JK na mama Salma Kikwete jana jioni walikaribisha watoto yatima ikulu ndogo ya chamwino na kula nao futari n kuwapa zawadi mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Hii ni Sala tosha.Mwenyezi Mungu hufurahishwa na matendo kama haya yakitendwa kwa moyo safi.Basi moyo huo usiishie mfungo wa Ramadhani tu.Laiti Mwenyezi Mungu angezifungua Paa za Nyumba mbalimbali kwa ghafla wakati mmoja basi Rais Kikwette angestaajabu ya Mussa kwa kuyaona yaliyomo ndani katika nyumba zile,watu wakitaabika japo kwa mlo mmoja kwa siku,familia ya watu saba ikilala katika chumba kimoja au viwili,watu waliopoteza matumaini ya kuishi kwa kukosa uwezo wakikabiliwa maradhi ya kila aina pamoja na yale ya akili,na kwa hakika ugumu wa maisha ukizidi kukaza kamba.Namtakia Rais Kikwette mfungo mwema wa Ramadhani.Ukiomba kwa dhati Mwenyezi Mungu husamehe kila kitu!

    ReplyDelete
  2. Hili suala linanikera. Tanzania ni nchi ya waislam na wakristo. walipokuwapo maraiasi wakristo kama Nyere na Mkapa hatukuwaona wanavaa wanavaa nguo za kipadri wala kiuchungaji. hata kama ni kwenda kwenye shughuli hizo baada walikuwa presentable katika suti ama nguo zinazoeleweka. Lakini wanpokuja ndugu zetu waislam ni kanzu tu bakarashea vinavaliwa. unamuona raisi na unaona udini ndani yake kutokana na kivazi. Naomba kuwakilisha dukuduku langu kwa ndugu zetu waislam na kwa heshima tele.

    ReplyDelete
  3. tunajifunza nn hapa !huu ni mfano bora sana kwetu! na usiwe mwezi huu tu iwe ndo utaratibu wa maisha! kwa walio ughaibuni, tulioko bongo, TUWAJALI NA KUWAPENDA MAYATIMA...bro misoup usinibanie...

    ReplyDelete
  4. Ahsanteni sanamheshimiwa rais na 'first lady.Hao watoto Yatima hawako Dodoma tu,wako nchi nzima.Ni jukumu la serikali kuhakikisha wanapata elimu na huduma zingine muhimu.
    Ndugu rais na mama Salma.Pale katika makutano ya barabara ya Morogoro na Msimbazikuna watoto wadogo kati ya miaka 6-12 hivi wamekuwa ombaomba na serikali ya jiji haijali.Ombaomba siyo wazuri'at all'lakini wale watoto wanatia huruma.Niliangalia huku na huku sikuona kitu kama walikuwa na wazazi pale karibu.
    Binafsi niliwaona pale tu lakini
    wanaweza kuwa sehemu nyingine ya Daresalaam au maeneo mengine ya nchi.
    Nina uhakika mh.rais au wasaidizi wako mtasoma maoni yangu.Mungu wabariki watoto wa Tanzania.

    ReplyDelete
  5. Anon wa 4.12 pm

    Hebu acha chuki zako wewe nani alikwambia kofia na kanzu ni vazi la kiislamu?. Hebu rudi dasarani kwanza kasome history. Kuna watu wangapi walikuwa wanavaa hivyo huko nyuma mtu kama Mkapa kavaa sana tu ni vazi la kawaida ndugu yangu acha chuki mungu akupe moyo wa kutafuta elimu.

    ReplyDelete
  6. Kunjibu huyo ndugu yangu.Wakristo wana mavazi kwa viongozi wa dini pekee na sio waumini wao.Waislamu hamna mavazi tofauti kati ya viongozi wa kidini na waumini.Na hapo ndio unapoona tatizo.Au unataka kusema kwamba Rais Kikwete asivae kanzu???Kwa sababu ni Rais???Mbona mwalimu alikuwa anavaa baraghashia yaani kofia zinazotumiwa na waislamu na hakuna alikuwa akihoji???Tuache dhana na kutafuta ubaya pale mbako hamna ubaya.Tanzania tuna bahati ya kuishi kwa amani bila ubaguzi wa kidini.Tusianze leo.

    ReplyDelete
  7. Huyo mheshimiwa wa 4.12 mpe pole
    Kwanza napenda kumjulisha kuwa kanzu na kofia sio vazi la kiislaam, naye mkristo akipenda aweza kulivaa bila matatatizo yeyote. Na unapokuwa raisi wa nchi si lazima usahau dini yako kwa sababu raia wengine wana dini mbali nawe.Zamani sana waislamu fulani Tanganyika walilalamika kuwa hapakuwa na mawaziri wa kiislaam kwenye serekali na mheshimiwa marehemu aliwaambia wasilete matatizo ya dini kwenye siasa. Basi jamaa nakuomba usilete matatizo ya dini kwenye siasa
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  8. Huyo anon wa pili anasumbuliwa na kale kaugonjwa kanakoitwa udini. Tanzania haina dini ila watu wake wana dini, raisi ni mtu pia.

    Katika uislamu hakuna vazi la shehe na mfuasi. Woote wavaa wawezavyo, uchaji si mavazi ni moyo.

    Kama unakerwa basi anza kupiga kampeni msichague tena mwisilamu kwani atavaa kanzu na msikitini ataenda.

    Hii si nchi ya kikristo ebo!!!! Na ina uhuru wa dini. Kuacha kufuata dini yako kwa sababu ya kuogopa waumini wa dini pinzani ni utumwa haswa.

    ReplyDelete
  9. Samahani sana , hilo swala ni kukera wewe ni kwasababu Raisi anafuatilia dini yake au? maanake upeo wako wa dini ni waajabu sana nenda shule soma. Au wewe umeishi katika nchi ambazo huelewi maana ya kanzu na dini. panua upeo wako. Mwalimu Nyerere amevaa sana kanzu na Mkapa na wali hudhuria sherehe za kiisalamu kama viongozi wa kikristo. Mimi ni mkristo na Mtanzania. Sioni baya kabisa. Raisi kuvaa kanzu. Naona Raisi anafnay kazi yake has wakati huu wa ramadhani. Huyo hapo juu anachuki na yuko naive na swala zima. labda hajaziliwa Tanzania. Unasikitisha. Get your knowledge at home In Tanzania is the best!
    Mwana blog;
    Mkristo

    ReplyDelete
  10. INAWEZEKANA LILE SOMO LA UVUMILIVU WA KIDINI LINAHUSU WAISLAMU KUWAVUMILIA WAKRISTO NA SI KINYUME.

    HATUWEZI KUWA SAWA, TUVUMILIANE, TUZOEE UVUMILIVU.

    ReplyDelete
  11. Pumbafu kabisa! tunapoteza maelekeo ya hii mada kuhusu kusaidiwa watoto yatima na wale wasiojiweza tunaanza kuongelea kivazi cha rais. When are we going to be civilized? Yaani ni ujinga tu na ndiyo haya mambo yanaturudisha nyuma kitaifa. Tafashali rudini kwenye mada na achaneni na huyo mpumbavu hapo juu. Mada ni kumpongeza raisi kwa kusaidia hawa watoto na kusisitiza misaada zaidi kwa masikini zaidi ya viongozi kujilimbikizia pesa wakati watu wanakufa kwa kukosa tu maji safi ya kunywa. KAMA HAUNA POINT NYAMAZA!

    ReplyDelete
  12. Anon wa pili acha extremism au fundamentalism

    ReplyDelete
  13. jibu kwa anony wa 4.12 pm...
    kama ulivyokwishaelezea, kanzi na baraghashia haimanishi kuwa we ni musilamu. Na hata kama ingekuwa ina maana hiyo... then so what? As a person Kikwete ana uhuru wa kuabudu dini atakayo ili mradi havunji sheria. Na kama kuipenda dini yake hakuingiliani kwa njia yoyote na uongozi wake, then tatizo liko wapi?

    ReplyDelete
  14. Naona mhe. anaongelea kanzu na kofia ana mapungufu ya kuelewa mavazi, labda nimkubushe tu kwamba Mwalimu pamoja na kuwa mkristo tene "RC" bado aliva kofia kam ahii ambayo Rais JK kavaa na bado alikwenda kanisani na bado hakusema kofia ile ni ya waislamu tuu!! Mbona Mzee Malecela, na hata Mzee Kaunda wa Zambia bado mpaka leo wanavaa "Cho en lai" kwani wao wachina? maana ni vazi la akina Mao Tse Tung!!! Kama walivyosema wadua wengine kwamba huyu mhe. anabidi kuongeza uelewa wake zaidi na hasa kuhusu kivazi na dini na kuwa mwangalifu sana kutojitumbukiza kwenye ugonjwa wa kansa ya dini!!! kha!! mbaguzi huyu.. KABURU wa kidini huyu!!! ni KABURU haswaaaa .. (dRU)

    ReplyDelete
  15. Hili swala la watoto yatima serikali inabidi iliangalie kwa makini...tusiwe tunamwagilia majani maji wakati mizizi mikavu.. kuna tatizo hapa ,,, Jamii inabidi itiliwe mkazo katika Marathi,Elimu na Afya bora!! kila mtoto anataka kukuwa na wazazi wake wawili na ndio elimu ya msingi inapoanzia..Serikali na wananchi tuzidi kuelimishana ili tupunguze hili tatizo la watoto yatima lisizidi kuongezeka..Kikwete Adapt hata watoto wa tatuu basi kuwa mfano kwa wananchi wako.. wanao wakubwa sasa ,, jamii itaiga!! Napenda kuwakilisha..

    ReplyDelete
  16. Eti huyo anon hapo juu anasema kuwa JK ni mdini! Hivi Mrema ni Muisilamu? Kwani namwona nae anavaa kofia kama aliyo nayo JK pichani. Mwalimu Nyerere pia alikuwa maarufu kwa kibandiko cha kibaraghashia. Au ulikuwa hujazaliwa bado wakati anavaa? Jamani wenzetu, acheni chuki za kidini. Tafuteni jingine.

    ReplyDelete
  17. Anon. wa pili pole sana usikereke jitahidi tu kujifunza kuishi na kila mtu na kila hali, hilo ndo tatizo nililokuona nalo unashindwa kukubaliana na hali za wengine unataka sote tuwe kama wewe ambavyo haitawezekana hata kidogo.Kwa kukusaidia ufafanuzi kidogo juu ya tatizo ambalo linakukera kuwa hilo vazi ni la kiungwana tu halina shida,si kwa dini flani makabila mengi pia wakristo wanavaa mfano wazee wote wa kihaya ukipewa mke tu bakora na kanzu ni zawadi muhimu ukichunguza wanaume wa kuhaya si waslam si wakristo wanavaa hilo vazi na wengi tu hulitumia na hasa ijumaa na mwezi wa ramadhani au wakati wa kwenda kuoa waislam sasa hapo ni mahli pake raisi alipolivaa haisumbui angevaa alipokuwa marekani akiomba misaada pale tusingekusumbua,kwani huko angevaa pia isingeharibu kitu almuradi amejistiri. Mbona mfalme mswati amekagua jeshi lake akiwa amevaa kiwinda tu tumbo nene liko wazi hukuchukizwa na alikuwa nusu uchi mbele ya kadamnasi?

    NendaZanzibar ndo utachoka na roho yako Kipindi cha nyuma kanisa la Anglikana,mama zetu wakienda na mabaibui yao kanisani na unapowakuta utawakuta wana baibui wakati wao wakristo akaja padre mpya toka bara akakuta wakinamama wanaingia kanisani na mabaibui akawagomba mno eti wasivae, kitokeo cha hapo mama zetu wakawa wanatoka home wamevaa wakifika mlango wa kanisa wanavua, mimi niliwahurumia sana mama zetu wale wakipata tabu kwa ajili ya mtu mmoja na tafsiri zake potofu kuwa baibui ni vazi la watu flani wakati ni stara tosha mahsusi kwa mama zetu wenye maumbo mapana. basi wamama wale wakawa wanaingia na akiba ya kanga wanajitupia kichwani na maungoni kujihifadhi mpaka ibada inaisha. Kinamama wtu toka bara waliolowea z'bar miaka mingi na watoto wao wanawaita wazalia. ila wanawakubali pamoja na tofauuti zao za kidini na itikadi wenyewe wanaridhiana.

    Uhauri: usiwe na hisia mbaya juu ya kila jambo ambalo linafanywa jaribu kukubaliana na wengine ili uishi maisha ya raha na furaha najamii inayokuzunguka, mnisamehe nimeongea nno.

    ReplyDelete
  18. We are losing the plot here
    Badala ya kushiriki na majadiliano ya matatizo ya wana masikini, zugumzo limepiga kona na kuzungumza dini na mavazi ya kofia baraghashia na kazu huzurungi. Hata mtu mmoja hajasema vipi nchi iwasaidie hao watoto wasiwe yatima pia kwenye elimu na hapo ni dodoma jee huko iringa na uvinza kuna mipango gani ya kuwasaidia watoto kama hao
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  19. Wewe tunazungumza kuhusu cheche zinazoweza kuunguza amani kwa misingi ya kidini. Jamaa kama Anon wa pili wako wengi saana bongo na wanatakiwa waelimishwe. Amani kwanza.

    Anatakiwa ajuwe maana ya udini si kufata dini bali kuwa na chuki kwa dini za wenzie. Tunatakiwa tufike mahala tumsaidie yeyote bil kujali imani yake. Inavyoonyesha Anon wa pili hawezi kumsaidia aliyevaa kanzu.

    ReplyDelete
  20. kweli tanzania ni nchi ya dini zote, lakini sidhani ulikuwa hai wakati wa nyerere, pia alikuwa anavaa barakashea, hizi nguo zisizo julikana nawe zilikuwepo bongo kabla ya wakoloni kuja,mimi nadhani ww umezaliwa ughaibuni,unazungumza kama vile juha ila huchekeshi

    ReplyDelete
  21. Mie katika suula la kidini hapana lakini nijuavyo hilo vazi sio la kidini bali ni la kiarabu.kwani hata kabla uislamu na ukiristu mavazi yaliyokuwa yanavaliwa ni ya aina hayo.Bali changamoto kwa kikwete apime upepo wa aliyoyakuta na alipo. Kwa ufupi nchi imemshindwa.Hata makusanyo ya kodi yamepungua sana!ANATUPELEKWA KWA MWINYIII


    by mangi kariakoo

    ReplyDelete
  22. Hata kama angekuwa kavaa kwa sababu za kidini, JK ana uhuru na haki ya kufuata dini yake kama katiba inavyosema. Au ule uhuru ni kwa wasio waislamu tuuu.

    Na haya maswala ya hisia kwa dini za watu wengine tutayaona ili mradi kuna vikundi vya ki-extremism vimeibuka siku hizi.

    TANZANIA IS SECULAR

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...