejembi, umeamua kuisaliti nchi, ndugu zako na marafiki kwa tamaa ya maisha mazuri mbaya zaidi huthamiki hapa wala bongo kwani huna elimu na kwa namna mnavyotoa maoni mnaonekana kabisa hamjasoma na hamuwezi kurudi bongo.
ReplyDeleteTumuache ndejembi aungane na kina mwakwembe kusafisha chama.
Ningefurahi sana kama Bwana ndejembi angewajibu hawa mafala wanaojifanya wanauchungu na tanzania, unajua nyie msisingizie ccm ungumu wa maisha mlionao unatokana na ujinga wenu wa kuamini kuwa marekani ndio suluhu ya maisha yenu mmesahau hata kufikiri namna ya kuisaidia nchi yenu. Mnadai jumuia za kitanzania, ni nani atanimpa mfano wa jumuiya yoyote ya kitanzaniailiyopo hapa marekani au hata nchi nyingine iliyofanikiwa japo kidogo tu ikawa mfano wa kuigwa. UPUMBAVU umewajaa sana nyie
ReplyDeletendio maana kila kitu kweni ni kupinga tu, mbaya zaidi hamtoi suruhisho. Aiiseeh! nawahofia sana watanzania maana ujinga umewaelemea sijui ni lini mtajitambua na kuweza kuwashemu wanao waongoza.
UNAJUA WENYE NIA MBAYA NA JAMBO LOLOTE HUFANIKIWA IKIWA WENYE UWELEWA NA UWEZO WA KUKEMEA WAKIA KIMYA, MAFISADI WAMEFANIKIWA SANA KUFISADI NCHI KWA KUWA NYIE MNAJIONA MNAJUA HAMKUCHUKUWA HATUA YOYOTE ZAIDI YA KUBWATUKA TU KAMA MAJUA, HAWA WANAOJARIBU MNAWAONA MAFISADI SIJUI KAMA MNAELEWA MAANA YA FISADI NA NAMNA ULIVYOFANIKIWA.
ReplyDeleteKAMA MNGEKUWA NA JAPO CHEMBE YA BUSARA NA KWA KUWA MMEAMUA KUIPINGA CCM SI MNGETUMIE JUMUA ZENU KUIOKOA NCHI? ACHENI UMBWEGE.
HONGERA NDEJEMBI HAWA WANAOANDIKA HAPA NI WATOTO WADOGO WALIKIMBIA TANZANIA ILI WAJE KUKUA USA KWA BAHATI MBAYA WAMEISHIA KUWA MABISHOLOLO.
ReplyDeleteENDELEZA LIBENEKE LA KUJENGA CCM USA, KILA JIMBO NA CITY IWE NA TAWI AU SHINA.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
HIVI NDIVYO SHUJAA ANAVYOANZA KAZI YAKE NI KWA KUPNGWA SANA NA KATU HATO KATA TAMAA, UNAJUA UZURI WAKE NI KWAMBA MTAISHIA KUSEMA TU HAKUNA WAKUINUA MKONO KUMPIGA KAMA UNABISHA JARIBU. KAMA HUAMINI KUWA HUYU NI SHUJAA FUATILIA HISTORIA YAKE YA MAISHA YA SHULE NA MAISHA KWA UJUMLA THEN UTAELEWA, NA WANAOMSAPOTI SIO WAJINGA NA WALIKUWA NA MISIMAMO KAMA YAKWENU WAMEMUELEWA NDIO MAANA WAKO NAE, NINGEKUWA MAREKANI BILA SHAKA NINGEKUWA NAE BEGA KWA BEGA.ACHENI USHENZI WENU KAZI KUROPOKA TU NDUGU ZENU WANAISHI KWA MSAADA WA MUNGU NYIE MMEKALIA MAJUNGU TU SAA UNADHANI NDEJEMBI AKIACHA NDIO MAFISADI YATAKWISHA? ILE HALI NYIE HAMNA MSAADA WOWOTE? NYIE KWELI MABWEGE.
ReplyDeletehembu niambieni kuna mwenye ushahidi kuwa huyu bwana ndejembi ni fisadi au familia yake ni ya kifisadi? naona kama mnakosea jamani. na nimeambiwa huyu bwana yuko houston na ni mkarimu sana sasa kama ni hivyo ni nini kinawafanya kumpinga?, nadhani ni wakati wa kusahuriana ama mngemshauri bwana ndejembi namna ya kuform umoja wenye nguvu hapa marekani ili tukawaondoe mefisadi wa kweli kule bongo.
ReplyDeleteNAUNGA NA WEWE MZEE, NILIDHANI LEO NI SIKU YA HAWA MAJUHA TU, KUMBE WAPO PIA WENYE BUSARA KAMA MIMI. NAUNGANA NA WEWE MZEE TUMSAPOTI KIJANA NDEJEMBI(NIMEAMBIA NI BWANA MDOGO TU SEMA NI KICHWA KINOMA) TUKAOKOE NCHI. NIWAULIZE HAWA MAJUHA UMOJA WA JUMUIA UMESHINDIKANA, UMOJA WA KIDINI UMETUSHINDA NYIE WAJINGA NI UMOJA GANI MNAUWEZA?
ReplyDeleteNYIE WANAOJIFANYA WATU SAFI SI NDIO WANAOKULA PESA MICHANGO YA MISIBA KILA SIKU? NYIE SIO MAFISADI? AU KWA KUWA HATUSEMI?
ACHENI UJINGA NYINYI ENDELEENI KUBEBA BOX MLIKUWEPO HAPA KITAMBO HAMKUONA HAJA YA KUISAIDIA NCHI WAACHENI WENYE MOYO SAFI WATUONGOZE.
NDEJEMBI WAACHE WATUMWA WAISHI KWENYE NCHI YA UTUMWA HAWA HAWAELEWI HATA KWA MSAADA WA YESU. KAZA BUTI NYOOSHA MGUU, SIKUJUI KAKA BUT ULIFANYALO NAAMINI NI KWA MANUFAA YA NDUGU ZANGU PIA.
ReplyDeletehuyu Ndejembi sio OBAMA BUT NI MTU WA AINA YA AKINA OBAMA mkishirikiana nae mtafanya kitu japo kidogo kwa ustawi wa tzania, lakini kwa mwendo huu wa kukosoa, mtawapoteza wengi na kubaki watumwa kwenye nchi za watu ile hali kwenu kuna chacha.
ReplyDeletehivi kuna mtu amewahi kutoa wazo lake ni vipi sisi watanzania tulio nje tushiriki kuokoa jahazi kule nyumbani? hata mabalozi wameshindwa, kama hakuna hamuoni kuwa kuna haja ya kukaa na kina ndejembi kuona wao wanataka kuisaidia vipi nchi ili nasisi tutoe mawazo yetu na kisha tuyasimamie wote kwa pamoja. Mimi namwona ndejembi kama kiongozi aliyekuja kutuunganisha ili tukatoe mchango flani kwa taifa letu. TUMUUNGE MKONO.
ReplyDeleteKAAAAAAAAAAZI KWELI KWELI! Naona mmeamua kutoa mawazo yenu kwa upande hasi, haya basi semeni tufanye nini and how if not enogh nani atuongoze kuisaidia nchi? kina ndejembi si mnawaona hawafai? mkishwindwa mjue hamna sababu ya kumpiga bwana ndejembi na mtakuwa medhihilisha ufinyi wenu wa fikra.
ReplyDeleteBIIIIIIIG UUUUUP NDEJEMBI!, C! C!M!, C! C! M!, C! C! M!.
ReplyDeleteDOGO ACHANA NA WATUMWA WA KWELI WA KIFIKRA, NDIO MAANA TUKO NYUMA HATA WAKENYA NA WAGANDA WAMETUZIDI, MNATUMIA MDA MWINGI KUKANDYA BADALA YA KUSHAURI, MNALETA UBABE WA KISHENZI BWANA, ETI TUSINGEKUNYWA NAE MAJI, OOH TUTAWAITA WAJOMBA! THEN IWEJE AKIRUDISHWA BONGO WE UTAONGEZEA PAY CHECK?
NINYI NI WAFA MAJI HAMNA JIPYA BONGO HAKURUDIKI MAREKANI HAKUKARIKI KUJIHALARISHA MNAJIFANYA CCM MBOVU.HIVI HAMJUI KUWA UJENZI WA TAIFA LOLOTE LINATEGEMEA WANANCHI WAKE?.
Hao wa halmashauri wamewapoteza hawa mwaka huu.
ReplyDeleteWanaowasifia hawa ni wakwao au wenyewe wanasema ili wasione aibu lakini mwenye akili anaona in black and white. There is no gray color here.
Kuna law inasema IF YOU SEE SOMETHING SAY SOME. You don't need to have a reason.
Ni kuwaambia tu kuwa wanarecruite watu wajiunge na chama na tunajua hiki chama cha kisiasa kitawaganya watu na kitaleta machafuko tukiwa hapa katika jumuiya yetu. That is it...
I am going to report this. Mubadili number zenu, mubadili muda au mfanyie mikutano chumbani kwenu majina tunayo.
Siye tulishawekwa kwenye rada kisa mume wangu ana jina la kiislamu na alikua ana nywele refu sana. Sasa niulizeni ni mara ngapi tulisha hojiwa hapa na kufuatwa fuatwa bila sababu. Kama mambo yetu yangekuwa ni ya hivi hivi tungekua tunaongelea bongo sasa hivi.
Tukiwaachia tu basi mtaendeleza uchafu huu kila kona na kutugombanisha hapa USA. Umoja wenyewe wa watanzania tunausotea kwa nguvu sasa mkileta mambo ya CCM na asiye CCM afanyaje? Aanzishe chama chake?
Hivi those people back home thought about that???? Crap ....
Wabongo wa marekani wameniua na kicheko...hehehe
ReplyDeleteWatu wana ma-biti ya kijinga humu ndani. Kwa mfano Anon wa September 11, 2008 9:36 PM. Eti social security number, nk tunazo...sijui hawa watu watakuwa deported. Wewe umesikia ni illegal immigrants hao? Wacha kunivunja mbavu hapa.
Mimi sio mkereketwa wa CCM...lakini nadhani mnaoishi marekani mnatambua na kuelewa katiba ya huko vizuri na mambo ya bill of rights na uhuru watu walionao. Hizi sio enzi za Cold War tena na mambo ya McCarthyism sijui usingizie mtu ni Mcommunisti...hehehe. Bush amekutana na Kikwete mara ngapi? unadhani hawatambui chama chake. Au mtasingizia ni magaidi...hehehe.
Mimi sielewi...Sasa wao wakikutana na kuanzisha tawi inawauma nini? Na nyie si muanzishe cha kwenu cha wapinzani!! Shida hapo ni nini?
"Kidumu Chama Cha Mapinduzi"
hapo wote mnatakiwa kuitikia: "KIDUMU"....hehehe
Au mnamsahau baba wenu wa Taifa...hehehehe
Huyu Dejembi kaja marekani sijui mwaka jana. Watu wamekaa Houston tangu enzi za I-10 iko two lanes na hawajawai kuweka Tawi la CCM wala Kanu. Ninachomwambia ni kwamba awe muangarifu sababu Houston ni popular kwa kususa, Na watu wanaweza kususia hata msiba wake. Hatupendi Upuuzi... Mimi nitatafuta namba yako na kukupigia official kukwambia okome tabia za kishwain.
ReplyDeleteFungua tawi la CCM mexico city sio kwenye aridhi ya democracia
HUYU BWANA MICHAEL NDEJEMBI NAFAHAM KIDOGO NILIKUTANA NAE KAMPALA KWENYE MKUTANO WA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU VYA EAST AFRIKA MWAKA 2005, NILISHAWISHIKA KUMFAHAM KWANZA KWA KUWA WOTE TULIKUWA TUKITOKA TANZANI JAPO KWENYE VYUO TOFAUTI, KUBWA ZAIDI NI UWEZO WAKE MKUBWA KUJENGA HOJA NA KUZITETEA, WAGANDA NA WAKENYA HAWAKUAMINI KUWA JAMAA NI MBONGO,
ReplyDeleteKI UKWELI ALITUBEBA WABONGO. SINA HAKIKA KAMA KUNA ANAEMJUA VYEMA HOFU YANGU NI KWA WATANZANIA KUWAKATISHA TAMAA VIONGOZI KAMA HAWA WALIOAMUA KUTUSAIDIA
Nimestukia huyo Ndejembi ameandika comments kibao na kujifanya ni mtu tofauti huku akitetea CCM.
ReplyDeleteTumeshawaambia jaribuni kufanya huo mkutano wenu halafu muone kitakachotokea ni nini. Hatuitaki CCM ndani ya Marekani iishie huko huko Bongo kwa mafisadi wenzenu. Ndejembi na wenzako tutahakikisha tunakurudisha Bongo pretty soon. Jamani na kesho simu ziendelee kuhakikisha agents wa ICE wanawakamata hawa wajinga wa CCM.
Mimi simfahamu vizuri huyu Ndugu Michael Ndejembi, lakini kama mnasema ni mpole na anaupeo mkubwa wa kusaidia watanzania... nafikiri ingekuwa vizuri kama asingefungamana na vyama vya kisiasa (CCM)! watanzania waliopo majuu wanahitaji mtu aliyepevuka kimawazo ya jinsi ya kuikomboa tanzania na watanzania wenyeje kwa kushirikiana wote kwa pamoja... LAKINI MAMBO YA CCM hii itatugawa watanzania badala ya kutuunganisha, kumbuka wengine tuliondoka tanzania kwa sababu ya CCM na sera zake mbovu, sasa wewe unatuletea mashina na matawi yake huku tena... jamani tukimbilie wapi?, namuomba huyu Ndejembi kama anafikiri anamawazo mazuri ya kuwasaidia watanzania..basi njoo bila kujali mambo ya kisiasa. vijana wa majuu tunategemea kumsikiliza mtu aliye neutral na vyama vya siasa!
ReplyDeleteMwalimu alisema mabadiliko ya nchi yatatokea ndani ya chama na si upinzani! mnajua alimaanisha nini?? naomba jibu. mdau uk
ReplyDeleteBaadhi ya wachangiaji mnataka kupotosha hoja ama kwa kutojua au kwa makusudi. Hakuna mchangiaji ambaye amesema anamchukia ndejembi kama ndejembi au kuwa na mashaka ya uwezo wake wa kuongoza na akademia, au kwamba asiwe mkereketwa wa ccm. Na ni kweli upinzani wa kweli unaweza kutoka ndani ya ccm. TUNACHOPINGA HAPA NI KUFUNGUA MATAWI hapa USA. Aliye na nia ya kutaka kuwa kiongozi wa ccm na kusaidia nchi akafungue matawi huko bongo.
ReplyDeleteWe anony wa 11:48am Mwalimu alishakufa, lets tugange yanayokuja, watanzania wenyewe kwa umoja wetu tutaleta mabadiliko ndani ya nchi, pia usituite wapinzani, sisi si wapinzani bali tunatofautiana sana kiitikadi na kimaono... babu alishakufa we can make our own history as free from political parties! NINAOMBA WATANZANIA WOTE TUISHIO NJE YA NCHI HII ISSUE IWE NI MWAMKO KWETU KUWA NA UJOMA WA NGUVU UTAKAOLETA MABADILIKO NYUMBANI...
ReplyDeleteSisi wa houston, ccm tutaisapoti, kwani tuna nia kuwasaidia washkaji bongo. Simuoni anaetoa hoja ya msingi yakupinga, wengi wanaonyesha chuki isiyo na msingi, mbaya zaidi tunaanza kutengana wenyewe kwa vigezo vya itikadi za kidini. kama hamuitaki ccm jiungeni na democratic au republican kama zinawatambua.
ReplyDeleteNimetoka kuongea na jamaa wa Immigration Office muda si mrefu uliopita na wamesema wanalishughulikia vilivyo hili suala.
ReplyDeleteWe anony wa huston 5:08 PM usiwe mbumbumbu! Wamarekani wametapakaa kila pembe ya dunia, ni wapi ambapo umesikia wamefungua matawi ya democratic au republican. Hii haijawazuia kuwa wanachama wala wakereketwa wa vyama vyao. ndio maana wanapiga maendeleo makubwa. siasa za ukereketwa ni nyumbani sio katika nchi za watu. vijana wa ki-tz mmesomea vyuo gani jamani!!!!
ReplyDeleteHuyu jamaa kayataka mwenyewe, unapoweka kitu ndani ya blog is free for discussion to everyone.
ReplyDeleteUmtete , usimtetee it all ok.
Watu hapa sio wanaipinga CCM , bali hawataki kufunguliwa matawi yake hapa USA. Kama unataka kuwa CCM nenda TZ matawi yanafunguliwa sana huko.
Watu hapa USA walikuja Kusoma , hivyo wengine bado wana- strugle kusoma na waliomaliza tayari wana-strugle na Ku-cope na maisha. Na walioamua kuondoka pia wana-strugle na maisha bongo au ku-cope na maisha huko vile vile.
Unapoona watu wanaandika hawataki matatizo lazima muelewe kwamba hawajamaliza mambo yao huku na wan-struggle sawa na watu nyumbani.
Angalia pesa watu wanazotuma huko TZ kwa familia zako na msiongee mambo ya kusema watu eti hawasaidii familia zao.
Acheni kufungua matawi ya CCM hapa marekani.
Asanteni sana watanzania wa US kwa mpambano mzuri. Je kuna mnaweza kuweka details za Michael Ndejembi na Deogratis ili tuweze kabisa kuong'oa shina. Vitu kama social, address, sehemu za kazi ili kama kuna dosari yoyote ni kuwachongea. Nia ni kuhakikisha hii kitu haitarudia tena.
ReplyDeleteHatumchukii Ndejembi kwa vile wengine hilo jina ndio mara ya kwanza kulisikia na hatumjui kabisa. Tunachukia mambo ya kuja na kuleta vyama vya kisiasa nchi hizi hatutaki.
ReplyDeleteHivyo vya UK, India na uswahilini kwingine vimesaidia nini? Unatafuta title wewe a kuwa "mwenyekiti wa CCM-USA" tafuta uwenyekiti wa international student utakusaidia kupata Ubunge bongo.
Awe na makaratasi au maplastic. Sheria ni sheria. Tunajua sheria za nchi hii na to be a good citizen tunakuabide by the law.
Na Jumamosi nipo home nitawaeleza hao uhamiaji soon mtasikia huyu mtu na makaratasi yake.
Asyliums waliokuwa wamepata citizenship tumeona wakirudihswa kwao Congo kwa vile wanakutana na kuanzisha vimikutano vyao sasa hawa ndio watajua.
Ati wamepata mwongozo wote kutoka Halmashauri kuu Dodoma. Go to the Attonery of State kuomba kufungua chama sio uende Dodoma.
Wewe kaka sifanyi hivi kwa vile nakuchukia lakini nitafanya hivi kwa vile tumechoshwa na CCM kutaka kugawanya watu nje na ndani ya nchi.
Jamani Umoja ni nguvu kila mtu piga simu tu popote ulipo and the good thing is you can stay anonymous.
unajua kama uwepo wa matawi ya si si emu hapa marekani yatawagawa au yameshawagawa watanzania basi nitakuwa na mashaka sana na uwelewa wa watanzania kuhusu democrasi. yaani tumtenge mtu tu kwa kuwa ni mwanachama au kiongozi wa chama furani!!? hainiingii akilini kabisa, tunaweza kumpinga mtu sio kumtenga na ni vizuri tukaelimishana juu ya hali hii kwani ikiachwa itatupeleka pabaya zaidi. kama hatukubaliani na sera za chama anachokiamini mwenzetu ni vema kukaa pembeni kuwaacha watakaokubali kujiunga nae, na sisi tuendele na itikadi zetu za kuamini vyama vingine au kuwa undecided.
ReplyDeletetunaoamini kuwa matawi yatatutenga mjue kuwa sisi ndio wabaguzi na ndio tuopaswa kupingwa na kutengwa kwani ndio tunaoneza siasa za kutengana kwa itikadi za kisiasa(sisi ndio waleta mgawanyiko ktk jamii). Nashauri tukosoane bila kuwakwaza wenzetu na kuleta utengano katika jumuia zetu.