"....asante sana shemeji, karibuni tena..."ndivyo JK na rais omar al bashir wa sudan wanavyosema wakati wa kuagana na mai waifu wa kila mmoja wao jioni ya leo baada ya JK kumaliza ziara ya kikazi ya siku mbili hapa khartoum. chini JK akiongea na waandishi wa habari kama mwenyekiti wa umoja wa afrika huku rais omar al bashi akiwa pembeni leo mchana ikulu ya khartoum. stori kamili soma chini hapo
Umoja wa Afrika (AU) utalifikisha tena katika Umoja wa Mataifa (UN) suala la kutolewa kwa hati ya kukamatwa kwa Rais wa Sudan, Omar Bashir kwa nia ya kuahirishwa kuchukuliwa hatua hiyo, ili kutoa nafasi ya kutafuta kwa amani katika eneo la Darfur nchini Sudan.
Badala yake, AU itautaka Umoja wa Mataifa kuelekeza nguvu zake katika kwanza kuleta amani katika eneo hilo la Sudan na kuondokana na mateso makubwa ya binadamu yanayosababishwa na hali ya sasa.
Msimamo huo wa AU umeelezwa leo (Jumatatu, Septemba 8, 2008) na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya Sudan, mjini Khartoum, mwishoni mwa ziara ya siku mbili ya kikazi katika Sudan kwa mwaliko wa Rais Bashir.
Amesema kuwa AU inapenda kuona hati hiyo ya kukamatwa kwa Bashir chini ya Mahakama ya Kimataifa ya Uharifu (ICC), inaahirishwa kutekelezwa kwa sasa na kuwa ombi hilo litawasilishwa katika Baraza la Usalama la UN.
Akizungumza na waandishi hao wa habari baada ya kukutana kwa mara ya pili na Rais Bashir, mwenyekiti huyo wa AU amesema kuwa Baraza la Amani na Usalama la AU limeziteua nchi za Tanzania na Nigeria kuwasilisha suala hilo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) wakati wa kikao kijacho cha Baraza la Kuu la Umoja huo.
Rais Kikwete amesema kuwa msimamo wa AU na sawa na ule wa Tanzania kwamba kukamatwa kwa Bashir siyo jambo la kipaumbele katika mgogoro wa Darfur hata kama ni vizuri haki ikatendeka ama kuonekana kutendeka katika suala la Darfur.
“Ningependa kusisitiza kuwa nia yetu siyo kupuuza suala la haki. Ni matumaini yetu kuwa pia kwa msimamo wetu tutakuwa hatuonyeshi dalili ama ishara zisizo sahihi, yaani ishara za kuunga mkono uovu. Haki ni lazima itendeke, na kama wasemavyo Wazungu haki ni lazima ionekane kutendeka,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Hata hivyo, tunadhani kuwa katika Darfur, jambo la kwanza na muhimu ni kuongeza jitihada za kuleta amani na kupunguza tatizo kubwa la kibinadamu linalowakabili mamilioni ya wananchi katika eneo hilo, na hivyo kutochukua hatua zozote zinazoweza kuvuruga zaidi hali ilivyo sasa katika eneo hilo.”
Amesema kuwa hatia ya kutaka kukamatwa kwa Bashir hatusaidia kuleta amani katika Darfur, bali kutavuruga zaidi mambo kwa vile suluhisho lolote katika hali ya sasa ya Darfur itategemea sana msimamo na mchango wa Rais Bashir na Serikali yake.
“Tunachosema katika AU ni kwamba tutangulize kufanya yale yaliyo muhimu kwa sasa ambayo ni kuleta amani, kuokoa maisha, kuondoa mateso kwa watu – yaani yale mambo ya kwanza. Hivyo, msimamo ni ikwamba tunaunga mkono hatua ya kuahirishwa kutekelezwa kwa hati hiyo ya kukamatwa kwa Raia Bashir.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Katika hili AU imeonyesha msimamo wa dhahiri. Tunataka kufanya kazi kwa pamoja katika hili kupitia mfumo wa UN. Nimekuja hapa kutoa msimamo na dhahira ya AU wa kufanyqa kazi kwa pamoja na UN, Serikali ya Sudan na jumuia ya kimataifa katika kukomesha mateso ya wana-darfur.”
Mwaka 2005, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ulimkabidhi jukumu la kuchunguza uharifu katika Darfur, na Julai 14 mwaka jana, Mwendeshaji Mashitaka Mkuu wa ICC, Luis Moreno-Ocampo aliitaka ICC kutoa hati ya kukamatwa kwa Rais Bashir kwa uharifu dhidi ya ubinadamu, uharifu wa kivita na mauaji ya kimbari katika Darfur.


wana jamii blogu ..tumpongeze mheshimiwa kwa safari hii ya kidiplomasia.
ReplyDeleteJapo olimpic tulifanya fyongo lakini kwenye politics bendera yapepea na ka-wimbo ketu tuliko-copi na ku-pasti toka kwa Madiba; kanasikika!!
Toka UNO hadi AU.,SADC.......na punde East Afria dederationiiiiiiii!!
Habri ndio Hiyo!!!!!!
au mnasemaje!??
wewe mkuu wa wilaya ya nanihii acha kubana baadhi ya coment
ReplyDelete