













Mmoja wa waratibu wa kinyang’anyiro hicho Judy Felician amesema kuwa walimbwende hao 13 wataingia kambi mwezi ujao pamoja na washindi wengine kutoka nchini za Kenya Uganda, Rwanda na Burundi kupata washindi wanne ambao watakwenda kushiriki kwenye shindano jingine la uanamitindo nchini Ugiriki.
Judy amesema nchi za Kenya Uganda, Rwanda na Burundi zitatoa walimbwende watatu kila moja ambao wataungana kambini na walimbwende 13 wa hapa nchini katika kambi ambayo itaanza Oktoba 25 jijini Dar.
Walimbwende 13 waliofuzu kutinga fainali ni Rihama Mohamed, Gloria Emson, Namrata Mandania, Nshoma Mkwabi, Sarah Kazaura, Cynthia Kimasha na Beatrice Wilbard.
Wengine ni Nelly Kamwelu, Doris Godfrey, Evanuru Isaack, Joyce Mbago na Irene Shirima .
Baadhi ya vigezo vilivyotumika kuwapata washiriki hao ni binti kuwa na umri kati ya miaka 18 hadi 22 na urefu wa sentimita 170-175, kifua cha upana wa sentimita 60.
Kwa mujibu wa Judy walimbwende hao 13 waliofuzu kutinga hatua ya fainali zitakazofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubileee jijini Dar walipatikana katika michakato miwili tofauti iliyofanyika Agosti 30 na Septemba 20 na kuhusisha walimbwende kutoka shemu mbalimbali za Tanzania .
Aidha mratibu huyo amesema katika fainali hizo walimbwende wanne watakaoshika nafasi nne za juu watapelekwa nchini Ugiriki na kampuni ya G-Cat ya Uingereza kushiriki katika kinyang’anyiro kingine ambacho kitawakutanisha na wanamitindo wengine kutoka ulaya.
Judy amesema wakiwa Ugiriki wanamitindo hao watachuana kuwania kupata mkataba wa mwaka mmoja kuonyesha mavazi kwa mwaka mzima huko ulaya.
Akizungumzia mustakabali wa walimbwende ambao watashindwa kufuzu kwenda huko juu Judy amesema watakuwa wakitumika katika shughuli mbalimbali za matangazo na masuala mbalimbali ya mitindo hapa nchini.
Shindano hilo linalenga kuwawezesha wanawake na kauli mbiu yake inasema ‘Wasichana wajihadhari na ujauzito katika umri mdogo, umalaya na utumiaji wa dawa za kulevya na Ukimwi’.
Kwanza kabisa nawapongeza ma-model hao wote kwa hatua waliyofikia. Ila sasa hao watatu walioanza hapo juu kidigooooooooooooo. Sijui hiyo wamepoziiiiiiiiiiiiiii
ReplyDeleteHivi bongo strobist doesnt exist?
ReplyDeleteThe first three Not good at all, mapoz mabaya sana, i wonder who took the picture and edit.
ReplyDelete#4__Sawa lakini huo ushanga sasa ndio unautangaza au tujue vipi?
#5__Kasheshe utazani mwanaume au transgender.
#6___Okay lakini umesimama kama unataka kujambo.
#7___Goog
#8___God knows huo makanda sasa unataka kuuvuta wa nini , umeharibu Poz na nywele simestailiwa vibaya
#___9Good
#10___Okay
#11_ Safi
#12_Fine
#13_Poz la kawaida hilo sio la kimoda kabisa
We COuld DO Better on the POZIIII
anon 26, 2008 10: 49
ReplyDeleteacha umbea na wala huna unalojua.
watu kujifanya wanajua kumbe hawana wanalojua.
tupe basi website yako uliyopiga watu picha wakapendeza.
mnaboa sana watu kama nyie.
msonyoooo