Pole na kazi kaka Michuzi
Mi ninaitwa Mwampona ni mdau Muziki hapa kigoma hivyo nikaona si vyema nikikaa kimya bila kuwafahamisha wa Tz wanzangu kwamba Kigoma tuna mambo mazuri katika swala zima la Burudani.
Mi ninaitwa Mwampona ni mdau Muziki hapa kigoma hivyo nikaona si vyema nikikaa kimya bila kuwafahamisha wa Tz wanzangu kwamba Kigoma tuna mambo mazuri katika swala zima la Burudani.
Tunayo Band inayojulikana kama Hitman Redemption Band yani {HRB} kazi kubwa ya band hii ni kuelemisha jamii kwa njia nyimbo kuhusu gonjwa hatari la Ukimwi, kuongea na vijana athari za madawa ya kulevya na kuwashauri wamgeukie Muumba wao bila kujari itikadi za Kidini, Na tunafanya kazi bega kwa bega na Serikali yetu ya mkoa katika swala zima la burudani pindi tunapopata wageni wa kitaifa na uhamasishaji mbali mbali.
Hapo ni vijana wakiwa kazini katika sherehe za May Mos 2008 katika viwanja vya Mwanga.Wako katika Ujenzi wa taifa
James Mwampona
James Mwampona
Mwenyekiti (HRB)
Mr. Mwampona nasikia Kigoma kuna uwanja wenye kuingiza watu 60,000. hivi ni kweli? Naomba ututumie picha ya Uwanja Wa Lake Tanganyika. Ahsante!
ReplyDeleteDoh!Kigoma kuna bendi!!inapigia muziki wake ktk ukumbi gani?au ni hapohapo ktk viwanja vya mchangani mwanga?poa sana.Na ile bendi ya Super Kibisa wamefia wapi?
ReplyDelete