ZAIN, kampuni ya simu za mkononi yenye mtandao katika nchi 22 barani Afrika na Mashariki ya Kati, imeendeleza programu yake ya kufuturisha watoto yatima wa kituo cha Abu-Abdulrahman jijini Tanga mwishoni mwa wiki.
Kwa mujibu wa Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe, hatua hiyo ya kufuturisha watoto wasiojiweza, ni programu iliyopangwa kuendelezwa na Zain katika kipindi cha mfungo wa Ramadhani.
Mbali ya kuwafuturisha, pia Zain ilitoa zawadi ya vyandarua kwa watoto wa kituo hicho cha Abu-Abdulrahman kilichopo chini ya taasisi ya Answar Muslim Youth Centre yenye maskani yake eneo la Makorola, Tanga.
Akizungumza na watoto hao wapatao 104 baada ya kuwafuturisha, Tunu alisema hiyo inadhihirisha Zain inavyowajali wasiojiweza, na akasema kampuni hiyo itaendelea kusaidia miradi mbalimbali ya jamii.
Mbali ya Tunu, pia Zain iliwakilishwa na Meneja wa Zain Kanda ya Kaskazini, Kizito Millambo, Mratibu Maendeleo ya Biashara wa Zain Tanga, Karugaba Rugaimukamu na Mhandisi wa Mitambo wa Zain Tanga, Abdallah Abdallah.
Akizungumza baada ya kufuturishwa watoto hao, Mlezi wa Abu-Abdulrahman Orphan Centre, Hassan Waziri aliishukuru Zain na kusema imefanya jambo linalompendeza Mungu, kitu ambacho kinasababisha kampuni hiyo izidi kufanikiwa siku hadi siku.
Waziri alisema kituo hicho hivi sasa kinalea watoto zaidi ya 100 wanaosoma chekechea, shule za msingi, sekondari na vyuo, wakiwamo wasichana na wavulana.
Mimi naunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na watu binafsi, makampuni, walimbwende na hata viongozi, za kuwatembelea watoto yatima mara-kwa-mara, wakati wa sikukuu na nyakati nyinginezo.
ReplyDeleteMungu akinijaalia nami pia nitakaporudi nyumbani nitajitahi cho chote nitakachokuwa nacho.
HOJA: Hata hivyo sidhani kama ni vizuri kila anayekwenda huko anataka kuwapiga picha akiwa anawalisha. Hasa hao wadogo wadogo.
Sidhani kama wangekuwa na uwezo wa kutumia ridhaa yao wenyewe wangekubali, kuambiwa "Haya jitayarishe fungua kinywa wakati mimi nashikilia chakula." Sidhani kama wangekubali.
Kwa sababu wao wako kwenye shida na kwa kweli wanahitaji siyo tu vile wanavyopelekewa bali na upendo pia.
Inawezekana naliangalia hili jambo katika mtizamo tofauti kidogo na wanzangu.
OMBI: Msiwashurutishe kuwapiga picha kwa kupozi kama mnawalisha.
Pia msitumie watoto yatima kutangazia biashara zenu. Liangalieni hili jambo kwa undani kidogo.
TAHADHALI; Maoni yangu yasieleweke kuwa msiwasaidie. HAPANA SI-MAANISHI HIVYO.
Nadhani hata miongozo ya dini inasema Unapotoa sadaka kwa mkono wakulia, jitahidi hata wa kushoto usijue.
Siyo lazima kila mtu anapokwenda kusaidia watoto.. WATOTO...jamani hao ni WATOTO YATIMA, tusialike vyombo vya habari ya "KU-pozi" nao kwenye picha.
Sijui Wenzangu hili mnalionaje.
Balozi wa Zain tafadhali usinitie kapuni.
Mdau, ughaibuni.
Brother Michuzi, asalaam aleikum.
ReplyDeletehebu naomba uniibie ndogondogo za bibie Tunu Kavishe maana ana mvuto na ni full package ya ndoa.naomba full data maana anataka kunifanya niwe zuzu kurudia rudia picha.
Mdau wa London
MashAllah, binti kajaaliwa umbo, sura, na roho njema....mola amzidishie. Will you mary me, Tunu?
ReplyDeleteTunu Kavishe Ingelikuwa ni jambo la busara kama ungevaa kama hao unaowahudumia katika kuwahudumia angalau kwenye mfungo huu wa mwezi wa Ramadhani!!!!!!!
ReplyDeleteNaungana na mdau wa kwanza, ni kweli si vizuri kuwatumia yatima na wanyonge wengine kujipatia umaarufu. Kuwasaidia ni wajibu wetu lakini msaada wa kweli ni ule ambao ukitoa kwa mkono wa kulia, mkono wa kushoto haujui.
ReplyDeleteKuhusu huyo dada ni kweli bomba ila kwenye hafla kama za futari hatuvai jeans iliyobana kama hiyo. Ni vizuri akachagua mavuzi kutokana na tukio.
Ama kweli..... cheo kimepata mtu!
ReplyDeleteAnko Muhidin,wewe wanifurahisha sana.Blog yako inakuwa 'sponsored' na 'Naniliii',wakati huo huo wewe ni balozi wa 'naniliii'.Huoni kwamba unaweza kuleta ugomvi hapo wa kibiashara?Mungu akuzidishie michu,huna ubaya na mtu.
ReplyDeletehahahaaa teh teh ila wadau mmenivunja mbavu,,
ReplyDeletedada jeans mbano,ramadhan,islam,futari,mavazi ya ao watoto,cheo chako,mahali ulipo,blogu hii,ze balozi wa zain-michu,,,hataaaari tupu no kulandana kbs
ila nyie midume kwa uchu???lzm mfe
Aaakh, mashallwah, ntotongwa tunu jamani, ntoto kaumbika huyo!!! Afu anaroho nzuri wajameni. Mwacheni muumba aitwe muumba.
ReplyDeleteMichuzi, ukisikia swaumu ina swii na mtu anapata swawabu ndiyo hii sasa, sio unafuturisha vigogo kiunafiki hapa.wale wenye nacho huongezewa wanapowakumbuka wasio nacho.
ReplyDeleteMbega
da!kweli nimekubali TUNU full package Uzuri + Ubinadamu=Mke.
ReplyDeleteMademu wachache wenye moyo kama wake,mungu akujalie dada.Mwingine asingekula nao sahani moja angeleta usister duh,hasa nyie wa ughaibuni.
Anon wa 12:33 AM..... Nani alikwambia kuwa Tunu alikula nao sahani moja? Hapo alitegesha mkono wake kusubiria picha tu. Tunu ni sister duh na sisi ndio tunao mjua.
ReplyDeleteHabari Ndo' Hio.
hAYA NI MATUSI...HAMNA ZAIDI SELF PROMOTION NA MAMABO YA DINI KUINGILIWA NA WATU WASIELEWEKA
ReplyDeleteHIVI MWEZI MTUKUFYU WOTE HUU KASHINDWA KUVAA NGUO YENYE NIDHAMU? KWANI KULIKUWA NA ULAZIMA GANI KUVAA SURUALI YA KUTUBATHWILISHA SWAUMU ZETU?
-bugurunikwamnyamani
NYIE NADHANI HAMJAMWELEWA HUYU SISTER DUH TUNU. KUNA PICHA ZAKE ZILITOLEWA KWENYE HII GLOBU YA MICHUZI AKIWA IRINGA NA WATU WAKA-COMMENT KUWA HAJUI KUVAA..... NADHANI WOTE MNAKUMBUKA. NDIO MAANA SASA HIVI AMEAMUA ATOKE NA KI-TIGHT JEANS ILI MJUE NA YEYE YUPO YUPO.
ReplyDeletehata kama mnasema hajui kuvaa lakini package inamlinda vyovyote atavyovaa minamuona yuko bomba,wengine ndo inabidi muwe makini.
ReplyDeleteDada uko bomba usisikilize wazushi.