kila mtu na wake wakati Rhino ya morogoro (jezi za njano) walipochuana na Kijiweni ya Mbeya
Picha na habari na John Nditi, Morogoro
TIMU ya Rhino FC ya Mkoa wa Morogoro inayoshiriki ligi Dalaja la kwanza msimu huu imeutumia vyema uwanja wake wa Jamhuri wa mjini hapa kwa kuilaza timu ngumu ya Kijiweni ya Mkoa wa Mbeya kwa magoli 3- 1 katika mchezo mgumu wa kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya kucheza ligi kuu msimu ujao.

Katika mchezo huo ulifanyika wikiendi hii katika uwanja wa Jamhuri wa Mjini hapa, wageni ndio waliokuwa wa kwanza kuzifumamia nyavu za Rhino katika dakika ya sita kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na mchezaji Bahati Silinjanje, na kumshinda kipa wa Rhino, Siri Sinai na hatimaye kujaa wavuni.

Hata hivyo katika kipindi hicho cha kwanza , timu ya Kijiweni iliweza kumiliki mchezo huo kwa kiasi kikubwa hali iliyoashiria kuwa ingeweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo uliokuwa ni wavuta ni kuvute.

Hata hivyo zikiwa zimesalia dakika nne, Rhino ilipata penati baada ya mchezji wake Tito Andrew kuangusha katika eneo la hatari na mwamuzi Alex Mahagi kutoka Jijini Dar es Salaam kuamuru ipigwe peneti kuelekea lango la Kijiweni na bila ya ajizi Mchezaji Josephat Jackson alipachika wavuni penati hiyo na kuandika goli la kusawazisha.

Timu hizo zilianda mapumziko zikiwa nguvu sawa, lakini katika kipindi cha pili , Rhino FC ikicheza kwa kushanmbuliwa kwa kushitukiza iliweza kujipatia bao la pili katika dakika ya 63 kupitia mchezaji Prosper Mkwama, baada ya kuunganisha krosi ya Kampo Ramadhani ya kumwacha kipa wa Kijiweni, Apolinal Edward akiwa hana la kufanya.

Hata hivyo timu hiyo ya Kijiweni licha ya kucheza pasi ndefu na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa Rhino, ilijikuta ikipata pigo katika dakika ya 89 kwa beki wake wa kutumainiwa Rahim Omari kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambu mmoja wa wachezaji wa Rhino, awali mchezaji huo alikuwa na kadi ya njao.

Mwamuzi wa mchezo huo aliamuru mpira wa adhabu na bila ya kusita mchezji wa Rhino , Baya Kassim , shuti lake likaenda moja kwa moja hadi wavuni na kuandikia timu yake bao la tatu katika dakika hizo za majeruhi.

Kocha Mkuu wa Rhino , Ally Jangalu, amesema huo ni mwanzo mzuri ikizingatiwa timu hiyo imefikisha poiti nne katika michezo yake mitatu kwa kushinda mmoja, sare mmoja na Ruvu Shootin ya 2-0 na kupiteza mmoja dhidi ya Pilisi Iringa kwa goli 1-0.

Kwa upande wake Kocha wa timu ya Kijiweni, Yusuf Hussen , alisema kufungwa kwa timu yake kwa magoli hayo kulichangiwa na maamuzi mabaya ya mwamuzi huyo.

" Wachezaji wangu walicheza vizuri katika muda wote wa kipindi cha kwanza…lakini kutolewa kwa penati kwa mazingira ya utata na kuingia kwa goli hilo kuliwavunja kuvu wachezaji wangu" alisema Kocha huyo.

Hata hivyo alikiri kuwa goli la pili la Rhino ndiyo goli lililokuwa nzuri na halikuwa na ubishi kutokana na kugongeana vizuri kwa wachezaji hao kabla ya kutolewa kwa krosi iliyomfikia mfugaji na kuandika goli hilo.

" Haya magoli mengine ukiachia lile la dakika ya 63 yamechangiwa na mwamuzi na kutokana na hali hii tunawaomba TFF wamewakini na waamuzi wa michuano hii" alisema Kocha huyo.

Timu hiyo hadi sasa imefikisha pointi tatu inatarajia kurudiana hivi karibuni kucheza mjini Mbeya na Ruvu Shooting , ambapo hadi sasa imecheza michezo mitatu , imefungwa mmoja na Rhino 3-1 , sare ya magoli 2-2 na Ruvu Shooting na kupata ushindi dhidi ya Ashanti ya magoli 2-0.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...