rais wa miss tourism world organisation john singh (kati) akipeana mikono na mh. aloyscious gonzaga mandago huku isaack kassanga akionesha mkataba ambao kampuni ya easy finance ambayo wao ni wakurugenzi imeingia na hiyo taasisi inayoendesha mashindano ya urembo ya utalii duniani. sherehe hii ilifanyika katika ofisi za easy finance iliyoko kinondoni, dar.

kwa mujibu wa makubaliano hayo, easy finance, ambayo pia ni mmoja wa wafadhili wakuu wa globu hii ya jamii, sasa itakuwa msimamizi wa mashindano ya miss tourism kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia januari 2009.
pia itasimamia na kuendesha, kupitia taasisi ingine ya nyumbani, mashindano ya miss tourism ya bongo. hal kadhalika itaandaa fainali za dunia za mashindano hapa bongo mwakani ambapo zaidi ya nchi 70 zitashiriki.

hii ina maana kwamba taasisi iliyokuwa ikiongozwa na gideon chipungahelo kwa miaka sita iliyopita haitohusika tena na uandaaji wa miss tourism hapa nyumbani.

habari zinasema taasisi mpya itayochukua nafasi ya ile ya chipungahelo imeshaanzishwa na easy finance na mambo yakienda mswano miss tanzania 1994 wa pili lucy ngongoseke kihwele ndiye atakayekuwa anaiongoza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mmh, hayo mambo? hela hizo ni sadaka? Gonzaga mbona umebadilika hivyo? na wewe ni milionea?

    ReplyDelete
  2. hee ni lazima atoe sadaka haiumi alizikomba pale atandad chatad mwiziiiii....!!!!!

    ReplyDelete
  3. Kuna kitu mimi kama mwanadamu nachukia sana tena sana wivu,ubinafsi na chuki.hivi kama watu walikwapua lakini wao wanafaidika na jamii inafaidika wewe inakukera nini kwasababu kuna watu wengine zinaishia mifukoni na matumboni mwao hiyo tumeona mifano mingi sana mimi binafsi sioni kosa walilofanya hao jamaa kwanza sijui ukweli wake maana ukweli wanaujua wenyewe kwahiyo kumwita mtu mwizi wakati unauwakika nikosa kubwa sana halafu hela imerudi nyumbani mlitaishie kwa wakoloni tu mbona watanzania mnakuwa hamtaki maendeleo hiyo kampuni it will never fall kwasababu hao makaka zetu wamesogeza kitu kidogo.nawatakia mafanikio mema na maendeleo mema.wacheni majungu wandugu tafuteni maendeleo mbona upatikanaji wa hela upo mwingi tu

    BIG UP tunashukuru sana kwa kudhamini blog yetu ya jamii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...