Ndio Kaka.

Natumai u-mwema na mfungo waendelea vema baada ya "vekesheni ya kikazi" ya Sudan.


Haya Kaka, turejee kwenye taswira. Majuzi nilitembelea Austin Texas nikaenda iliko CAPITOL yao na nikapata picha hiyo ya usiku kwa nje, kisha kesho yake nikaenda na kupata picha ya "dungu" lililo juu kutoka kwenye ground yake (nili-offset kidogo kupata shape yake), kisha nikaendelea kusimama hapohapo nilipopata picha ya dungu nikamuomba mtu aende juuu apate picha yangu.


Ni kwema na kunapendeza, Ofisi za Senate na House of Representatives, duka la zawadi na pia mtu wa kueleza kila kitu kuhusu utawala mzima wa Texas na picha za magavana wote waliopata kuongoza jimbo hilo kubwa hapa nchini.

Enjoy ka-zawadi ka mfungo hako Kaka
Mdau
----------------------------------------------------
Mdau!
asante sana kwa zawadi hizi njema za mfungo. zimetulia kaka. hasa hiyo ya nje, usiku. ila nxt taim jaribu kukweka kaukuta hako ka chini kulia, kanaharibu pozi.
hata hivyo nakushukuru kwa kuendeleza libeneke. pia naendelea kukaribisha picha na mijadala ya picha kwa wagonjwa wa snepu wenzetu wote.
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. WE SHANGAA TU KWA WATU UTAWEKWA NDANI!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...