juu nikiwa na mdau wa italy baraka wa chibiriti break point ya mjini kabla ya ramadhani kuanza, chini chibiriti, mie na mdau wa dubai, ustaaz mansab, hapo hapo break point kabla ya mfungo kuanza
Hi Bro.Michuzi.
POLE KWA SHUGHULI.
Kwanza kabisa natoa salamu zangu nyingi sana kwako na kwa wadau wote wooteee....!!!!!!
Napenda sana kutoa shukrani zangu nyingi sana kwa kunipokea vizuri sana na kunitembeza kwenye ofisi yako, na kunipa mlo wa nguvu wa mchana yaani sasa naukumbuka sana baada ya kurudi huku, nikiangalia picha hizo hamu inaniijia ya msosi wa huko kwetu Bongo.
Pia natoa shukrani nyingi sana kwa wadau wote wana fotobaraza kwa kunipokea na kuniaga vizuri sana hapo makumbusho Dar. Kwakweli lengo langu hasa la leo ni kushukuru sana tena sana, baada ya safari yangu ya kurudi huku kwenda salama kabisa.
Pia natoa salamu sana kwa wadau wote wa blog hii najua kuna wengine watakuwa wamenimiss sana, pia wengine......sisemi sana, mimi natoa salamu sana kwa woteee bila kubakugua hata mmoja, nasema nimerudi kuendeleza libeneke kama kawaida ulingoni.
Kila lakheri kwa wote hasa mwezi huu mtukufu, tuzidi kupendana sana siku zote, kama tulivyo siku zote watanzania.
Salamu sana
Kila lakheri kwa wote hasa mwezi huu mtukufu, tuzidi kupendana sana siku zote, kama tulivyo siku zote watanzania.
Salamu sana
B.F.CHIBIRITI.


wee chiriti unarudi lini italy'
ReplyDeleteChibiriti hata mimi nimekumiss, wanasemaje huko Italia? je umepata mtanzania mwenzako huko?
ReplyDeleteAu umekuja TZ kutafuta jiko la kiswahili?
ebwanae,chibiriti ndani ya nyumba!! karibu tena kwenye blog mtu wetu!!!kwi kwi kwi...
ReplyDeleteMichuzi huyu jamaa naona kama una relate naye kidogo, au ni jamaa wa familia?
ReplyDelete