Home
Unlabelled
kausafiri ka azam fc
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Wadau haya ndio mambo ambayo wapenda sipoti tulikuwa tunasubiri, Hawa azam wataendesha timu yao kama za wenzetu kule. Utashangaa kaseja kahamia Azam kwa milioni 50. Mambo biashara tu.
ReplyDeleteBalozi,
ReplyDeletehii ya Bakhressa kumiliki timu nimeipenda, na zaidi ya hapo kuipa timu nyenzo muhimu za kazi. Huu ni mfano wa kuigwa.
Mimi ningemshauri hata Yusuph Manji nae achukue timu yake binafsi aachane na Yanga ambao kila kukicha ni migogoro.
kwa kuongezea tu, wasiishie hapo kununua basi. wawe na ofisi ya kueleweka na uwanja wao wa mazoezi na vifaa vyote muhimu na vya kisasa vya mazoezi. kwa style hii Maximo hatakuwa anaumiza kichwa kupata vijana ktk kikosi chake.
Simba na yanga majungu mengi, mpira kidogo. zimebakia kuwa sehemu ya historia.
Michuzi, katika pita pita yangu nikakutana na hii: http://www.azamfc.com/ inaelekea jamaaa anajua anachokifanya, ushauri wangu ni kuwa hawa jamaa wenye pesa inabidi kabla hawajawekeza waangalie masuala ya Domain.. mimi simlaumu huyu jamaa, kwani inaekekea anajua anachokifanya!
ReplyDeletehttp://www.azamfc.com/ Ni jina kubwa kisoka na kibiashara katika Tanzania. ni vizuri wakaliainisha na Club yenyewe.
Watanzania tuamke....
Very good.Barabara kwa sasa siyo mbaya sana nchini.Wataweza kufika Bukoba kucheza na Kagera sugar ndani ya siku moja na kuzunguka,chato,geita sengerema, mwanza kucheza na toto bila matatizo.Go go boys
ReplyDeletenimekubali babake kametulia kweli
ReplyDeleteNembo yao ni nzuri sana..imetulia na ina akili: inaonyesha timu na kampuni! ni kazi nzuri iliyofanywa kwa ubunifu!!! basi lao zuri na ni la kwanza la aina yake kutumiwa na timu ya mpira hapa bongo!! congratulations SS...Sifa nyingine zinakwenda kwa mpiga picha!! that is a good shot safi sana mkuu na hongera kwa kazi nzuri!! pia nawapongeza wachezaji na viongozi wote wa AZAM kwa kazi nzuri wanayoionyesha uwanjani
ReplyDeleteHii ni lugha gani jamani? asili yake wapi?
ReplyDeleteHaya ndio maendeleo tunayoyataka katika soka letu bongo. Cahkushangaza timu za Simba na Yanga hadi hii leo haziwezi hata kumiliki basi. Hivi hao viongozi walishakaa wakapiga mahesabu gharama za usafiri zinawacost kiasi gani kwa mwaka? Ni bora wakanunua mabasi yao wenyewe. Hongera timu hizi ndogo na hii inaonyesha wazi kuwa umiri wa mtu binafsi au kampuni ni bora kuliko timu za wanachama kazi kukaa milangoni kuiba fedha. Hongera Azam tunasubiri website na nyie muwe kama Mtibwa Sugar. Simba ziii Yanga ziiii!!
ReplyDeleteAnony wa September 16, 2008 7:07 PM, wewe ni majungu type, hebu jiulize kwanza hicho kiswahili unachozungumza kilikujaje kuwa kiswahili.
ReplyDeleteTatizo ni kwamba na yeye "Bakhresa" si tu mpenzi bali ni miongoni mwa friends of simba ninachoona mimi hiyo timu kitaikuta kinachoikuta mtibwa , kilichoikuta Moro United baadae Kajumulo baadae tena Moro united kwa kifupi kupata maendeleo kisoka itakuwa shughuli, natuiombee
ReplyDeletewewe wa september 17, 2008 1:24 una akili finyu kweli! eti ni majungu type na kiswahili ninachozungumza kilikujaje? jawabu sijui lakini alichooandika mwanzilishi wa topic hii ni lugha ya utumbo mtupu! wakati watu wanatukuza na kukipeleka mbele kiswahili nyinyi mnakirudisha nyuma miaka elfu. watu wanajenga nyinyi mnabomoa! eti mnaona ndio maendeleo kila kitu kuanza na "ka" amkeni!!!!
ReplyDeleteHawa wadau wa Yanga nini? Yaani mnaleta migogoro na hapa pia??? lol
ReplyDeleteacheni kufananisha maziwa na tui la nazi hapo?
===
Buffalo,
New York
Mnamwonea mtoa kichwa cha habari.Huu msemo wa kutumia 'ka'(kutokana na madhara ya lugha za kienyeji) upo sana kwenye makabila hasa ya kanda ya ziwa(Mwz,Shy) nimesikia sana kule.Nina uhakika aliyepost,ameandika hivyo makusdi kabisaaa akifahamu siyo kiswahili sanifu(kutoa burudani!).Ni kama vile barabara ya Mandela road.Sisi wanablog tunaelewa.Hapa siyo BAKITA hii ni blog.Soma tahariri ya daily news ya tar 16,watoto(Manyara) walimwimbia rais(J.Kikwete) nyimbo za kifaransa na kizungu,rais kuwauliza kwa nini hawakuimba kiswahili wakamjibu 'we do not know swahili!!!
ReplyDeleteBasi Kali Kinoma. Changamoto Hiyo kwa Wadau wengine Wa Soka Bongo.
ReplyDelete