njia kuu ielekeayo el mourada nje ya jiji la khartoum
katikati ya jiji la khartoum
mojawapo ya alama za jiji la khartoum ni hilo jengo ambalo ni hoteli inayomilikiwa na libya
barabara zaa khartoum ni pana na safi na zina alama zote muhimu
hapa ni katika ukingo wa mto nile ambapo inakutana white nile na blue nile. angalia maji ya upande wa kuume ambayo ni mekundu (blue nile, maji yake yakitirika tokea ethiopia) na upande wa kulia ni meupe (white nile ambayo maji yake yanatiririka toka lake victoria upande wa kaskazini) katika sehemu inayoitwa al-mogran
mkuu wa wilaya ya nanihii akiwa khartoum, sudan, kwenye vekesheni ya mwezi mtukufu



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. The fulana's

    ReplyDelete
  2. We kwenda zako acha kutu kambaisha sisi, vekesheni wapi ,uko na JK huko , muone kwanza na kifulana chako !

    ReplyDelete
  3. As salaam aleikum Sheikh Michu!
    Hongera kwa kuwa huko mwezi huu mtukufu wa Ramadhan - Tatizo hapa ni FULANAZZZZZZ!
    Kwikwikwikwikwi!!!!

    ReplyDelete
  4. Kweli hii blog yako, ukienda vichakani kunya unatuambia, ukiwa bila shaka! haya uwenatuambia na unapotoa huduma nyinginezo.....!

    ReplyDelete
  5. hi Bro michuzi hiyo fulana ndio uniform yako? maana naona picha nyingi ni kifulana kitaimba alleluya

    ReplyDelete
  6. Kaka Fulanaz inatalii kushinda mimi ziara njema mchunge JK asije akaacha kufunga

    ReplyDelete
  7. kakaaaaa wewe kila siku vekesheni?

    ReplyDelete
  8. Ramadhan Kareem Sheikh Michuzi!!!

    Wadau msikalie kupiga kelele fulana fulana, si mumuulize mkuu wa wilaya ya tegeta ina siri gani hiyo fulana...!!!!

    Mdau

    ReplyDelete
  9. mmnh hiyo fulana si bure, tushakuweka alama kwa hiyo fulana, ingekuwa na mdomo ingesema jamani nimechokaaa lol!!

    ReplyDelete
  10. Sasa wewe Michuzi kila trip ni vekesheni!? au huijui maana ya vekesheni?

    ReplyDelete
  11. Swali Ni Kwamba!..Hiyo FULANAZ Unaitunza Vipi?..Manake Haichuji..lol...Ur The Greatest Michuzi!..Pamoja!

    ReplyDelete
  12. Mshukuru Sana JK Usingepanda Ndege

    ReplyDelete
  13. Michuzi, tunacheza nao hao hivi karibuni usisahau kuchukua mchanga ndani ya 18 na katikati ya uwanja niletee niufanyie kazi. Nitafute ukirudi.

    ReplyDelete
  14. Kuna mdau hapo juu ana hasira kweli unaposema uko vacation ....Big bro take it easy ....watu wengine sijui njaa au vipi....

    Kwani akisema vacatio nyie inawauma nini...?????????????? kazi yake naimind sana tu ninavyopenda kutembea hata mimi ningeringa kama ningekua na kzi inanitembeza allover the world like him

    ReplyDelete
  15. Cha kusikitisha ktk watu ambao wanashangaza kwa vitimbwi kama watanzania na vilevile wepesi kulaghaiwa ,sasa huyu kaka wa watu yuko kazi au vekesheni tatizo ni nini , hatuwezi kuandika mambo ya maana mpaka tumtusi mtu yeye anajaribu kutuonesha kile ambacho watu wengi tulikuwa hatukioni kama picha na habari za nyumbani, jamani imefika wakati tutambue michango na kazi za watu sio tusubiri mpaka afe ndo tuseme ukweli wetu wa maoni huyu kwa mtazamo wangu ni mtu maarufu sana kiasi cha kuwa tishio pale atakapoamua kuingia kwenye siasa za tanzania

    ReplyDelete
  16. KAKA MICHUZI FULANA NI YAKO BWANA HIYO INAONYESHA NI JINSI GANI ULIVYO MWANA UCHUMI NA MAENDELEO NDIO YANAKUJA KWA KUWA HIVYO ILI MRADI TU HAINUKI KIKWAPA, SASA HAPO SUDAN UKIPATA MUDA NENDA HAPO KWENYE SUPERMARKET KUBWA KULIKO ZOTE SUDAN NI KARIBU NA AIRPORT INAITWA AFRAA UKALE ICE CREAM ZA KILA AINA UKITOKA HAPO BASI UENDE KUNA SOKO MOJA KUBWA SANA UKAJIONE MWENYEWE KARIAKOO YA HAPO PIA USIHAU KUPANDA BAJAJ ZIPO NYINGI SANA HAPO ZINAITWA TUKTUK,USISAHAU HAIRUSIWI KUNYWA LAGA WALA KUVAA KAPTULA JAPO JOTO LA CHINI NI NYUZI JOTO 40.
    KAMA WEWE NI MTU WA GYM AU SWIMMING BASI NENDA CLUB MOJA INAITWA GERMAN CLUB LAKINI SIKU YA ALHAMISI NI SIKU YA KINA MAMA PEKE YAO KINA BABA NOOOOOP,
    USISAHAU KABISA KUPIGA PICHA CHAKULA KIKUU CHA WASUDAN KINAITWA FUUUUUUL
    BALTAZAR
    KIPEPEO TOURS

    ReplyDelete
  17. Michuzi achana na waosha vinywa. Kula vekesheni yako kiulaini.

    ReplyDelete
  18. Kazi nzuri mkuu wa nanihii. Asante kwa kutupa vidokezo vya Khartoum. Sijui wabongo elimu yetu inatusaidia nini. Hata mtoto wa darasa la saba atatambua kuwa Michuzi anatumia lugha ya picha, istilahi, utani, nk. ikiwa ni katika jitihada za kufanya anayotupeperushia yasitu-bore, km mkuu wa nanihii, vekesheni, nk sio lazima kuyachukulia katika maana zake za msingi. Nyie watu mmepata elimu kiasi gani? Ngumbalu?
    Swali kwa mkuu wa nanihii: 1)utamaduni umenipita kando, mkono wa kuume ni upi? na unahusianaje na mkono wa kulia?
    2) Je vakesheni itakufikisha hadi Darfur ili uweze kutumegea ya huko?

    ReplyDelete
  19. Twende mbele turudi nyuma ingawaje hawa jamaa ni maskini kuliko sisi lakini infrastructure zao zinapendezesha macho.Angalia hizo barabara zilivyopana na safi kama vile mamtoni.Kwa muonekano huu hapa inaonyesha wapanga mji wa sudan walikwenda hadi form 4 wa kwetu waliishia form 2.Barabara za home zimefinyana kama nyanya ktk tenga.Sidhani hawa jamaa wana shida ya kupanua barabara kila muda.
    I've never been there.Im judging from the appearence of the photos

    ReplyDelete
  20. NAKUUNGA MKONO MTOA MAONI WA SEPT 07,2008 10:35 SAWA KABISA ULICHOKIANDIKA. KAZI IPO YA KUILIMISHA WATU HATA YASIO YA MUHIMU ITABIDI KUELIMWISHWA TUKITEGEMEA NI RAHISI KUELEWA LAKINI BADO AU SIJUI NI ROHO MBAYA.... NAMFAGILIA SAAANA BWANA MICHUZI .

    ReplyDelete
  21. asalam aleykum kaka michu, naomba unisaidie hilo hotel hapo khartoum mbona liko na shepu ya bomu? na hivyo basi linamaana gani kwa sudan na Libya? naomba majibu kaka.
    mdau
    ETM

    ReplyDelete
  22. mdau Mbigiri, kwa mujibu wa takwimu za shirikala fedha duniani, IMF, pato la ndani la taifa kwa kaya (per capita GDP) la Sudan kwa mwaka 2007 ni dola za kimataifa 2,171.874 (nafasi ya 123 duniani), wakati Tanzania ni 1,255.956 (nafasi ya 156 duniani). Wakati takwimu za Benki ya Dunia inaonyesha kuwa pato la Tanzania ni takribani dola za kimataifa 1208.622 (nafasi 123) na Sudan ni 2087.768 (nafasi 145). Hivyo hawajatuzidi umasikini (kama ukichukulia wastani kwa kaya). Sema tu kwa wenzetu hawa naona kutakuwa kuna "magepu" makubwa kwa ajili ya vita, ukame, n.k. Uwiano wa maisha kati ya tabaka la juu na ndugu zetu wa Darfur ni tofauti sana.

    Nakubaliana nawe kuwa kwa picha chache hizi za Khartoum, inaonekana kimiundombinu jamaa wametuacha mbali. Hii ni pamoja na matatizo yote yaliyowakumba. Fikiria bila ya hivyo wangekuwa wapi. Naona wanayumia vyema mafuta na pamba... sis dhahabu yetu vipi jamani?

    ReplyDelete
  23. Hawa viongozi wa kibongo, hawana mpango wowote. Ukimsifia mtu tuu unapewa post. Michuzi mara nyingi unasafiri kutokana na taaluma yako ya uandishi, pia ni mwajiriwa wa Daily News. Unapata muda gani wa kuangalia matatizo wilayani kwako? Kweli kwenye fungu huenda nyongeza, kodi za ndugu zetu zinaliwa bure bure tuu, hata kama mtu hafanyi kazi, ili mradi umsifie kiongozi fulani na usiandike maovu ya serikali. Kaka Michuzi uache unafiki, hata kama hukuweka comment hii. Sio Sudan, UK, tuwekee na picha za Manzese uwanja wa fisi na vijijini huko bongo, tuone hayo anayosema huyo rais "maisha bora kwa kila Mtz". Judgement day is coming.

    ReplyDelete
  24. ukimaliza hiyo vekesheni mstue mista president akatembelee kule Darfur tuone napo kukoje!

    ReplyDelete
  25. Anonym. wa 5.22AM, nakuunga mkono kwa 101% ulonena. Wanamipango miji wa kwetu kutwa nzima wanawaza ufisadi, sio wabunifu hatakidogo. Naona ukilinganisha wanamipango miji wa huko (Khatum) na wa kwetu ambao wamekulia na kusomeshwa ndani ya nchi ya amani,hata hiyo F 2. umewapendelea. Ni wababaishaji kinoma, wao kuwaza kuuza viwanja mara mbili mbili, hapo aaakh, wanazodegeree haswa!!
    Mimi naona serikali inahaja ya kulibebea bango suala la wana mipango miji wetu, yaani bado mawazo yao yapo miongo saba ilopita.
    Ah, inakera ndugu zanguni.

    ReplyDelete
  26. MICHUZI, MKONO WA KUUME NDIYO MKONO WA KULIA....AU MWENZETU MIKONO YAKO YOTE YA KULIA? KIINGEREZA NINGEKUELEWA, HATA KISWAHILI PIA? MH..

    ReplyDelete
  27. mkono wa kulia ni wapi?ki-kwako uvosimama ktk picha au sie watazamaji tuonavo??
    afu mkono wa kulia na kuume...sijaelewa apa..nijuavo ni sehemu moja
    ebu mnieleweshe

    ReplyDelete
  28. Mbona huko city center magorofa yanahesabika???? yaani hata mwanza inaifunika khartoum LOL

    ...ila kwenye usafi nawapa big up hao janjaweed

    ReplyDelete
  29. Kakaz...........Fulana Isi the mosti travelled fulanaz in the Worldi............Cozi of thati i wanti to buyi iti fromi you kama memorabilia..........Naomba offeri yako?????????????????????

    ramadhan Karim.........

    ReplyDelete
  30. Wow asante kwa kutuelimisha. mimi nikisikia sudani nakumbukia tu zile picha za njaa na vita tu .Kumbe kuzuri hivyo na kusafi hivyo.Hata kama wanasehemu zilizomasikini kama kwetu lakini jiji lao lisafi bwana.

    Achana na waosha vichwa hapo juu...fulana yako...vacation yako...watu wanaona donge hawawezi kutalii kama wewe at kama sio JK asingepanda ndege...so what.....Wivu umewajaa sana tu ....

    ReplyDelete
  31. Unaesema city centre maghorofa hakuna hujui ulisemalo wenzako wana mipango miji.weye unataka paonekane kama huko kwenu hata parking ni issue??kama kariakoo??tembea ujionee sio kukaa hapo bongo ndo ukafikiri miji yote iko hivyo,hovyoooooooooooooo.
    cha chandu - uk

    ReplyDelete
  32. HII NDO FAIDA YA KUWA MWANACHAMA WA OIC KIKWETE AKISAFIRI LAZIMA ASAFIRI NA MICHUZI MWISILAMU MWENZIE,WANAFUNZI WALIOKUTANA NAO SUDAN WOTE NANIHII NAFIKIRI WALIKWENDA KUFUTURU NA JK.
    INASIKITISHA MH.MKUU WA WILAYA YA NANI HII NDUGUYO HANA SERA.UKIPENDA POST HII AU ACHA.

    ReplyDelete
  33. HIVI MICHUZI HUNA FULANA NYINGINE ?? MBONA KILA SIKU HIYOHIYO ??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...