Habari za kazi kaka.....
Mimi ni mdau wa globu yetu ya jamii. Nipo hapa Lund, Sweden. Leo nilikuwa nafanya google search kutafuta radio yoyote inayopatikana online ikitangaza kutokea Tanzania. Sikufanikiwa kupata radio station yoyote kaka.
Kama kuna mdau anajua link ya kituo cha radio ambayo naweza kubofya na kusikiliza habari za nyumbani au hata TV station hata kama ni ya kulipia naomba airushe hiyo link hewani.

Cha kushangaza ni kwamba nilipobadili neno Tanzania na kuweka Kenya badala yake, nimepata station kibao za radio za pale Nairobi na hata fm stations za vijijini Kenya. Hii imekaaje wadau? Ina maana redio zetu ndo zinaishia Magomeni tu? Msaada wajameni...

Mbona majuzi wakati nipo Dar nilikuwa nasikia www dot komu kibao kwenye redio? Au ndo zile zile doti komu za akina Masanja Mkandamizaji ambazo huwa hazi-exist?
Naomba msaada wajameni.....
Naitwa Mwemezi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Unaweza kusikiliza online Radio Maria kwa kubofya link ifuatayo"
    http://radiomariatanzania.co.tz/v2/

    ReplyDelete
  2. Ndio mdau mwenzangu kwa kweli inasikitisha kuona Wamiliki wa Radio tofauti tofauti wanashindwa kuweka matangazo yao yawe yanapatikana kwenye tovuti.

    Sioni sababu ya msingi Redio kubwa kama Radio One,Radio Tanzania DSM, Clouds FM, Radio free Africa nk kutokuwa na online live radio wakati Radio maria TZ wanay. Cha kushangaza zaidi hata TSJ ambayo ni taasisi iliyopaswa kuwa mfano haina kilichopo ni kivuli tu hiyo radio hai fuction. Kuhusu TV STAR TV UNAWEZA KUON ya kulipia ila wazushi tu wanaweka recorded programmes na wala sio live unless wamejirekebisha.
    Kwa hiyo basi kuhusu Live Radio kwa nchini mwetu tembelea LIVE RADIO
    http://www.live-radio.ne/info.shtml
    THEN CLICK AFRICA THEN CLICK TANZANIA ITAJITOKEZA RADIO MARIA HAPO UTAENJOY LIVE BROADCAST, IKIWA NI PAMOJA NA TAHARIFA ZA HABARI LIVE.


    Enjoy it B. Kimbache Kipatimu Kilwa.

    ReplyDelete
  3. Japo siandiki kutoa msaada (samahani), Naandika kuunga mkono kabisa ombi lako, nikimaanisha kama kuna mtu ataweka hiyo link basi hata sisi huku mashariki ya mbali tutafaidika

    ReplyDelete
  4. wewe usilinganishe kenya na tanzania,siku zote mnaambiwa kenya ni anga zingine

    ReplyDelete
  5. Hawa watu walituwekea tv star na chamnnel ten.lakini habari zilikuwa zimepitwa na wakati sanaaaa,wanarekodi ndio wanatuwekea,taarifa ya habari ya jumapili unaipata alhamisi ijayo..wewe redio kali ni redio maria..tuwachangie jamani redio maria.kwa kuwapa chochote kila..mdau norway

    ReplyDelete
  6. radio online www.live365.com/ingoo music 24/7 Franco,Koffi,Madilu,
    Mabele, Pepe Kale, Nyboma Mwadindo Tabuley, Tshala Muana, Pierrete Adams, Mlimani Park, Ongala n.k listi ni ndefu naomba uende kwenye site mwenyewe.

    Site nyingine kwa ajili ya kuweza ku-download miziki ya afrika mashariki tembelea: www.ntwiga.net/blog hapo una download vitu bila tabu.
    Rocky
    London

    ReplyDelete
  7. Huwezi kufanya comparison ya kenya na nchi yetu. juzi nilipita pale Jomo kenyata airport nilishindwa kuhesabu madege ya Kenya airways.Leo nimesoma Tanzania Daima na mkurugenzi wa ATCL anasema Tuna Ndege Tatu na sijui zote ni mbovu

    ReplyDelete
  8. Huwezi kufanya comparison ya kenya na nchi yetu. juzi nilipita pale Jomo kenyata airport nilishindwa kuhesabu madege ya Kenya airways.Leo nimesoma Tanzania Daima na mkurugenzi wa ATCL anasema Tuna Ndege Tatu na sijui zote ni mbovu

    ReplyDelete
  9. wadau wenzangu karibu mtapata radio za kitanzania live streamin kwenye link ya www.radio.co.tz tuko mbio kuanza kabla nafikili mpaka mwisho wa mwezi oct itakuwa tayari, naomba maoni yenu kwa msaada wa kufunikisha hili email yangu gkusila@hotmail.com

    ReplyDelete
  10. www.radio.co.tz karibuni itakuwa itakuwa inawaletea live streamin radio kutoka tanzania kwa maoni tuma gkusila@hotmail.com

    ReplyDelete
  11. www.radio.co.tz karibuni itakuwa itakuwa inawaletea live streamin radio kutoka tanzania kwa maoni tuma gkusila@hotmail.com

    ReplyDelete
  12. Ni radio Maria tu wengine wote wazushi.
    Triple M na Clouds walikuwa hewani wakapigwa shoka moja chini mpaka leo na kama kawa hata hawasemi nini kinaendelea! Hii ni tabia mbaya sana kama chombo cha habari kinataka kuwa credible!

    Kama ilivyojulikana wakati huo, Radio Tanzania / TVT wakati fulani tulijulishwa hapa kuwa oh! wataanza hivi karibuni mpaka tukapewa na tovuti hapa jamvini. Yamebaki maneno tu na hata hawajaomba msamaha kwa kutudanganya mpaka kesho! Tabia ile ile kutoomba radhi.

    Ni aibu kama Taifa lnakosa angalau Radio mtandaoni mpaka tunabaki kumsikiliza Mwanakijiji tu na jamii forums mpaka tuchizike! Walisema 'Hulka hujaza.....'

    Kumbukeni kuwa information is power!
    Mh. Waziri wa habari, hata kama walioko nje au kwenye mitandao ni wachache kuliko wengine, huwezi kukaa kimya juu ya hii changamoto, maana wakitokea akina 'Michael Moore' wawili tu kutuhabarisha ya kwetu Tanzania kwa mitizamo yao basi tusije kulaumiana!!

    ReplyDelete
  13. tuondolee inzi hapa wewe kama unataka kusikiliza redio za kibongo si urudi bongo, au ndiyo tamaa ya kutaka vyote.vilimshinda fisi

    ReplyDelete
  14. WADAU HABARI HUWA HAIPITWI NA WAKATI PIA GAZETI HALIPITWI NA WAKATI NDIO MAANA KUNA MAKTABA ILI KUTUNZA KUMBUKUMBU USIJALI UMEPATA HABARI WAKATI GANI JALI TUU UMEIPATA MFANO LEO NI TAREHE 13 SEPT GAZETI LA TAREHE 20 MWEZI WAA NANE LINA MATOKEO YAKO YA SHULE SASA UNA PESA YA KUNUNUA GAZETI GAZETI MOJA HUWEZI KUNUNUA LALEO UKAACHA YENYE HABARI MUHIMU. AINA MAANA GAZETI LA KESHO NI MUHIMU. HABARI SIO KAMA CHAKULA FRESH AU KILICHOCHACHA. HABARI ZA UMUHIMU NA HARAKA NI KAMA ZA HALI YA HEWA. MFANO HIKI NI KIPINDI CHA CLAB RAHA LEO JULLIASI NJAISANGA MIAKA HIYO HEBU SIKILIZA

    http://www.eastafricantube.com/media/11745/CLUB_RAHA_LEO_SHOW-JULIUS_NYAISANGA/

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...