KWA NIABA YA FAMILIA YA MR RAPHAEL DAMAS WA NYEGEZI KALIFONIA MWANZA, TUNAPENDA KUMKUMBUKA MPENDWA WETU REBECA R DAMAS TOKA AIAGE DUNIA MWEZI HUU AMETIMIZA MIAKA KUMI.
REBECA MPENZI UCHESHI WAKO NA UKARIMU WAKO UMEBAKI KUWA KUMBUKUMBU KUBWA SANA KWETU JAPOKUWA SIKU ULIPOTUTOKA ILIKUWA SIKU YA MAJONZI MAKUBWA SANA KWETU.
KWASABABU KIFO CHAKO KILIKUWA CHA GHAFLA, JIONI YA TAREHE MOJA SEPTEMBER 1998 TULIPOLETEWA HABARI KUWA GARI MLILOPANDA LIMEPATA AJALI NA WEWE NA RAFIKI ZAKO MMEPOTEZA MAISHA HAPO HAPO MLIPOKUWA MKITOKA MPIRANI KUELEKEA NYUMBANI .
NI PENGO LISILOZIBIKA LAKINI KAZI YA BWANA HAINA MAKOSA BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
TUNAMSHUKURU MUNGU KWAKUTUPA UJASIRI NA UVUMILIVU TOKA UTUTOKE FAMILIA YOTE NDUGU.
NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI TUNAMUOMBA MUNGU AWAWEKE MAHALA PEMA PEPONI PAMOJA RAFIKI ZAKO NA WATU WOTE WALIOKWISHA TUTANGULIA MBELE ZA HAKI
AMINA
DADA YAKO MPENDWA
DEVOTA R DAMAS

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. POleni kwa kipindi hiki kigumu Mungu awazidishie wana familia na kumpa marehemu pumziko la milele. kwa kweli hamna jambo linaloweza e;ezea uchungu wa kifo lakini pamoja na yote ni kumshukuru Mungu kwani yeye ananguvu ya kutufariji na kutupa nguvu mpya. Mungu awabariki wote na awaangazie neema yake katika mfanyalo bila mwenzi wenu.

    ReplyDelete
  2. Devota dear so sorry for your loss, Mungu awape uvumilivu!
    RIP REBECA kipenzi!

    ReplyDelete
  3. Poeni sana familia ya Rebeck Damas. Mimi binafsi niliumia sana siku niliposikia kwamba Rebecka Damas amefariki dunia. Na leo tena nilipoona picha yake nililengwalengwa na machozi. Rebecka alikuwa classmate wangu pale Pamba Secondary School Mwanza na desk lake lilikuwa mbele ya desk langu mwaka 1996 tukiwa form three (3) Rebecka alikuwa rafiki yangu na rafiki wa kila mtu pale darasani. Alikuwa mcheshi, mtulivu na mwenye mapenzi na watu wote. Nimeguswa sana baada ya kuona picha yake tena baada ya miaka 10.

    Rest in peace Rebeck.

    Samson.

    ReplyDelete
  4. Lovely girl! Mungu hakika amemlaza pema.
    I am sure she led a lovely life to the fullest.
    I am so happy that she has remained in your souls. This is how we should live and die.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...