mh. balozi,
asante kwa kuanzisha libeneke la taswirazzz. hapa nami naomba nichangie huku nikikuuliza wewe na wadau je ungekuwa wewe ungfanyaje katika hali kama hiyo. utatoka uende mjini kutafuta matariri mapya ama utabaki garini ufe na njaa??
mdau sauzi
-----------------------
mdau sauzi,
dah! hii kali. mie bwana ningekufa na njaa kuliko kuliwa laivu na hao wadudu. yaani kama tairi linaliwa kama steki je kapaja kangu si katakuwa kama soseji?
hata hivyo picha bomba na zimekidhi kila haja, ya kuelezea stori. isipokuwa mpigaji angefungua kioo cha gari lake na kupiga kamera ikiwa huru ingekuwa bomba sana. kioo cha gari kimeleta ukungu kwa jaaaamu.
mwanga hauna shida sana kwani naona kulikuwa na kawingu kalikoziba jua, vinginevyo kwa muda huo rangi ingefubaa. hata hivyo unasamehewa kwani hapo hakuna jinsi zaidi ya kupiga ukiwa garini huku vioo umefunga.
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Taswira hizi kwa kweli zimeniacha hoi, ila ninachoshangaa mbona waliopo ndani ya gari hiyo sura zao tofauti na zoezi linaloendelea nje ya gari! They don't look scared at all! Yaani ndio kwanzaaa wanaendelea kuonyeshana sijui wanyama wengine au milima! Bro Michuzi, wewe mwenzetu una utaalam wa picha naomba kueleweshwa halii hii nyie wataalam mnaiitaje! Au mie ni uoga wangu tu?!! Manake wenzetu wamejaaliwa kuwa watu wa kupenda adventures...

    ReplyDelete
  2. daaaah!!!
    ningekufa kbs,,,yan izi mnyama mbona wanauwezo wa kubomoa ata kioo cha gari walahi wakiwa na izi njaa,,,
    hii pic ni kweeeli kbs,,,wazungu bwana hawaogopi kbs izi vitu yan wana mioyo ya ajabu mno

    ReplyDelete
  3. Michuzi , Simba anakula tairi na kunguruma hapo chini wewe unawashawauri wafungue kioo wapige picha ...kwa nini unawatakia wenzako kifo ?

    ReplyDelete
  4. hehehe nice taswira ila hao jamaa hawapo scared wanajua kunaulinzi nearby na pia wanabinduki wakileta nyodo wanawapiga walale sio kuwaua

    ReplyDelete
  5. Mdau wa kwanza hapo juu ukipiga hesabu ndogo tu utagundua kuwa kuna mtu (au kundi la watu) wengine ambao alikuwa anapiga hizo picha. Kwa hiyo ukute huyo mtu ndio alikuwa anakuja kuwasaidia ndio maana hawana mcheche.

    ReplyDelete
  6. kwani unadhani nani kapiga hizi picha wewe? Mbona unakuwa na maswali ya ajabu?
    Jiulize...mpiga picha yuko wapi? Ndo utaelewa kwa nini wasiwe na wasiwasi.

    Au siku izi national park kumefungwa CCTVs....tehehehe


    mtoto

    ReplyDelete
  7. na uhakika bro michuzi kutokana na kutaka picha bora yani ungetoka nje ya gari kufotoa hilo tukio,nakuaminia mzee

    ReplyDelete
  8. Mdau wa kwanza hapo juu ukipiga hesabu ndogo tu utagundua kuwa kuna mtu (au kundi la watu) wengine ambao (w)alikuwa (w)anapiga hizo picha. Kwa hiyo ukute huyo mtu (au hao watu) ndio (w)alikuwa (w)anakuja kuwasaidia ndio maana hawana mcheche.

    ReplyDelete
  9. Michuzi, hii picha inanikumbusha siku mimi na marehemu mpiga picha wa Daily News, Clement Matuja, tulivyokutana na simba dume wawili huko Mikumi National Park. Tulikuwa ndani ya Land Rover ya World Wildlife Fund tunaelekea Lodge kwa dinner. Basi wakatokea simba kama hao kwenye picha wanatembea katikati ya barabara kama vile ni barabara ya baba yao. Basi dereva alismamisha gari, huko tunahaha ndani ya gari. Woga ulimshika Matuja, badala ya kufunga dirisha lake alikuwa anafungua.

    Kwa bahati nzuri hao simba walitupita kwa staili. Kila moja kashika upande wake wa gari halafu waliendelea na safari yao.

    ReplyDelete
  10. kwa uzoefu wangu wa porini hawa simba inaelekea hawakupata msosi kama siku 5 au 7 hivi ndiyo maana wamekuwa desperate kutafuna matairi(kutowa upepo)Hii inaonyesha sio binadamu wanaopiga mahesabu ya hisabati.tehe tehe tehe teteteee

    ReplyDelete
  11. Nina hakika kuonekana kwa muokoaji haina maana uokoaji tayari, unaweza ukaangalia kwa mtazamo mwingine kuwa hilo gari lingine lenyewe limekuja na matairi ya chuma kuwa hayatatafunwa? Au wamekuja na uezo wa ajabu kuwa wao watashuka kwenye gari na kubadili tairi au kufunga gari kwa ajili ya kulivuta bila kudhurika? Though the idea of bunduki za usingizi looks better, if and only if, waliokuja ni wataalam wa mbuga/hifadhi na siyo adventurers wenzao.

    Wadau wengine bwana, kama swali ni ajabu kwako kwa wengine ni tofauti, hutadhurika kwa kutumia ustaarabu kwenye responses zako....

    ReplyDelete
  12. Mimi nauliza yule kifaru ama kiboko pale langoni mwa ngorongoro crater bado yupo? Kuna jina walikua wanamuita la kike mara mbili alishatufanya tujikojolee wengine.

    Hawa watu hawaogopi kwa vile simba hawezi kusukuma hilo gari yule sijui kiboko au kifaru pale alikua anasukuma na kupiga gari

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...