

Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
tupatieni msimamo wa ligi basi angalau.
ReplyDeletehizo picha za akina Karume, nyerere Kikwete zinafanya nini kwenye viwanja vya michezo.Tz kila kitu ni siasa.
ReplyDeleteYaani inaboa kweli.
Mheshimiwa Mkuu wa Tegeta,
ReplyDeleteKama kuna kitu kinanishangaza kuhusu suala la kipa Mserbia ni kuwa watu wanashangilia uzungu wake. Kuna watu ambao yawezekana wanataka tuamini kuwa golikipa huyu (kama ni mzuri hivyo langoni) basi inatokana na kuwa yeye ni Mzungu.
Ni kama watu wanaotukuza "nzi wa kizungu, ng'ombe wa kizungu, nyumba ya kizungu, mitaa ya uzunguni n.k". Tunashindwa kuelewa kuwa mafanikio ya mtu au jamii yoyote yanatokana na mtu au jamii hiyo kulipa gharama ya maendeleo yake na kufanya kila wawezacho kufanikiwa.
Wazungu wana damu nyekundu kama sisi na wao wakifa miili yao huoza na kuliwa na funza.
Tunapotoa pongezi kwa golikipa huyu Mserbia tujue kuwa yawezekana amekuwa akidaka tangu "chandimu" ya kwao, na amepitia mazoezi mbalimbali kiasi cha kujiamini kuweza kulinda lango lao. Miaka ile ya Umiseta nilihamia kwenye shule moja ya sekondari iliyokuwa haifanyi ziru kwenye soka. Mwaka nilioingia mimi tukaweza kwenda hadi mashindano ya kanda, na nilichokifanya nilikuwa ndio golikipa wa timu. Tulipocheza na timu ya Singe (Babati), nilifuta penati ambayo ingeweza kuwapa ushindi Singe. Kitendo hicho kilijenga confidence kwa timu yangu na tuliweza hadi kutoa karibu wachezaji wanne kuunda timu ya mkoa baada ya sifa za "nyanda" kueneza.
Lakini hilo halitokani na mimi kuwa mtu wa kabila lolote au vinginevyo. Inatokana na mazoezi, kujituma na kutokubali kushindwa. Ni ile competitive spirit. Tukitambua mambo hayo tutagundua kuwa hatuhitaji Rais Mzungu ili tuweze kulinda mali zetu, hatuhitaji Waziri toka Japani ili tuweze kusimamia raslimali zetu.
Ni lazima tuanze kujiamini sisi wenyewe na kufanya vitu kwa kujituma zaidi, kuthubutu zaidi na kwa hakika kutoogopa kufanya makosa. Huyo golikipa nakuhakikishia hata akifungwa goli moja hatobabaika kwani ni sehemu ya mchezo.
Tatizo litakuja siku atakapofunga mabao bila, utaona ule Uzungu wake si kitu tena!!!!
we mwanakijiji hapa watu wanatoa comments siyo uchambuzi.
ReplyDeleteNakubaliana na Mdau Mwanakijiji, Huyo kipa mserbia anataka kuongeza CV yake, mawazo yake ni kama ya Shaabani Nonda(Blackburn Rovers). Kuwa kuchezea Yanga au Simba siyo ndiyo ametimiza ndoto yake.
ReplyDeleteNdoto za huyu mserbia na kama ilivyokuwa kwa Shaabani Nonda ni kujituma kucheza vizuri ili siku zijazo aweze kujiunga na timu bora zaidi duniani kimpira na kimaslahi.
Mfano halisi ManUTD, Arsenal na Chelsea, mameneja na wachezaji wa timu hizo mawazo yao ni kuyakua kombe la premier league na makombe ya UEFA, Championship na supercups. mfano Liverpool ilipocheza juzi na Stoke City, au Chelsea na ManCity, Arsenal na Fulham au ManUtd na Wigan, mawazo yao ni kuchukua Premier Cup,UEFA& Champion Cup na SuperCup
Mawazo ya mameneja, wachezaji, mashabiki na 'kamati za ufundi' za Yanga na Simba ni kushindana wenyewe ndani ya mipaka ya Tanzania tu, hakuna anayewaza kuzifunga timu za Cameroun, Tunisia , Egypt na kuchukua kombe la CAF n.k
Mpaka mitizamo na mikakati yetu itapobadilika tutakuwa tunawaza kuishia kunyakua kombe la ligi Kuu Tanzania bara kama kipimo cha mafanikio ya klabu,wachezaji, kamati za ufundi na furaha isiyo kifani kwa mashabiki wa timu hizi kongwe za Tanzania.
Mdau
Rocky
London.
Acha hasira we mwanakijiji ili wajingawajinga watembelee zaidi hi globu ni lazima pumba ziwe nyingi. we unafikiri ukiweka mambo ya maana humu watu siwapungua sana. ukitaka busara soma website zenye akili.humu ni ndio mambo yake hayo..libeneke, mzungu, picha za kulisha watoto yatima...! wakati wanajitangaza kibiashara.....Ila michizi we sijui Islamu gani, unatumia mayatima kujipatia kipato, unawezaje kuweka picha ya yatima kutangaza biashara...haya baba ramadhani hii inshalah...
ReplyDeleteDuh afadhali kandmbili wamepata wa kumsakizia kukaa golini siku na simba,huyu akifungwa tunaweza kujiliwaza kua hajazoea simba na yanga,lakini kaseja na mapunda mhh
ReplyDeleteNgojea hii topic kuhusu picha za maraisi wapya na wazamani, naweza kutetea sababu huo uwanja wa taifa na pia nikiwanja cha serikali, Sema sikubaliani na uwanja kama Amani zanzibar au Arusha au uwanja mpya wa dar-es-salaam kuwa na picha za ma raisi haiwahusu, tuweke picha za michezo kama filbert bayi au wachezaji wa zamani, Jamaa iliotowa topic kuhusu hizo pic nimekubaliana naye sio siri haipendezi tunarudi kwenye hii ya kipa mzungu sijui chotara asubiri apigwe na simba basi yanga wataanza kumuweka juma kaseja bao sababu mweusi hahaah sorry nimefanya ubaguzi kipa wenu mzungu sijui chotara.
ReplyDeleteTanzania tunaonesha kama hatuweki ubaguzi tunatizama kipaji tuanze kuwaweka na Wahindi wa kitanzania sasa kwenye mpira, huyu jamaa aliyesema kadaka penalt mpira wa ndani alikuwa hajui siunajuwa zamani kama hujui mpira unaambiwa kaa kipa hahahaa. sorry ni jokes tu Simba soon tutaleta Striker wa kibagachori kama Chopra wa Sunderland. kuna jamaa mmoja katika wa dosi wamepiga mpira hakuna kama yule alikuwa PSG na AC MIlan anaitwa dhorasso au nimekosea jina kama nimekosea naomba mtu anitajie yule jama alipiga midlfield ya nguvu ufaransa hawabagui wachezaji.
Duh...Isega Isindani 'Mwana Mbeya'mwenzagu kakumbukwa!!!
ReplyDeletekaka michuzi mimi nina kaswali kamoja kadogo kenye vipengele kama vitatu hivi kukusu huyu kipa mzungu wa yanga, ninafahamu fika kwamba wewe sio muhusika na huwezi kunijibu maswali yangu kiufasaha, ila unaweza kuwa na ufahamu kiasi fulani,swali lenyewe ni hili!
ReplyDelete(a)ameletwa yanga moja kwa moja kutoka sebia kwa ajili ya kuichezea au ana ishu zake hapo bongo na kwa kuwa ni golikipa akaamua kuliunga juu kwa juu?
(b)kama ameletwa moja kwa moja kutoka huko sebia je mikataba yake ikoje? nikimaanisha analipwa kiasi gani? anakaa wapi? usafiri na mambo mengine kama hayo
(c)kama ni kweli kwamba ametolewa moja kwa moja sebia, je ni nani aliyemuona huko sebia na akaleta habari kwamba huna kipa huko, na jee huko sebia alikuwa anachezea timu gani? maana lazima tufahamu hizo imfo zote, sio tunapelekwa pelekwa tu eti kwa kuwa ni mzungu,hata timu kubwa hutangaza imfo za wachezaji hata kabla ya kuwachukia ili watu wafahamu ametokea wapi na ana sifa zipi, asije akawa shemeji yake na manji halafu si tunaambiwa ni mchezaji wa kulipwa!
Kichwa cha habari kinataka kuleta Tafrani humu.kimekaa 'kiubaguzi'?Sidhani.Mimi binafsi sioni hatari huyu kipa huyu kudakia Yanga kama ana viwango vinavyohitajika kwa Yanga.Kwani hamjaona makipa weusi wakidakia timu za wazungu?Golikipa wa Marseille na Ufaransa Steve Mandanda mbona hamsemi?Nani asiyemkumbuka golikipa mmoja maarufu Uingereza&Trinidad/Tobago Shaka Hislop West: Ham,Portsmouth,N/castle,reading?ebu tuacheni comments zinazolenga Ubaguzi jamani.
ReplyDeleteNI MIMI PETER NALITOLELA NIMEIBUKA UPYA NDANI YA BULOGO YA JAMII KUTOKEA MBAGALA. MIMI NAONA HUYU KIPA SISI WABONGO TUNAOGOPA KUPIGA PEMBENI MIPIRA KWA SABABU NI MZUNGU TU.INABIDI TUACHANE NA TABIA ZA KIZAMANI HUYU KIPA NI RANGI TU KWANZA ANAUZA SURA SIDHANI NI MZURI KAMA HAMISI KINYE WALA MUHAMED MWAMEJA? WADAU WOTE MIMI NAWA LOVE SANA NINGEPENDA VIJANA WANGU WA MUZUMBE TUWE TUNAWASILIANA KUPITIA HII BULOGU YA KAKA YETU MICHUZI.NAWAPENDA WOTE HASA HASA MICHUZI NAVIPENDA VITOP VYAKE FULANAZZZZZ NA TABASUMU MOTO MOTO..! EX MUZUMBE P. NALITOLELA
ReplyDeleteMpeni dual citizenship huyo !
ReplyDeleteWote tunajua kipa wetu shati ,atatusaidia timu ya taifa
Kaima
Mwana Kijiji,
ReplyDeleteMaoni mazuri. Wazungu ni watu tu kama sisi. Tena mimi shuleni wengi tu nilikuwa nawapita. Wengine walikuwa wakitusafishia vyoo, kutupikia, kutandika vitanda nk nk. Si kwamba nataka kujisifu ila huo ndiyo ukweli wenyewe. Tuache kuona watu weupe kama ni kitu cha ajabu. Mwisho ni kuwa kwako wee Michuzi, kama mwandishi wa HABARI, kutumia neno MZUNGU ni dhambi. Wazungu wanaojua Kiswahili huwa wanajiona kama "Kwenye Basi kuna ABIRIA 49 na MMAKONDE mmoja..." Sasa swali kwani Mzungu si MTU??? Tuanze kubadilika. Mdau wako Sikonge.
ZIPO HABARI ZA UZUSHI ZINAZOSEMA KUWA UWANJA HUU UMECHUKULIWA NA CCM NDIYO SABABU YA KUBANDIKWA HIZO PICHA NA UTAITWA UWANJA WA CCM TEMEKE! watanzania tuamke tudai viwanja vyote ccm ilivyopora toka kwa wananchi. PIA VYAMA VYA MICHEZO VYA TAIFA VIACHE KUTUMIA VIWANJA AMBAVYOCCM ILIPORA, NI HARAMU TFF KUILIPA CCM KWA VIWANJA AMBAVYO HAIKUVIJENGA.
ReplyDelete