Jumamosi hii jiji la Atlanta litawaka moto pale lile gwiji la bongoflava linalondelea kutesa hapa USA, ALI KIBA atakapo uwasha moto hapa ATL.
La hasha si hayo tu kwani kabla ya ALI KIBA kuwarusha rusha watu katika show hiyo itakayofanyika katika ukumbi wa TRAVEL LODGE uliopo Marietta pia siku hiyo kutakuwa na soka tournerment ambayo itajumuisha timu mbali mbali ikiwemo ile timu maarufu ya Tanzanite FC ambayo itakuwa inaikaribisha timu ya Bongo United toka washington DC.
Baada ya mtanange huo utakaofanyika
Maddox Park Atlanta
(1142 Bankhead Ave. Nw, Atlanta).
Nyamachoma na vinywaji baridi vitakuwepo.
Njoo ujumuike na wana Afrika Mashariki wenzako!
See you there!
Mdau Hadjihelper

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Jamani Ali akiba nazipenda sana nyimbo zake na huu wimbo huu wa Cinderella.Nakutakia kila la heri ali kiba

    ReplyDelete
  2. Shaka au Michuzi, tunaomba email yenu ya Shaka Entertainment ili tuwasialiane.

    ReplyDelete
  3. Oya lini unarudi home au ndio umezamia aaa

    ReplyDelete
  4. JAMANI ALI KIBA VISA YAKE BADO IKO VALID? ISIJE IKAWA TABU BAADAYE. OOH! NA MUMPE PESA YAKE AKIRUDI NYUMBANI SIO MUMTUMIE KWA FAIDA ZENU. MESSAGE SENT...

    ReplyDelete
  5. Jamani mbona hili onyesho la Atl linabadilishwa tarehe kila siku? Nilifikiri ni wk end ya Thanx giving, duh! itabidi nilikose onyesho lake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...