Kwa kweli Michuzi, mimi ni mdau mkubwa sana wa blog yako inayotuelimishakila siku.
Mimi ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Nilipata nafasi yakuhudhuria na kupresent paper kwenye mkutano ulioandaliwa na UNESCO nachuo Kikuu Hacettepe huko mjini Ankara tarehe 2-5 Sept. 2008.
Mimi ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Nilipata nafasi yakuhudhuria na kupresent paper kwenye mkutano ulioandaliwa na UNESCO nachuo Kikuu Hacettepe huko mjini Ankara tarehe 2-5 Sept. 2008.
Ila yaliyonikuta katika harakati za kupata viza ya kwenda huko Uturukikatika balozi yako huko nairobi nashindwa hata nianzie wapi.
Nilipata e-ticket tarehe 26, nikaamua kusafiri kwenda Naii kwa ajili yakuaply viza hiyo kwani Uturuki hawana ubalozi hapa kwetu.
Nilipanda prisisheni airline hadi A town ambapo nilipanda Peajot kutokaarusha hadi namanag, afu Hiecetown kutoka namanga hadi naiii, ambao nilifika naii saa tatu usiku.
Nilipokelewa na rafiki angu nilopsoma naye kwa m7 miaka ya 2001-2004,anayeishi Buruburu estates.
Tuliamka asubuhi na mapema tukielekea GIGIRI street palipo ofisi za ubalozi husika, guess what happened...
Tuliwakuta dancers wanaoitwa "Star Dancers" wakitokea mombasa, walikujakwa interview ya visa ya kwenda uturuki na mwenyejiao, buze bize...
Tuliomba kupewa nafasi ya kuwakilisha fomu zetu kwani nilitakiwa kusafiritarehe 31.08.08 na hapo ilikuwa tarehe 27.08.08.
Wale sekyuriti people waliniruhusu kwani nilitokea mbali, na haya ndoyaliponikuta nilipowakilisha fomu.
Cjui cheo cha yule dada aliyekagua fomuzangu na viambatanisho vyote, ambappo niliambatanisha, barua ya mwaliko,barua ya utambulisho kutoka chuoni, paspoti yangu, na e-ticket.
"your documents misses bank statement..." alisema yule dada.
nikamwambia,mimi nitalipiwa na chuo kila kitu, kwani tukisafiri nje ya nchi tunalipwaoff-pocket allawanses, perdiems na subsistance... yule dada akazidikuinsist, nikampa story ya safari yangu kutoka bongo hadi naiiii, dah,kabla cjamaliza akaja dada alokuwa amekaa kwa nyuma, akachukuwa forms zangu then akanambia nikae....
Nikakaaaa kaaa weee,....... then akanirudishia folder nlokuwa nimewekaforms....akanambia...
"YOUR VISA HAS BEEN DENIED"............TRY NEXT TIME"
just likethat...unaweza imagine...
Nilichoka niakwa mpole....cjui pa kwenda....hakuna pa kwendakuappeal....nikawa nawaza,....je ni east african cooperation inavofanyakazi? kwani wale walikuwa purely KENYANS....WALIVONITREAT....NILIFEEL BAAAAD SAAAAAAANA HATA CWEZI ELEZEA.
NILITUMIA ALMOST 500,000TSHS KWENDA HADI NAIROBI AND THAT WAS THE ANSWERSI GOT.
NIKASHINDWA KWENDA KUDEFEND RESEARCH YANGU, NA KUITANGAZA NCHI.
NISAIDIENI WASOMAJI WA BLOG HII, JE HUO NI UMOJA KWELI...NADHANI TUFIKIRISANA...
ASANTE
Mdau Dar
Mhadhiri wa chuo Huria pole sana.For me nadhani hakuna suala la ukenya wala Utanzania hapo.They were doing there job!Labda tu wangeweza kupiga simu kazini kwako ili kudhibitisha udhamini wako,badala ya kutoa jibu la haraka.Otherwise Pole sana.Walikuwa wanafanya kazi yao!!
ReplyDeleteBalozi zote za Uturuki zina matatizo sana kwani ile nchi ya kiarabu pia ina ubaguzi kidogo. Mimi naishi Uk niliapply visa kwenda holiday pale na kwasababu natumia pasport ya Tanzania nilipofika hapo ubalozini niliambiwa niache vielelezo vyangu na nitajibiwa kati ya wiki mbili mpaka miezi sita. Sasa hiyo miezi kweli hiyo holiday inangojea tu ila niliamua kuacha document zangu lakini huwezi amini nilijibiwa baada ya mwaka na miezi 2 ndio nikaitwa kuchukua visa. Niliamua kutokwenda maana nilikuwa sina likizo tena.
ReplyDeleteUlikuwa na barua kutoka hicho ikionyesha watakups full support? Yaani malazi, matumizi na kusoma? Ni kwa muda wa miaka mingapi? My thoughts ni kuwa hawakupata evidence za kutosha kuonyesha kuwa safari yako yote itakuwa sponsored na wao. Kwa hiyo hapo wanaitaji bank statement ya kuonyesha kuwa kunafunds sehemu either za kwako au za mtu anayekusponsor. Kwa hiyo nahisi sababu ya wao kukataa ni kuwa wanaona kuna chnce wewe uka immigrate hiyo nchi na hivyo wanataka kithibitisho kuwa unasababu za kurudi yaani kuomba visa saa nyingione inabidi ubebe extra information ambazo zinaweza kuuliziwa kama bank statement letter from your employer showing you will be back to work etc. Hayo ni mahisio tu lakini wanatakiwa wakupe sababu ya kukataliwa na wewe you had the right to know the reasons right them kabla ujaondoka ubalozini. Unaweza ukapata information zaidi (vitu ambavyo vilikosekana)ukarudi kuappeal lakini itabidi ucheck regulations na procedures za kufanya hivyo. Kila binadamu anahaki lakini ndiyo nchi nyingine inatumia vikwazo tofauti kubagua. Wewe kama kila kitu unacho kinachotakiwa na unahisi ubaguzi umetokea unapeal na hata lawyer anaweza akakusaidia ukashinda kesi. Ila jiandae kwa chochote.
ReplyDeletenani amekwambia unakata tiketi then ndo unaaply visa!! visa ni kama bahati nasibu, first, inachukua wiki hadi itoke, sasa wewe unaenda 27 kutafuta viza huku safari ni ya 31 haikuwa sahihi. kama uliwahi fanya hivyo bongo, ilikuwa ni bahati tuu. but ni jinsi nchi yetu isvyokuwa na wasafiri wa uturuki ndo maana hakuna balozi hapo, si uturuki tu, hata nchi nyengine kama slovakia, nk. pole mwaya.
ReplyDeleteSasa mzee pole kwa yote yaliyokukuta,japokuwa naweza kuwa nakosea kwa ushauri wangu lakini huu ni uwanja wa uwazi na ukweli siku nyinge unapo-plan au (kujiandaa)safari yoyote jaribu kuwa na document zote kwani ndio maana ukapewa jibu ulilolipata na sizani kama hao watu wa ubalozi wana makosa wao wanachokifanya ni kufuata taratibu/sheria za kazi.na kwa ushauri wangu kama kutakuwa na muda zaidi unaweza ukajipanga upya kwa kuwasiliana an hao waliokualika au vipi jaribu kuwasiliana na hao waliokualika wakakuongezea muda zaidi ili uwende upya na benk statement
ReplyDeleteMhadhiri you know better,ingetakiwa uweshafanya reseach na kujua ni supporting Doc.gani zilihitajiaka kabla hata ya kwenda huko mbali hivyo,kilichokupoza ni ule uhakika wa kwamba wewe ni Mhadhiri kwenye well recognised institution kumbe wenzako hawagopi hicho.Bongo ukisema wewe ni mhadhiri some people will be a bit scared lakini nchini zingine ni tofauti kidogo.
ReplyDeleteMhe.Mhadhiri weka document zako pamoja visa hautakaa unyimwe maana ni haki yako.
pole.
ReplyDeletehadithi ndefu na precision air na peugeot nk hazina umuhimu.
Ulpaswa kujua kila kitu kabla ya kuomba VISA. that simple.
Acha ujinga wewe nani ka kwambia visa ni bahati nasibu! eh! hiyo wewe na ukoo wenu. Ukiwa na documents zote zinazoitajika katika check list yako hakuna mtu ana haki ya kukunyima visa. Na wewe of all the countries uliona Uturuki kwa wabaguzi hao wamejaa Holland na Germany kama labours!! hawana issue isipokuwa dada zao wazuri tu. ndio hayo tunayokataa na ICO hawana deal hawa watu absolutely nuthing my friends went there wamekimbia wote second yr wako hapa UK an USA sasa.
ReplyDeleteHao wadada kama ni wivu hautawafikisha popote watabaki na jua kali wao hapo Nairobers.
Kuna such personality na kinda people in many Embassies in Africa in the thought that huku ni paradise hell no! u have to work ya ass off as well to get ya bread. Since it's Proposal usife moyo inform them about what happend tafuta hiyo BS soma check list vizuri make sure all requirements ume-meet, we msomi dude, check mara mbili hata tatu then tafuta a friend who can check for you as well then wavae tena wewe mharidhi laki tano is nah that much. Nenda tena don't let any kenyan a**let u down ever Pleaseee na utuhabarishe tena kwamba umepata
Good lucky dude
Dole Gumba
London
Msiwatetee hao akina dada wa balozi ya Uturuki Nairobi, hasa watoa comment wawili wa mwisho(Anony, september 05, 2008, 2:01 AM) mnaonekana kutoelewa kama hawo akina dada. Huyu bwana alikuwa haendi kusoma, alikuwa anaenda kwenye kwenya symposium/ kwa kiswahili naweza kusema ni WASHA, KONGAMANO, SEMINA ya siku moja au mbili hivi na ange-present paper yake pengine ni kwa saa kadha tu, alikuwa anenda kupresent/kutoa mada yake ya utafiti/research paper kama sikosei alikuwa na barua ya mwaliko kutoka chombo husika huko Uturuki, pia alikuwa na barua ya utambulisho toka kazini,kama mtu unafahamu kazi yako ni rahisi sana kuelewa hali halisi ya huyu bwana na kutolea uamuzi, lakini watu huwa wanakariri kazi hawana flexibility, nahisi wao walidhani anaenda kusoma, kumbe yeye alikuwa haendi kusoma alikuwa anaenda kutoa mada katika kongamano ambalo alikuwa amealikwa na nchi ya uturuki yenyewe. TATIZO HAPO LILIKUWA UELEWA MFINYU na kujaji kitu kabla hata mhusika ajasema lolote nahisi wao waliamua hata kabla hajatoa document zake na kuzi-study and three day is just more than enough to study them kwani kuna mtu hapo anasema alikuwa amechelewa eti 27 na anaondoka 31, ndo maana alikwenda in personal, hata kama hizo visa zina fees huwa zinatofautana ya mtu anaye-post na anayekwenda mwenyewe na kutaka visa siku hiyo hiyo huwa analipa zaidi, kitu ambacho kipo na appplicable balozi zote duniani, hata balozi zetu za uchwara huko duniani huwa zinatoa visa siku hiyohiyo. Mimi namshauri aandike barua kwa balozi wa uturuki Nairobi kuelezea mkasa mzima na copy kwa kile chombo kilichokuwa kimemwalika ili iwe kama shule kwa future kwa watu wa aina yake. ELIMU NI KITU MUHIMU SANA, PAMOJA NA EXPOSURE, PENGINE WALIKUWA HAWAJUWI KABISA KU-PRESENT REASERCH PAPER NI NINI KAMA ILIVYOTOKEA HAPO JUU KWA BAADHI YA WATOA MAONI, HAYA MAMBO HUFANYIKA DUNIANI KOTE, HASA KWA WALIMU WA VYUO VIKUU, HATA KWA WATU BINAFSI AMBAO WAMESOMA VIZURI FANI ZAO WASHA ZIKO NYINGI TU DUNIANI TENA UNALIPIWA KILA KITU, KAMA MKALI WA NONDOZZZ MAPESA YAKO NJE NJE YA PAPER PRESENTATION.
ReplyDeleteEwe mzee wa chuo Huria, Sijui hiyo panctuality ulijufunzia wapi..wewe unaenda kichwa kichwa tu bila hata kufanya ka -utafiti, au ulifikiri kwamba ka utafiti kako uliokuwa unaenda ku-defend katika kanatosha!! Ongea na watu bwana wakupe data sio tu kukurupuka kama sungura aliyekurupushwa na mbwa porini.
ReplyDeletePili: Isingewezekana wewe kuondoka tu bila kuwahoji sababu za kuntimwa visa hasa ikizingatiwa kwamba umewalipa viza fees, kama wangekaa kukupa sababu basi wao wezi na ungekataa kuondoka mpaka wahakikishe kwamba either wao wawa-contact hao jamaa zako wa uturuki au wewe mwenye shida...
Kama ni documents pekee, ungewaambia wakupe muda wa siku kadhaa ili u-submit, na hapo ungekuwa na nafasi ya labda kukubali au kumwomba mkeo kama unaye aku-faxie kama wanakubali fax ,hiyo bank statement..na pia ungewauliza ni kiasi gani wangetaka kuona.. maana ungeweza kurudi dar, unaleta benk statement halafu unaambiwa fedha hazitoshi...
Hawa waturuki ni wajinga sana, akina oran, wewe acha tu sisi tunawajua.. hata kimombo chenyewe hakipandi.. kila siku wanataka interpreters hapa UK... ni watu wa benefits na off license..nao pia wan-beg kujiunga EU , nafikiri wanachofanyiwa na wana Eu ndo nao wanataka kulipiza kisasi..
Tanzania nayo iamuke toka usingizini na ku-apply same measures..but I doubt kwani haya yaliyokukumba hayajawakumba ..
Pole sana...
Nchi zote zina sheria ya kuingia kwao na ujue sio lazima wakupe visa kwa kuwa wewe unakila kitu wanachotaka. Wanazo sababu za msingi za kumnyima mtu yeyote visa bila kujali ukaribu au utimizo wa vitu walivyouliza.
ReplyDeleteIeleweke kwamba visa ni ombi na utambulisho wako kwao tu na amri au uwezo wa kukupa visa au kukataa uko kwao.
Ni sawa na wewe unavyoweza amua kumfungulia mlango wa nyumba yako mgeni anayegonga mlango wako au kukataa kumfungulia mlango.Sababu ni zako hata kama huyo mgeni unamjua au ana haki ya kuingia.(Mfano ni pale wewe binafsi unapoweza mnyima mtoto wako ruhusa ya kuja nyumbani kwako)
kuitwa kwenda ku-present sio sababu ya kupewa visa hata kama wao ndio wanakulipia. Huwezi jua hapo ubalozini Nairobi waliongea nini na huko Uturuki- chuoni bila wewe kujua na wao walijibu nini.
Ninachoweza kusema ni kwamba inaonekana hii ni mara yako ya kwanza kwenda kuomba visa katika ofisi za mabalozi, kwa maana kama ungekuwa umesoma nje ya Tanzania ungejua kwamba hili swala la kukosa visa halina uhusiano wowote wa kuwa mfanyakazi ni Mkenya na hata kuwa member wa Afrika Mashariki.
Mabalozi mengi pale Dar- Tanzania wafanyakazi wake ni WATZ na bado wananyima watu (watanzania wenzao) VISa za kwenda nchi wanazozifanyia kazi.Je hiyo pia kwako ni kwamba hawako fair?
Kingine kikubwa na ambacho nimekushangaa ni kwamba wewe kama mwalimu tena wa chuo kikuu huria chnini Tanzania unalalamika kwamba haikuwa fair wewe kunyimwa visa, sasa hao wanafunzi wako unawafundisha nini au degree gani?Maana una- onajana wao (Wanafunzi)pia wakikuhoji au wakigoma kwa kukusa grade zao nzuri ambazo wewe uliwafelisha utasemaje.
Lets be carefull na kulamika kwetu kila mara na hasa pale ambapo sisi wenyewe ndo huwa tumeshindwa ku-present wanachohitaji. Sheria lazima uwe na bank statement ya kuonyesha huko ulikotoka yaani TZ utaweza rudi presentation ikkisha sasa kam ahuna Bank statement- yaani fedha za kununua unga TZ kwa nini wakupeleke Uturuki.
Pole Mhadhiri naona ule usemi wa zamani hapendwi mtu bado uko mbali na wewe. Ingekuwa ni hivyo wewe unavyofikiria basi watu wangeenda every where. Hata kama unaenda kuwakilisha nchi kwenye riadha au ubondia mapesa ni muhimu. Wewe ni professor hivyo nakuomba tena uutembelee ule msemo wa hapendwi mtu. Hiyo uliyokuwa unawaambia katika kazi zinaitwa ni siasa au story. Nenda kajipange vyema and everything should be ok next time
ReplyDeleteMICHUZI NAKUOMBA USINIWEKE KAPUNI, YAWEKE MAONI YANGU
ReplyDeleteangekuwa mtu mwingine nimemhurumia lakini kwa sababu umesema ni mwalimu wa open university nimefurahi kwa yaliyokukuta kwani mtambue kuwa huo ni usumbufu mdogo sana umeumia hivyo na umetumia sh 500,000 tu lakini sisi wanafunzi wenu mnatuhangaisha sana kutupatia majibu ya mitihani watu tumeshamaliza miaka mitatu iliyopita lakini mnapoteza majibu ya mitihani yetu na kutulazimisha wengine turudie mitihani zaidi ya mara mbili. samahani lakini utambue malipo ni duniani na unapomsumbua mwenzako nawe utasumbuliwa. hiyo ni adhabu ndogo sana subirini mungu atawalipia zaidi.
mwanafunzi wa chuo kikuu huria.
kwanza hizo habari za wewe kuchuka sijui presisheni sijui nini na nini hazina msingi wacha majivuno kijana.
ReplyDeletewewe hint to the point inatosha acha mambo ya kuzunguka zunguka.
una asili ya kinoa rwegonanii nini wewe?
kwa taarifa yako sijui mhadhiri gani hujui mambo ya international affairs...visa sio gurantee kupata, ni uamuzi wa ubalozi kukupa au kutokupa huna cha kulaumu.
kwanza info zako hazitoshelezi then unaleta za kuleta....pole lakini ndo ujifunze.
Ndio maan sisi tuko ulaya na pasipoti za EU. Hatuna matatizo tena tunashukuru. Wale wanaosema kwa nini tuwe na pasipoti mbili, sababu imeshatolewa kama ya huyu jamaa hapa. Pasi zetu hazihishimiwi kutokana na umasikini na watu kutoweka wakienda majuu. Japokuwa Uturuki ni walala hoi hapa Ulaya, lakini uchumi wao ni mara 20 ya afrika kusini, tajiri wa afrika yetu.
ReplyDeleteTanzania kama huna pesa ya maana kama Ndugu Michuzi basi ujue kwamba kupata viza itakuwa sawa na kujaribu bahati nasibu iwe Nairoberry au Dar, Afisa atakuwa mkali tuu.
Ndugu michuzi, lini tutaruhusiwa na Bunge kuwa na pasi mbili? nasikia mwaka huu.
Shukurani na kazi njema.
kaka pole sana
ReplyDeletemimi imenitokea kama yako,nilipata intenship kupitia chama cha wanafunzi wa sheria barani ulaya,ilikuwa inafanyika instanbul,wakati nasubmit doccuments zangu walinambia nisubiri mwezi mmoja,nikauliza ili nipate maelezo ya kutosha wakanambia diplomatic relation kati ya tanzania na turkey kuhusu visa ndo huu,kwani kuna nchi zingine ambazo hawaitaji visa kabisa but kwa mwezi mmoja tu ikiwepo kenya,ukraine,russia na nchi zingine za kiarabu,nikashindwa kwenda kwani muda utakuwa umepita,kosa walilofanya hao watu ni kutikuwa wahungwana kwa kukuelewesha vizuri,kwangu mimi hadi simu toka foreign affairs turkey ilipigwa hapo embassy lakini walikataa kwani wanafanya kazi kutokana na taratibu,ila usijari kaka,pole sana.
Annony 10:13 am Kumiliki pasi ya EU ndio nini? Hata watu wa EU pia wako wengi wamekataliwa visa kwenye nchi nyingi, tatizo sio Pasi bali kutimizwa taratibu za uhamiaji, si werevu au sababu ya wewe kubeza wananchi wa nchi za chini, mimi ni mzawa wa Ulaya na namiliki EU citizenship lakini hio si sababu ya ujivuni kamwe, ni kweli huyu Prof. alipaswa aangalie taratibu za kuingia katika Turkey na ajiandae matayarisho yake mapema, pole sana Prof, lakini ofisa wa ubalozi alitakiwa akueleweshe sababu ya kukataliwa na utaratibu kwa vile pengine ni mara yako ya kwanza, kila nchi zina taratibu zake hivo kabla ya kuomba Visa angalia mtandao wa nchi husika.
ReplyDeletebaadhi ya watu humu ukisoma comments zao unahaki hadi unataka kupiga ngumi computer yako.
ReplyDeletetena sijui hawa wapo wapi na naamini hawajafumbuka macho kabisa na masuali ya visa za nchi mbali mbali.
mfano:
kuna alosema huhitaji kuonyesha tickets unapokwenda omba visa! wrong nchi tele zinasisitiza hilo au atleast proof ya kuwa ume book ticket.
alosema oh ni uturuki nchi ya waarabu ni wabaguzi! ubaguzi hauhusiani hapa! n chi tele zina ubaguzi hata tanzania umejaa (tunabaguana kila siku). mfano ni huyo alosema ni nchi ya kiarabu, ku mention asili yao tayari ni ubaguzi !!Jambo lisipokwenda utakavyo usisingizie ubaguzi.
Halafu kuna yule alojisifu kuwa ana pasi ya EU, So what? unadhani kwa kuwa una pasi hiyo ndiyo unaweza kuingia nchi yeyote ile? au unapewa visa haraka? dream on! kuna nchi tele za europe huingii kama huna visa hata uwe na pasi gani. Mfano mzuri ni alo uk haingii rusia, pia hata usa unaingia kama mtalii lakini kama ni kufanya kazi au hata jambo lolote litakalo husisha wewe kulipwa ni lazima upate clearance, otherwise utajikuta pabaya!
Tena halafu mhadhiri wetu na elimu yake yote anafanya matayarisho yake yote ya safari na anangoja hadi siku nne kabla ya kuondoka ndio akaombe visa?! kwa nini hakufanya utafiti na kuangalia kwenye internet ni muda gani inachukuwa kupata visa? kuna nchi unakwenda asubuhi visa unapata jioni, kuna nchi unapeleka leo unajibu baada ya masaa 24, kuna nchi unapelekwa maombi halafu unapewa siku ya kwenda kwenye mahojiano. kwa ufupi kila nchi ina taratibu zake, sasa usipofuata tartibu zao usilaumu mwengine na kuanza kutumia karata ya ubaguzi.
Kama mhadhiri kweli basi check and double check ni moja katika tabia yako, sasa kwa nini hukuangalia katika requirements za maombi ya visa uturuki wanataka bank statements zako?
Mhadhiri weye hujawahi kusafiri kwenye nchi za watu? Bachelor (Dar), M.Sc (Dar), Ph.D (Dar)? Hata conference tu zote Dar? Ni nchi gani ya Ulaya e.g unaweza kupata visa ya ghafla na bila kutimiza vigezo?
ReplyDeleteSina la kuongea la kumwambia huyu mbongo mwenzangu.
ReplyDeleteNinachosema hapa ni kuwa wengi wametowa comments PUMBA kama watu ambao hawajaenda shule.Kuna mmoja tu ninayekubaliana naye(Anon sept 5,5:23Am.)Huyu ndiye nakubaliana naye.That was very intelligent comment bro/sis whatever.Watu wanadhani ukiwa na kila document eti una haki ya kupewa visa.Ulizeni wangapi wamenyimwa visa ya kuja marekani na marundo yao ya documents.Nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 90 tulinyimwa visa ya kuja marekani tulikuwa na paper zote zinazohitajika na bado washenz wakatumwaga.Pia kuna hata wale wanaoshinda GREEN CARD LOTTERY za kuhamia marekani nao huwa wananyimwa visa.fikiria mwenyewe.Kuwa na paper si lazima upewe visa ya kwenda nchi fulani.Fumbukeni.
As for anon 5:23Am you seem very intelligent person.Much more compared to others
Bwana mhadhiri,
ReplyDeleteSamahani sana kwa kukukwaza, lakini ulicho andika hapo ni utumbo mtupu.
Haiingii akilini mwadhiri akawa ametuandikia ujumbe huu tuliouona, nakushauri siku nyingine, usiwaonyeshe watu wewe kichwani kwako hamna kitu.
Ni mara kumi uandike kiswahili kitupu kuliko kujidai kuchanganya lugha.
Ulianza na mkwara mzitooooooo wa kuondoka na ndege, mara sijui Hiace mara sijui Peugeot, haya ya nini?
Tabu yako unataka tukuonee huruma, lakini kama kweli unaandika utumbo kama huu, sijui huko ulikotaka kwenda ungeiteteaje nchi yetu.
Sasa, narudi kwenye swali la msingi baada ya utambulisho. Kuwa na barua ya mwaliko sio sababu, tatizo lililokuwepo hapo ni kuwa hawakujua ni jinsi gani unaweza mudu kuishi huko. Full stop, hakuna kuremba.
Mara sijui mbwembwe za ninapewa sijui perdiem, sijui masurufu nani anataka.
You deserve the BANG brother
paka akitoka panya hutawala...huku ulaya wanadharauliwa na kukataliwa kuingia eu wanafeel better maybe wakipelekesha nchi ndogo nao angalau wajione kidogo. turkey kwanza jamani nani atataka kuzamia dunia hii labda kusoma na kutembea ila kuzamia wao wanyewe wanajaribu kuzamia nchi za watu. weather or not alikua na makaratasi ya kutosha clearly this matter was not handled proffessional. ilibidi kueleza kwanini imekataliwa na nini wanahitaji zaidi.
ReplyDeleteNaombeni niulize! Kwani visa inatolewa na desk staffs? Hao wakenya unaowalaumu sidhani kama wanatoa visa, wao ni kupokea na maybe na kupitia na kuona kama supporting documents zote ziko sawa na kuwasilisha mbele kwa visa kutoka! Kuwalaumu huyo mdada as if yeye ndo alikua na final and conclusive decision ni kumuonea! Tuambie baada ya kujibiwa na huyo dada ulichukua hatua gani? Kama aliona una all supporting docs? Kwanini hukutaka muona muhusika mwenyewe?
ReplyDeleteHukuwa na paper ya ku-present, na it seems ulitaka jibu kama hilo au ulienda tu talii!
Mimi naona you should find a diary uandike kumbukumbu zako. Mambo mengine wala hatutaki kujua ....huko Kenya ulifikia wapi, mlifaamianaje huyo mwenyeji wako, anaishi wapi, ulifikaje that is non of our business....Kiswahili kirefu sana labda ndio maana hawakukuelewa huko.
ReplyDeleteWao wanafanya kazi yao hata kama wawe ni wakenya au waturuki. Tumezoea kila kitu bongo ni kwa mwendo wa kujuana ndio maana tukifika sehemu zenye kutumia sheria tunakuwa wepesi kulalamika.....
Na kama mtu hataki uende nyumbani kwake sidhani kuna sababu ya kulalamika. Je ukija nyumbani kwangu nikikwambia vua viatu hapo mlangoni kabla hujaingia si wajibu wako kuamua kuvua uingie au kama hutaki si wajibu wako pia kugeuza na kuondoka. Wao wanataka a bank statement, hukutaka kutoa au hukui prepare before or you were not aware of it then you have no right to complain. Ndio maana wamekwambia TRT NEXT TIME...that time utakua unajua yanayotakiwa.
Kuwa sponsored na Govt sio sababu ya kuwahakikishia wao kuwa utarudi nyumbani baada ya mambo yako. Walikua maybe wanataka tu kuona bongo unasave vipi for your future. Na wala hawakusema hiyo bank statement iwe na shilling ngapi huko.....just a bank....u see ....easy....
Pole sana lakini ndio kujifunza 1st watu hawanunui tickets kabla ya kupata VISA na 2nd hizo E-tickets sometimes ni bomu...the cheapest the bomuest......Non refundable....mhhhhhh patamu hapo......
Usitoe mifano ya Visa ya USA na hapa UK na hizo nchi zingine kamwe. hawa wanajua kabla hata ya wewe kuingia ubalozini kama watu wanataka kuzamia nchi zao so hata kama una green card kama ujatimiza requirements unamwagwa. wanachojaribu kupunguza ni nyie mnaokuja huku na kuanza kusema uhongo oh tuna vita sijui bla bla nyingiii. Sasa wewe atii pass ya EU ndio wealthy au? si unapiga box kama kawaida kwani ni issue hiyo acha ujinga alafu unasound kama mpemba weye atii aziishimiwi ndio kiswahii gani. Vijana walienda ubalozi wa marekani miaka hiyo walikuwa wanataka kujifanya wamarekani wakati hata nje ya nchi hawajawahi kutoka wasijue watu ubalozini akipiga interview na wewe tu anajui huyu mkweli au hamna kitu. kuna vitu vingi hata unapofanyiwa interview.Google interview skills...utapata tips. jitayarishe kila kona incase akigusa doc. hii unayo etc etc
ReplyDeleteHuyo anayesema ukiwa na kila documet unaruhusiwa kwenda popote hajui anachosema. Watu wengi wana document zote na wanakataliwa kila siku.
ReplyDeleteNa mimi ni mfano hai wa kuingia USA bila Bank Statement kwa hiyo sometime hata hizo document ni ya kujua nini hasa ni malengo yako au utaishije huko unakokwenda.....niliingia bila bank statement kwenda shule ambayo wala sikuwa na scholarship yeyote wakati ninaaply Visa. Kila nikimwambia mtu hivyo hawaamini...But yeah nilikua na document zote lakini I was naive...or I didn't have .... who knows lakini ..waliniuliza wazazi wako wanafanya nini nikawaeleza. Watawezaje kukulipia shule na kuishi huko. Nikawaambia all I know ni kuwa tuna tuition fees na hela za kutafuta mahali pa kuishi za semester ya kwanza ..na hizo nyingine I have no clue...Mungu atatupa jibu...Lakini wazazi wangu wamesema watafanya kila njia ili nisome kwa vile mimi ndio wakwanza kufika form VI katika familia yetu na kufaulu vizuri.....na aliyenitafutia hizi shule ni rafiki yangu yuko huko anasoma na aliapply vyuo vitatu na vyote wamenikubalia ila nikubali kwenda the cheapest one. ....Wakaniuliza jina la huyo rafiki yangu na yeye alikua naye ni mwanafunzi wakati huo...wakachukua na mabarua ya zile shule nyingine nilizosema nimekubaliwa....That was it...Sijui niliambiwa nini tena ila NILIPATA SHULE BILA Bank statement na niliingina USA bila Bank statement...
Ila miaka yetu ilikua tofauti sio kama sasa
annonymous wa pili aliandika "Balozi zote za Uturuki zina matatizo sana kwani ile nchi ya kiarabu pia ina ubaguzi kidogo" huu ni utumbo balozi zina matatizo kwa sababu ya asili yao? na kwa sababu ya asili yao ndio wabaguzi? nakubaliana na yule alosema kuwa ubaguzi uko kila mahali hata tanzania. na mfano ndio wewe jambo jengine unarukia rangi na asili ya mtu.
ReplyDeletematatizo? umewahi kuomba visa za nchi ngapi?umejaribu france? usa? spain? na kiboko yao china na russia? sasa niambie kama wote hao wanatupa matatizo kwa sababu wao ni waarabu!
Pia yule alosema eti ukiwa na documents zote huwezi kukataliwa visa ya nchi yeyote! hivi hata siamini kama mtu aliweza hata kusema hayo, visa si haki ya mtu ni uamuzi wa wenye nchi (balozi) period.
Na yule aloona ajigambe kuwa ana passport ya EU big deal lakini bado ukitaka kwenda kwenye nchi tele duniani ni lazima uombe visa na mfumo ndio ule ule kama wenye passport nyengine ni lazima ufuate masharti yao na upeleke kila walichosema uwe nacho (hii ni hata katika baadhi ya nchi za europe unabidi uombe visa hata kama una EU passport). Naona mwenzetu labda baada ya kuondoka tz na kufika huko uliko ndio basi na unadhani dunia nzima ni tanzania na europe tu.
Nimepata visa mara tatu UK na schengen bila interview bila bank statement naambiwa tu njoo saa...hapo inakuwaje? au utasema...
ReplyDeleteNimeangaalia haraka haraka website za ubalozi kama nchi 20 kutoka sehemu mbali mbali duniani hapa Uingereza. Nikitaka viza, nje ya EU, naweza kuomba kupitia posta bila ya kulipa ada benki kwanza wala kusubiri mstari. Niliposafiri Uturuki kwa likizo na Urusi kwa kikazi, viza yangu niliipata kupitia posta. Sijakanyaga ubalozi wao wala sijaulizwa maswali au interview katika simu.
ReplyDeleteNilipokuja Bongo nililipa dola 50 na kupatiwa viza yangu uwanja wa ndege. Ilinichukua sio zaidi ya dakika 20. Watanzania lazima waombe viza miezi kabla ya safari, wajaze mafomu kibao, malipo kibao, interview na mwisho wasipate hio viza kama Afisa Ubalozi hajaridhika na majibu na makaratasi ya mwombaji.
Wale wadau wanaosema kuwa masharti ni sawa sawa wajaribu basi kuomba viza kupitia posta kama watapata na pasi zao za Bongo.
Umasikini ni sababu muhimu ya kubanwa kupewa viza. Mpaka hapo Tanzania itakapotajirika, ndio viz a itakuwa rahisi kupatikana kwa wananchi wake.
Hii sababu wadau mtaikubali au mtaikataa ni juu yenu, hali halisi ni kwamba sisi wenye pasi za nchi za kitajiri kama EU tutatesa sana ikija mambo ya kuomba viza, iwe kwenda bongo, uturuki, china au nchi nyingine yoyote duniani.
wewe unaesema kuwa una EU passport hebu nielimishe EU passport iko ikoje?
ReplyDeleteMhadhiri ambaye kapatwa na tatizo ubalozi wa uturuki kuhusu visa then analaumu wadada wakenya and anahadithia kapanda precision air na gari gani sijuwi kwa michuzi.
ReplyDeleteSioni tofauti ya hii kesi na ile ya mtu aliyepewa kauli yakujipulizia perfumes na kupakaa lotion yake pale airport.
Zote hizi zinaonesha jinsi watu wanavyopenda usanii mbele ya sheria na taratibu. Badala yakupeleka vielelezo vyakutosha or kuprove ndani yabarua zako kwamba unaweza kuishi huko na unasababu unalialia tuuuu.
Sasa unataka tukuambie nini? tukusaidie nini kwauzembe wako? eti unasema niliongea nao nikawaambia kwamba kila kitu kitalipiwa na chuo???? mami anapenda longolongo? next time peleka documents ambazo zinajitosheleza bila kukenua midomo kaya yako.
By the way nyie kama alivyosema mtu mmoja hapo juu, open university mumeshindwa hata kuwapanctual katika kazi zenu nashangaa leo unalia kilio kikuuubwa... sikuiti pumbavu kwani wadau hawapendi but natamani kufanya hivyo.
G7
UK
Oyaa,next time chukua viza ya Syria ,utagongewa viza ya Uturuki hapo Syria ipo ghetto bila hata kwenda Alepo ubalozi wa wabata (uturuki).lipo viza kanyenye hapo ghetto nyoo na dolla 20 tu,kazi kwako uturuki kuna Bankasi na Bankunya.
ReplyDeleteNdugu anoni unayetaka kujua kuhusu pasi ya EU. Kwa kifupi sana, pasi yoyote ya wanachama wa European Union, ni pasi ya EU. Kwa mfano, pasi ya Uingereza, Ujerumani, Sweden na kadhalika. Kuna wanachama zaidi ya 20 na wanaweza kuishi na kufanyakazi katika jumuia yao bila ya viza. Baadhi ya wanachama wanatumia Euro kama pesa yao, kuna wengine kama Uingereza bado inagoma na Poland haijaruhusiwa bado.
ReplyDeleteKwa taarifa zaidi jitahidi ku-google "European Union".
Nategemea nimekupa elimu kidogo kama ulivyoomba hapo juu.
Kilichonikuta ctakisahau, kwani niliwapigia simu wahusika wa viza nikiwa tanzania yet, na wakanambia nahitajika inperson ndiyo maana nikaenda, otherwise ningeweza kutumia DHL kutuma documents zangu, infact ni mara ya kwanza kwenda uturuki, I was amazed kwani kwa nchi nyingine huwa napiga simu, then they get us all instructions and procedures afu tunafanya malipo na tuanpata the same day.
ReplyDeleteKinachoshangaza ni kuwa, we are training people to work according to the environment/situations na siyo kukariri kazi, moreover, nilitegemea wangenidirect kwa visa officer ambaye angenipa more details and explanations.
Pia, kilichoniuma zaidi ni ile hali ye EA Community, which nilidhani tungeheshimiana na kujaliana, mtu anatoka Dar hadi Naii then anakuwa attended like that, its even against human rites, au ndo kanunu na sheria za kuattend watu!?
Tujifunze sana, sisi wabongo tumekuwa very keen katika kuwapa wakenya and other members wa EA comunity services.
Nnachotaka ni tufanye kazi as per situations and know tuko na njia ndefu towards EA Federation.
Thanks for your comments pple.
Unachotakiwa kujua nikwamba kuna watanzania kibao wamepata visa na wameenda uturuki kupitia Nirobi bila tatizo. wewe kwakuwa umezowea kudesa, kukariri ndio maana umedhani kila balozi inatumia njia moja tu.
ReplyDeleteAfter all open university mumepoteza matokeo ya wanafunzi wenu mara nyingi sana. Je kama munawatrain watu wafanye kazi bora mbona wenyewe hamufanyi vizuri?? Integrity ya kazi yenu hamna kabisa, munauza papers... so munalaumu nini hapa?
eti mimi mhadhiri!! wenzio tunapita same embassy wewe mhadhili unashindwa: kukariri definitions huko.
G7
On my way home..
Mhadhiri pole nimesoma comments za wote sikuona hata mmoja aliyekuelewa unataka kutuambia kitu gani.Nina wasiwasi wote waliotoa comments waliowengi ni wale waliozamia nchi za ulaya kwa kukimbia njaa na uchumi tata.Mtu aliye na busara kuanzaia Desk officer wa Uturuki ningetarajia wangekueleza kwa kirefu kwa nini utakiwe bank statement wakati wewe huendi kusoma huko wala huna mpango wa kuishi huko,ningeelewa kama wangekuuliza una kiasi gani cha pesa za kujikimu kwa mfano Travelers cheques or $au pound ngapi nataka kuungana na msemaji aliyesema kuwa uturuki ni nchi ya jamaa waliosoma madrasaa hivyo siajabu kuelewa kwao kukawa kama wenzetu ambao tunaona mabo wanavyoyashughulikia.
ReplyDelete