John Tyler Hammons ni kati ya ma-Meya wenye umri mdogo kabisa hapa nchini Marekani na ni kati ya ma-meya wenye umri mdogo wanaohudhuria mkutano unaoendelea kumuidhinisha mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican huko Minnesota.

Akiwa na umri wa miaka 19, Meya Hammons alishinda uchaguzi wa kiti hicho katika mji wa Muskogee, Oklahoma kwa asilimia 70 ya kura dhidi ya meya aliyewahi kushikilia kiti hicho kwa mihula mitatu na anajumuishwa katika kundi la viongozi hao wachanga lijumuishalo Mayor.

Hii yaweza kuwa changamoto kubwa kwa wanasiasa wachanga nyumbani na alama ya mabadiliko kwa wakongwe wasiopenda kung'atuka.

Ni CHANGAMOTO YETU sote kujua mabadiliko tuhitajiyo, watu watakaotuletea na kisha kuwachagua pasina kung'ang'ania kina fulani ambao wamekuwepo miaka nenda rudi bila mabadiliko.

Kwa habari zaidi juu ya John Tyler Hammons click
wiki/John_Tyler_Hammons

na kwa orodha ya ma-meya wenye umri mdogo kupata kushika nafasi hizo nchini marekani bofya
of_the_youngest_mayors_in_the_United_States


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hawa ndivyo walivyo Wa-shingo nyekundu. Kwa nini asijiongezee walao ka-elimu ka digrii ya kwanza kisha akaingia kwenye siasa!!!! Shingo nyekundu wavivu wa kufikiri na wabaguzi wakutupwa!!!!

    ReplyDelete
  2. Now You Tell Me that THAT Guy Does not Have Bright FUTURE..

    ..Kalaghabao!

    ReplyDelete
  3. Wewe acha kukurupuka tu na kusema mambo...huyo kijana ni mdogo na kamsi kenyewe ni kama kasarah palin tu...Na pi huko kwenye mjini kwao ni kuwa sheria yao yeye ni mayor lakini mwenye kufanya mbo yote ni deput something ...yeye hayoko hata kwenye mambo ya badget wala nini na ndio maana waliopita before yeye walikua too old....

    Ni kama nchi iwe na rais lakini prime minister ndio awe na saying zote

    ReplyDelete
  4. The guy runs the city budget, schools district, the police force etc. This shows that ONLY IN AMERICA YOU CAN BE WHO YOU WANNA BE na wala sio bongo.
    Bakini na CCM yenu kwani sisi tunajichukulia uraia wetu kwa maslahi ya wanetu.
    IDUMU BONGO NA CCM YENU MLIOCHOKA NA SISI HUKU TUNAENDELEZA LIBENEKE LA KUWAACHIA WENETU MAISHA YA KWELI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...