Meneja Msaidizi wa Duka la Zain Bi. Veronica Madata akimkabidhi simu ya kisasa ya Blackberry jijini Dar jana , Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Cossiga, Bw. Francis Mapunda aliyeshinda katika promosheni ya Endesha Ndoto kwa kufikisha pointi 9,721. Ili kushiriki prmosheni hiyo, mteja wa Zain anapaswa kutuma sms ya neno ndoto kwenda 100, na kila anapozungumza anajisogeza karibu na Ndoto pointi.

Dar es Salaam, Septemba 3, 2008
ZAIN, kampuni ya simu za mkononi inayotoa huduma katika nchi 22 barani Afrika na Mashariki ya Kati, imekabidhi zawadi anuwai kwa washindi wa 137 wa promosheni ya Ndoto Points inayoendeshwa na kampuni hiyo.

Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania, Beatrice Singano alisema Dar es Salaam jana kuwa mpaka sasa wamekwishatoa zawadi anuwai zikiwamo simu mpya aina ya Nokia na ya kisasa aina ya Blackberry, kwa wateja wao wa Dar es Salaam na mikoa mingine Tanzania kwa kushinda promosheni ya Ndoto Points.
Ndoto Points ni mwendelezo wa promosheni ya Endesha Ndoto Yako 2 ya Zain, ambayo zawadi kubwa inayotolewa ni gari aina ya Toyota RAV 4 na Toyota Land Cruiser ambayo mshindi wake atajulikana Desemba, mwaka huu.
Promosheni ya Endesha Ndoto ni sehemu ya programu endelevu ya Zain Tanzania.
“Lengo letu ni kuboresha maisha ya wateja wetu na kuwafanya waishi kwa raha zaidi kwa kuzingatia kauli mbiu yetu ya A Wonderful World (Ulimwengu Maridhawa),” alisema Beatrice.

Mpaka sasa droo ya Endesha Ndoto Yako 2 ya Zain imekwishawawezesha watu watano kuibuka washindi wa magari aina ya Toyota RAV 4.
Mshindi wa kwanza alitoka Dar es Salaam, wa pili alitoka mkoani Mbeya, wa tatu Iringa, wa nne Pwani na wa tano Tanga. Mshindi wa sita anatoka Dar es Salaam na anatarajiwa kukabidhiwa gari hivi karibuni.

Francis Mapunda, mfanyabiashara mkazi wa Dar es Salaam ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya ujenzi wa barabara ya Cossiga, aliyeshinda zawadi ya Blackberry, alikabidhiwa simu hiyo ofisi za makao makuu ya Zain, Dar es Salaam juzi, na akasema hakuwa na ndoto kama kuna siku angeshinda Blackberry.
"Ninashukuru Zain kwa kuwajali wateja wake, na ninafurahia kupata simu ya Blackberry itakayoniwezesha kupata mawasiliano kwa urahisi zaidi," alisema Mapunda aliyeshinda baada ya kufikisha pointi 9,721.
Mteja wa Zain akifikisha pointi 9,001 na kuendelea anajishindia Blackberry ya bure.

Mshindi mwingine wa Blackberry, John Mapigano, ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Mwanza alisema tangu apate Blackberry shughuli zake zimekuwa zikifanyika vizuri zaidi.

Wenceslaus Vincent, pia mkazi wa Dar es Salaam ambaye pia alishinda Blackberry alisema anajiona yuko kwenye Ulimwengu Maridhawa kwa kushinda Blackberry inayomwezesha kupata huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na intaneti.

Ili kushiriki promosheni ya Endesha Ndaoto 2, mteja anapaswa kutuma sms ya neno ndoto kwenda nambari 100 na atakuwa ameingia rasmi kwenye promosheni hiyo.

Mbali ya zawadi ya magari, Zain pia inatoa zawadi nyingine anuwai kupitia Ndoto Pointi. Kila mara mteja wa Zain anapozungumza anajisogeza karibu na Ndoto Pointi. Kwa kila Tsh 500 anayozungumza anajipatia ndoto pointi moja.
“Mteja akifika kati ya Ndoto Pointi 1,000 hadi 3,000 anajishindia kufurushi cha zawadi kutoka Zain, akifika Ndoto Pointi 3,001 hadi 5,000, anajishindia simu mpya aina ya Nokia 1110i.
Mteja akifika pointi 5,001 hadi 7,001 anajishindia simu aina ya Nokia 1650 wakati pointi 7,001 hadi 9,000 anajinyakulia Nokia 5310 au Ipod.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Inaelekea huko bongo Rav4 ndilo gari(s.u.v) linalotamba/kutanulia,liko affordable,maana naona kila anashinda ujinga fulani anapewa Rav4.Hawa watowaji Zawadi wanabidi wa upgrade their game sio kila siku.Au imekuwa kama katikati na mwishoni mwa NINETY(ies)ambapo kila mshindi wa kuonyesha nyuchi alikuwa anapewa MARK MBILI?

    ReplyDelete
  2. Mh! Veronica upo juu,si mchezooo,still looking good.

    ReplyDelete
  3. Veronica mambo yako supa nakuaminia dear,, miss u so much

    ReplyDelete
  4. Looking good those days unakuala sinza kijiweni kwa mzee chaulembo daaa wish yajirudie hayo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...