Ras Nas akiwa na prizenta wa BBC Laura Hubber

Msanii mkongwe wa muziki wa reggae na muziki wa dansi, Ras Nas au Nasibu Mwanukuzi, amefanya mahojiano na BBC prizenta Laura Hubber wa kipindi maarufu cha 'The Beat'.

Mahojiano hayo ambayo yanahusu albamu mpya ya Ras Nas, Dar-es-Salaam, yalifanyika 2 Septemba jijini Oslo, Norway na yatarushwa wiki mbili zijazo.

Wadau kaeni chonjo, wabongo twakubalika!

Kipindi hicho cha BBC husikilizwa na mamilioni ya watu. Vigogo wengi wa muziki hapa duniani wamepitia pale kwanza kabla ya kulipuka.

Zaidi ya kufanya kazi ya BBC Laura Hubber vile vile ni prodyuza mmojawapo wa 'American Next Top Model'.

Siku na taimu ya kipindi tutawajulisheni.

Asanteni

KonPro – Kongoi Productions
And
Hassan Nganzo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Jamani niondoeni tongotongo,kuna jambo lantatiza mwenzenu, hivi ukiwa Ras au JAh, ni lazima uache madevu bila hata kuyapitisha chanuo?
    Naomba msaada na waosah vinywa osheni kwa kunielewesha.
    Naomba kuwasilisha.

    Q

    ReplyDelete
  2. Weye Q vipi. Unaogopa madevu au? Jamaa kayaachia kama anavyotaka. Labda viwembe bei mbaya au ndio staili ya kivyake vyake hiyo. Mwachie huyo jamaa na madevu yake!

    ReplyDelete
  3. JAMAA BAYA KAMA DUDU-MTU

    ReplyDelete
  4. It's very easy even a cave man can do it.

    ReplyDelete
  5. Anoy wa 6:19 PM tuletee picha yako tuiangalie basi, mbona unajificha. Unaona haya?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...