Je Nape Nnauye (pichani) anajutia uamuzi wake wa kukemea kile alichokiona kuwa ni ufisadi ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM, jumuiya ambayo anataka kuiongoza? Sikiliza mahojiano hayo hapa na pia kwenye klhnews.com.


Wakati huo huo toleo letu la nne la kijarida cha "Cheche za Fikra liko mitaani" na kwenye mtandao wa klhnews.com jipatie nakala yako bure kabisa.


Ukitaka nakala ya kijarida hicho ikufikie moja kwa moja kwenye email yako tuandikie


mhariri#

klhnews.com

ambapo alama ya # imesimama badala ya @.


Title: KLH News Episode:

Mahojiano na Nape Nnauye kuhusu kusimamishwa uanachama


/entry/2008-09-08T21_58_59-07_00

Enjoy!
thumb/13384/300x300_1203612.jpg

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Wapiganaji hawafi kirahisi. kama walijua wanammaliza kijana yule waliyemtengeneza wenyewe, basi wamemwimarisha. Nyerere alitabiri: Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM. Nenda Nape, nenda!!!

    ReplyDelete
  2. Kiukweli mshkaji wamemuonea. hakuna democracy CCM hii imedhihirisha kweli ni chukua chako mapema. Kwanini wasimpe warning letter? Mbona Mafisadi wachukulia hatua za haraka maka walizompa Nape? Weka wazi kaka Michuzi kosa alilofanya Nape hadi wamsimamisha ghafla. Wafanye hivyo pia kwa mafisadi sio kwa watu wa chini tu au sheria ni kwa wanyonge tu? wenzetu wa juu sheria haiwagusi. inauma sana.

    ReplyDelete
  3. CMM kama Chadema na CUF zina taratibu na kanuni zake katika kutoa maoni. Wangwe alikeuka taratibu za Chadema akatimuliwa cheo chake. Nape amekiuka kanuni za CCM na ana kila haki ya kutimuliwa.

    Watanzania tusipojifunza kufuata kanuni tulizozitunga wenyewe hatufiki tunakokusudia.

    ReplyDelete
  4. Nape.....Nape....Nape chama kina wenyewe hicho ulikuwa hujui?Hiyo ndio tabu ya kuwa na hao akina Makamba walioishia form four na wanafanya CCM kama wamerithishwa na wazazi wao.Yani wanadhani kila mtu anafurahia na maovu wanayofanya,wanadhani wataburuza kila mtu katika ulimwengu wa sayansi na tknolojia kani hawajui siku hizi dunia ni moja na inaitwa kijiji ambapo watu hujifunza kutoka sehemu nyingine duniani?Makamba utawala wa Imla haupo kwa sasa inabidi mkubali changamoto kwa sababu wananchi wameamka.Nape wewe bado kijana na naamini siku moja utafika tu hata kama si katika CCM vyama viko vingi japo sio strong sana lakini nenda hata Chadema.Na nyie akina Makamba imefika wakati mnatakiwa mfahamu hiko cahama si cha kisoshalism ambapo watu hamna sauti.Kwa mtindo huo ufisadi hauishi na utaendelea kutokea CCM kila siku.Kwani mtu kukosoa chama ni kosa sasa mnadhani mtajifunza lini?me nafikiri mjifunze kutoka kwa wenzenu Democrats na Republican ambao wamekomaa me naona nyie mnapoteza muda tu,kwa mfano hii hoja "Nape pia amekuwa akiweka alama ya kuuliza kwenye uhai wa mradi huo hasa katika kipengele kimojawapo ambacho kinasema kwamba mwekezaji ataendeleza mradi huo milele, huku Jumuiya hiyo ikipata asilimia 25 na mwekezaji akipata asilimia 75" ,yani bado mtu mnamuona mmbaya au ndio vile mnanufaika?Yani I wish ningeweza kuibadilisha hii nchi na vingozi wake.Naamini hivi vyama vina matatizo ya sera,wataalam na si ushabiki kama wa akina Makamba na Kingunge.Nasisitiza tena wapendwa tuamke elimu ya uadilifu ianzie chini ili tuwe na watu wanaofaa.Nilikuwa napenda sana siku moja kuwa mwanasiasa lakini kwa sasa sitamani manake najua mimi napenda kuhoji karibu kila kitu kwa lugha nyingine mimi ni skeptik so naona nikiingia katika chama kama hiki watanitoa sadaka bure,bora niachane na haya masuala.Vijana lazima muwe na kauli mbiu hakuna kuburuzwa lazima muhoji ni haki yenu mkiwaacha hawa viumbe na huu urasimu wao mtabakia ndio na mtachelewesha maendeleo katika nchi yenu.Najua wengi tumewapoteza lakini kama umeyavulia nguo maji ni lazima utayaoga kama si kunawa miguu.Vijana nyie ndio taifa la leo na si la kesho hao wakina Kamba wansogeza siku tu lakini nyie ndio wenyewe.Naomba kuwakilisha

    ReplyDelete
  5. Poor guy...

    Kwa mwendo huu haturudi bongo ng'oooooo.

    Sasa kama umri umeenda kidogo hupati kazi nchi gani hiyo?

    Kweli tukizamia huku mtatusema?

    ReplyDelete
  6. Huwezi kuibadili CCM. Cha muhimu bro bora uanze na ukatetee maslahi ya walalahoi kwenye chama kingine. CCM Ina wenyeqwe na wewe si mmoja wao nadhani kwa sasa utakuwa umeelewa. CCM bado ina mizee yenye fikra za kiujima na hawawezi kuelewa ukweli wa mambo.
    kakbla ya kushushiwa kijini au kukutwa na makuu bora uanze kwani wewe si wa kwanza kutaka kuitingisha CCM bila ya mafanikio.
    walala hoi watakuelewa zaidi pale unapokuwa na msimamo hata ikibidi ni kupoteza nafasi na maslahi.

    ReplyDelete
  7. Nape, hiyo ni changamoto, nakupa tano kubwa sana. Hao jamaa zako wamelelewa kifisadi, sasa wewe unaposema kinyume na maadili yao mabovu walokuzwa nayo kwao tabu tupu. BIG UP SANA.

    ReplyDelete
  8. YAANI NYIE KWANI MMESAHAU UTAMADUNI WA KIAFRIKA??? MBONA MNACHEKESHA.....NGOJA NIWAKUMBUSHE... MKUBWA AKIJAMBA HATA KAMA UMESHUHUDIA INABIDI UNYAMAZE

    ReplyDelete
  9. Nape usife moyo Mungu yuko pamoja nawe. Hiki chama cha mafisadi ccm sijui lini kitajirekebisha na huyu raisi mkwere sijui alitoka wapi anazidi kumkumbatia lowasa anaona ndie mshauri wake. Hilo jengo la umoja wa vijana aliyeliuza ni Lowasa hamjui kajiuzuli lakini huyo mkwere anazidi kumtetea tu mwaka 2010 hatumtaki madarakani bora mapambano yaanze mapema kumtoa jk hatufai kabisaaaaaaaaaaaaa na hao akina makamba wake wasiojua lolote, mikakati inaendelea 2010 kutakuwa na sisiem mbili moja ccm ulaji ya pili ccm wapenda maendeleo tumechoka jamani. Watanzania tumeichoka CcM inanuka rushwa,unyanyasaji,uonevu,uchawi,ushirikina,uuaji na mengine mengi.

    ReplyDelete
  10. Nape usife moyo Mungu yuko pamoja nawe. Hiki chama cha mafisadi ccm sijui lini kitajirekebisha na huyu raisi mkwere sijui alitoka wapi anazidi kumkumbatia lowasa anaona ndie mshauri wake. Hilo jengo la umoja wa vijana aliyeliuza ni Lowasa hamjui kajiuzuli lakini huyo mkwere anazidi kumtetea tu mwaka 2010 hatumtaki madarakani bora mapambano yaanze mapema kumtoa jk hatufai kabisaaaaaaaaaaaaa na hao akina makamba wake wasiojua lolote, mikakati inaendelea 2010 kutakuwa na sisiem mbili moja ccm ulaji ya pili ccm wapenda maendeleo tumechoka jamani. Watanzania tumeichoka CcM inanuka rushwa,unyanyasaji,uonevu,uchawi,ushirikina,uuaji na mengine mengi.

    ReplyDelete
  11. utanyamaza wewe fisadi nani anaweza kuvumilia ushuzi wa mtu koma. utamaduni gani wa kiafrika mbona uko kama makamba wewe s*nz#4

    ReplyDelete
  12. Mnauye karibu sana katika Chama tarajiwa cha:-
    CCMC yaani 'CHAMA CHA MAPINDUZI CHANYA' AMBACHO KINAONGOZWA NA WAZALENDO-MAWE AMBAYO WAMEYAKATAA WAASHI NA 2010 YATAKUWA MAWE MAKUU YA PEMBENI!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...