CHAMA CHA MAPINDUZI

MKUTANO WA CCM SHINA LA READING

CHAMA CHA MAPINDUZI- CCM READING

WANACHAMA WOTE –CCM READING
WAKEREKETWA WOTE-CCM READING
WAPENZI NA WANAMAPINDUZI WOTE WA READING
TAREHE; 06/09/08 SAA 8 MCHANA HADI SAA 12 JIONI

MAHALI:
UKUMBI 79 LONDON ROAD {KIJIWENI}
READING RG 1 5BY
KADI ZIPO KWA WANACHAMA WAPYA KUMBUKA KUJA NA PICHA BEI YA KADI NI POUND TATU NA POUND KUMI NA MBILI ADA YA MWAKA MZIMA.


KWA MAELEZO ZAIDI TAFADHARI WASILIANA NA;
MAIRA MIGIRE- 07799212095
KATIBU WA SHINA LA READING

WOTE MNAKARIBISHWA – KUTAKUWA NA VINYWAJI, NYAMA CHOMA NA MUZIKI BAADA YA SHUGHULI ZOTE.
KIINGILIO BURE!!!!!!!!


Akhasante.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. du jamaa kweli wana akili sana,wamestukia challenge itatoka kwa wananchi wa nje kwahiyo wanawateka mapema polepole.
    ili mzidi kuwakumbatia kwa mabaya wanayoyafanya.

    ReplyDelete
  2. Tumekuja kutafuta maisha tuondoelee ujinga

    ReplyDelete
  3. Hiyo siyo bendera ya CCM. Angalieni rangi zake. Jamani mbona mnatuaibisha sasa? Kuweni makini vijana.

    ReplyDelete
  4. Kama mnataka chama cha siasa na uongozi, nendeni bongo. Agenda gani ya mkutano mtaweka? Inabidi muwasaidie bongo, misje mkaleta wizi kukusanya michango ya watu. Wapi na wapi? Hatujasikia Democratic au Republican kuwepo Berlin au Labour Party kuwepo DC! Tuondoleeni upuuzi hapa na mavumbi yenu yaliyowajaa.

    ReplyDelete
  5. ccm ccm tumewachoka sisi tumeshajiripua sisi ccm itatusaidia nini kama nyama choma twazilia majumbani kwetu sio uchafu huo mnaouweka huko kama hamna makaratasi yakurudi bongo mtajijua. mtawapata washamba wenzenu,na wasabato au walokole.bora nijiandikishe na labour itanipa kazi au income support kuliko huo upumbavu. mdau reading.

    ReplyDelete
  6. Mimi ni Mwanachama Mwanzilishi na Mkereketwa wa CCM Shina la Reading.Natoa pongezi sana kwa Viongozi wetu wa shina la Reading kwa kuwa hodari na wachapakazi makini waliopania kukieneza chama hata ughaibuni ambako Tanzania haijulikani na mtu.Napendekeza katika Kikao kijacho MOJA YA AJENDA ZA KIKAO tutakayo ijadili iwe ile ya RIPOTI YA UKAGUZI WA MAHESABU YA CHAMA CHA CCM KWA MWAKA 2007!AUDITED ANNUAL ACCOUNTS OF CCM FOR THE YEAR 2007.Nasema hivyo kwasababu hapa Reading tumepania kwelikweli kutunisha Mfuko wa Chama ili ukasaidie upanuzi wa chama huko nyumbani na katika matawi mengine huku ughaibuni.Ni vyema wanachama wakapewa taarifa hizo ili wawe na imani kuhusu usalama wa pesa na michango yao.Ajenda nyingine napendekeza ijadiliwe iwe kuhusu Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Jinsi Wanavyochaguliwa.Maana baadhi yetu tuna malengo ya mbali.Hatuingii katika chama hivi hivi burebure tu.Tuna Malengo.Ajenda zingine nawaachia wenzangu watapendekeza.Nia ni kukijenga chama huku ughaibuni.Nyumbani hata kikiwa dhaifu nguvu ya ziada itatoka huku nje.nawasilisha.nitafurahi kupata mwongozo kuhusu hilo kabla ya siku ya kikao ili niweze kuwahamasisha wenzangu wengi zaidi waje kikaoni ingawa ni wabishi sana.Labda taarifa yako itasaidia Mkuu!CCM Damudamu,2010 oyee!

    ReplyDelete
  7. hivi nyie bado mpo na ccm tu? acheni ushamba na kujipendekeza hizi ni zama za mabadiliko hatukumbatii mafisadi tena [ ccm ]

    ReplyDelete
  8. hiyo bendera si ya ccm.

    ReplyDelete
  9. wewe unaewasema wasabato na walokole wamekukosea nini? kama htaki ccm ishia tu hapo sio kuongelea na madhehebu kama huna dini ni wewe.

    ReplyDelete
  10. Kuna umasikini wa kila aina, ila pale unapokuwa masikini ukatumia hela yako mfukoni ikaisha, ukokopa mpaka watu wa kujikopesha wakaisha; kinachofuata unatumia akili yote mwishowe unabaki mbumbu.
    Basi hicho ndo kinaendelea na hawa wenzetu wa Ukerewe, mimi nilifikiri viongozi wetu ndo hawana huruma na wananchi kiasi cha kuifanya nchi haitamaniki kumbe hata sisi tuliokuja ughaibuni kusoma na kutafuta maisha hatuitakii nchi yetu maendeleo.
    Kweli kweli bado kuna mtu na akili zake yuko ughaibuni ameona kwa macho yake nini kinafanyika ughaibuni ili kuendeleza nchi lakini bado anapapasa mdomo kwamba kidumu chama cha mapinduzi.
    Unajua rafiki yangu aliwahi kunimbia kwamba alivyofika ughaibuni akagundua kwamba Watanzania wana laana, nilimkatalia ila sasa naona inawezekana kuna ukweli ndani yake.

    ReplyDelete
  11. Tunsomsns repoet ya mwaka mzima toka hivyo vyama vianze nadhani vimeshafikisha mwaka.....sasa jamani hebu tuambieni mmefanya nini katika kipindi hicho? Ili na siye ambao hatujajiunga basi tuwe na moyo...Sytaki kusikia kuwa mmeweza kuandikisha wananchi kadhaa...bali mmefanya nini na hiyo hela mnayopata kwa uwanachama mumeiwekeza wapi na faid ani ipi....? nadhani tukiona haya tutakua namoyo wa kujiunga na chama hata tusio wapenzi wa siasa...You know people are fired up....read to go...siku hizi sio mikutano tu kila siku..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...