makamu wa rais dk mohamed ali shein na waziri mkuu mh. mizengo pinda wakifuturu jana nyumbani kwa makamu wa rais. wa pili shoto ni kaimu mufti mkuu, sheikh suleiman gorogosi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Pinda mkao gani huooo...?

    ReplyDelete
  2. We annon 10:21pm..... Swali gani hilo unauliza na mbona hujauliza kwa nini Pinda hana kibandiko (a.k.a. baraghashia)? Huo mkao wa wenye vibandiko unahitaji mazoezi. Mimi mwenyewe huo mkao nishajaribu nikashindwa. Nadhani hata wadau wenzangu mtaniunga mguu na mkono.

    ReplyDelete
  3. anon wa sept, 29, 10:21 umenivunja mbavu zangu :) huo ndo mkao wa kukuna nazi ha haaaaaaa!!

    ReplyDelete
  4. ulitaka akaaje? muhimu kukaa au kufuturu ndugu yangu, halafu uwe na heshima kidogo huyo pinda ni waziri mkuu usimwite weee kama mwanao! jifunze ustaarabu na ukirudia tena nitakufuatilia hadi nijue ulipo kisha nikakuhifadhi mahali ili uwe mstaarabu

    ReplyDelete
  5. Wadau mi nina swali moja, hivi viongozi wa serikali wanavyoandaa futari huwa wanatumia hela zao za mfukoni au hela zetu sisi walipa kodi? Dr Shein last week alifuturisha Pemba na jana Kafuturisha DSM naomba kujua jamani.

    Mdau,
    Columbus,Ohio.

    ReplyDelete
  6. NIMEKUWA NIKISUBIRI FUTARI ILIYOANDALIWA NA MKUU WA WILAYA YA NANNIHII AMBAYE SASA NI MHESHIMIWA BALOZI WA NANIHII....TUNAWEZA KUTUMIA FUTARI HIYO KUMPONGEZA MKUU HUYO KWA KUPATA VYEO VIWILI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA NA KUJADILI SUALA LA FULANAZZZZZZ NA MAMBO MENGINE YA GLOBU HIII!!! LAKINI INAELEKEA MHESHIMIWA MKUU WA WILAYA ANAENDEKEZA LIBENEKE LA ZIARA ZA NJE NA VEKESHENI

    ReplyDelete
  7. Wadau nisaidieni, mimi sijui.
    1. Futari ni kwa waliofunga tu au wote?
    2.Futari hutolewa ili watu wasio na uwezo wa kupata hiyo futari nao waweze kufuturu au hata watu wenye uwezo wa kupata futari wajimix humo humo?

    ReplyDelete
  8. MBONA VIONGOZI WA UPINZANI HATUWAONI WAKIKARIBISHWA KWENYE HIZI FUTARI? AU DINI HAIRUHUSU? NI VIPI WANAKARIBISHWA VIONGOZI WA CCM WASIOFUNGA NA KUWAACHA WAUPINZANI WALIOFUNGA? FUTARI HIZI NI ZA UPENDO KWELI AU ZINA LAKE JAMBO? MAANA WAANDAAJI NI WAFANYA BIASHARA WANAOSAMEHEWA KODI KWA MIAKA.

    ReplyDelete
  9. Alieuliza kuhusu wapinzani amuombe Michuzi aweke tena picha za ramadhan ya mwaka wa jana.

    ReplyDelete
  10. Anafuturisha kwa pesa ya serikali sasa wewe unataka nini au unasemaje, umeumia. Zingekuwa zimetumika kupamba ofisi ya ikulu kwa ajili ya krisimasi ungesema?

    ReplyDelete
  11. kanifurahisha mhe. pinda alivyopinda miguu akiteremsha kaimati na vitumbua ah!!nimecheka sana!!

    ReplyDelete
  12. Anony wa 7:02PM, ngoja nikusaidie huyu muulizaji akionaga mambo ya waislamu huwa anapataga kigugumizi kweli, sasa nataka kumuuliza sio kupamba tu ikulu kwa ajili ya kirisimasi, yaani maofisi yote ya serikali yanavyopambwa kirisimasi, mapati ya kusherehekea kirisimasi na mwaka mpya, pesa huwa zinatoka mifuko gani? Mbona huwa haulizi, isitoshe hayo maandazi, kalimati, bajia, na ndizi mzuzu na tambi ndio zamtoa roho? Mbona mabia na makuku ya party za mwaka mpya hawasemi? Au utadai mwaka mpya ni wa wote? Hapana waislam wana kalenda yao na mwaka wao mpya, wahindu na mwaka wao mpya, na wachina na mabudha nao wana mwaka wao mpya. Huo mwaka mpya huwa unasherehekewa kila mwaka kuhitisha miaka kadhaa tangu kuzaliwa kristo. (kuna AC, na BC)

    ReplyDelete
  13. Ahsante anon wa oct 01,12:25 AM tena huyu jamaa imekuwa kila akiona habari za waislamu hutafuta japo kijisababu chochote cha chuki chuki hivi,ili mradi atie watu dhiki tu, hebu wacha zako wewe wacha wazee futari iwateremke kwa raha zao, utaumwa hivyo hivyo tu kama mwiba ulokusakama kooni pole!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  14. wakishafuturisha ndiyo wanawasahau kabisa waislamu mpaka ramadhani nyingine. huku ni kujikosha tu.

    ReplyDelete
  15. Wait .... Hilo ni swala binafsi, sio la ofisi ya makamu wa rais bali ni la makamu wa rais (ukishindwa kutafsiri utajua mwenyewe). Kuwaalika wapinzani sio lazima, ila inajenga utaifa. Hata hivyo, hiyo ni sio sherehe ya kitaifa bali ni futari, na muandaaji anaweza kumualika yeyote aonae anapendezwa nae. Mbona usiulize Kikwete yu wapi, au Sita?

    Na nyie mambumbu hapo juu, msifanye mjadala kuwa wa udini. Pelekeni udini huko ...nanii wanakopigana wakristo kwa waisilamu. This is Tanzania, hatuna na hatutaki mambo yenu ya udini humu. Shenzi nyie.

    Najua michuzi utabania comment yangu kwa kuwa ina neno shenzi, lakini wont without it >> wenye udini, ukabila na 'uchama' usiozingatia utaifa ni washenzi hadi mwisho wa dahari. Ukisoma ukabana, bado meseji itakuwa delivadi kwako pia.

    MZEE SHEIN, TAKE CARE, WEWE SIJAKUONA UKITAJWA KWENYE ORODHA YA MAFISADI... VIPI WEWE 'HULI?' MKUU PINDA NAE TUNAMFUATILIA. I LIKE HIM BECAUSE HE IS VERY GENTLE! MOLA AWALINDE NA KUWAJALIA SIHA NJEMA NA HEKIMA ZAIDI YA ZILE ZA MFALME SULEIMAN (ila msizitumie kuwa na wake wengi wazee).

    ReplyDelete
  16. Watu wengi hufikiri udini ni kufuata dini, bali udini ni kuwakunjia (kona, korosho, roho mbaya, husuda n.k.) watu wa dini nyengine.

    ReplyDelete
  17. Sikujua kuwa mpaka leo kuna mijitu ina udini mpaka basi, sasa mtu kuuliza kama ni hela za serikali ama za kwake, watu ooh krismass etc. Muwe na tabia za kuvumiliana!!!

    ReplyDelete
  18. hahaha, pinda unakuna naz au

    ReplyDelete
  19. kaz, kweli kweli

    ReplyDelete
  20. Mdau wa Columbus Ohio, unaniabisha, mbona uko cheap hivyo. Watu wasisocilize? Tumekuwa Warusi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...