Kwa "walevi wa picha" kama sisi, kuona ka-taswira ka kuvutia namna hii usikanase inakuwa kama dhambi. Mwaga critics tuzoe maujuzi zaidi Kaka katika hizi taswira mbalimbali zikabilianazo na jua.
Blessings
Mdau
-------------------------------------------------
asante mdau kwa taswira mwanana za jua kuzama. kabla sijasema jambo naomba uelewe kwamba katika fani hii ya picha kuna kitu kama mtu kupenda uzuri fulani, hivyo kwako inaweza ikawa mbaya kwangu ikawa nzuri. yaani beauty lies in the eye of the beholder. hivyo hakuna jawabu kamili kwenye ubaya ama uzuri wa picha kama ilivyo katika hisabati. hayo ni maoni yangu mimi na sintokasirika kama nitapingwa, kwani hii sio hisabati. ni picha.
taswira 1. ni nzuri ila ungewahi kidogo kajua kakabakia kwenye pachu za huo mfereji ama mdomoni pa huto tukuta tuwili ingekuwa ya kuvutia na kustaajabisha mno.
taswira 2. picha imekufa kwa sababu jua limekula uonekano wa mnara, na pia umelifuata jua na kula upande wa shoto wa mnara na kuunyima haki yake ya kuonekana. hapo ungeuacha mnara wote kama taswira 1. ili kieleweke maana hapo haijulikani unataka kuonesha nini. pia ungefanya utundu kama ule wa taswira 1. ingefaa zaidi katika hiyo
taswira 3. hamna kitu hapa. unataka kuonesha nini?
taswira 4. hii ni bonge la picha na kukosekana kwa 'shake' inaoesha ulitumia tripod ama kamera iliwekwa sehemu muafaka ama mkono wako uko imara. kwa kuongezea utamu na kama kamera yako inarihusu manual operations ungeweka slow shutter speed ili taa za gari zipitazo zisiwe dhahiri. yaani zionekane kama mistari inayofukuza na kufukuzwa na gari.
vinginevyo ni jaribio zuri na kwa kuomba kukosolewa inaonesha ni jinsi gani uko makini kwenye fani. ushauri wangu endapo kama utataka kupata picha nzuri zaidi jaribu kufanya utafiti siku moja kabla kuona mwelekeo wa mwanga na muda. pia inabidi uje ukiwa na uelewa kwamba mtazamaji wako ama wewe mwenyewe unataka nini. pia acha uvivu. zunguka subject na jaribu kila mpigo na vipimo (bracketting) ili katika picha tano ama kumi moja ama mbili ziwe bora.
nakutakia 'ulevi' mwema wa picha na hongera kwa kutufungulia mjadala huu
-michuzi
Kaka Michuzi naona unatoa Tuition ya Bure/dezo....
ReplyDeletemichu hiyo ya kwanza kama angetumia filter ndhani ingekuwa bomba zaidi. ingeonekana ni jioni. au kabla ya kuituma angeenda kwenye photo shop akaifanya ionekane ni alfajiri au machewo.inategemea na messege anayotaka kuiwakilisha kwa watazamaji.najua ma dinosour wa picha kama wewe huwa hampendi mambo ya digital.manake ushauri ulompa jamaa umetumia basic za kikongwe. but its iteresting .mlevi wa camera
ReplyDeletemichuzi naomba unisaidie. huwa naamini picha yoote nzuri especially za harusi lazima ziwe black n white.je mimi ni kichaaa au kuna sababu za kitaalam?nimefanya jaribio nilioa mwaka 03 nikawa na copy mbili za picha zangu jana nimeangalia hizo picha cha kushangaza zile za b n w ziko bomba saana ila za rangi nimeona ka zimefubaa. je niko right au ni imani yangu ya picha inanipotosha??au ni kweli mie ni kichaa??? kichaa wa picha
ReplyDeleteHiyo picha ya chini kabisa ni makutano ya M street na 24 street northwest- washington, dc (my home town)
ReplyDeleteWow! ndio maana naamkiaga hii blog kila asubuhi. Leo ni bonge la lecture. Manake mimi ni mpenzi wa picha na ninaspend so much money kwenye camera na digital image softwares lakini sina darasa katika mambo haya. Na picha ninazopenda kuzhukua ni za nature na wanyama.
ReplyDeleteUkweli haya yote nilikua siyajui ila mimi sio mvivu huwa nachukua picha kama kumi ili nipate the best one to keep.
Asante kwa darasa lako.
Ujuzi wa kupiga picha hauhitaji photoshop. Nakubaliana na michuzi na picha ya chini kabisa. Ila nafikiri mpigaji hakutumia tripod, ungepunguza shutter speed yako kidogo na labda ongeza ISO ungepata taswira nzuri.
ReplyDeleteMdau wa digital photography!
Bro Michuzi anzisha mashindano ya kupata picha bora ya wiki au mwezi. Kama sehemu nyingize ughaibuni wanavyofanya. Pia kutokana na haya mashindano watu watajifunza jinsi ya kupata snap nzuri. Pia ni burudani ya aina yake.
ReplyDeleteHeshima kwako Kaka.
ReplyDeleteNia ilikuwa kupata critics zako kwa hili na nashukuru kuwa wengi wamejifunza na wengi wameelezea waliyoona kulingana na utaalamu wao. Ni chachandu njema na nashukuru kuwa kila niombapo critics huwa unaniwezesha kupata zilizo njema zaidi muda unaofuata.
Heshima kwako na kwa wadau wote wenye "ulevi wa picha"
Mzee wa Changamoto
Taswira 4=101%.
ReplyDelete