Mwanamuziki Alikiba athibitisha umahiri wake huko Wichita Kansas jumamosi iliyopita baada ya kufanya show ya masaa mawili iliyokidhi kiu ya mashabiki wake waliofurika kwa wingi kumuona.

Kwa wale wote waliofanikiwa kushuhudia njonjo zake jukwaani, hakuna asiyekubali ya kwamba, Alikiba is one of the best performers from East Africa Period.


Kama bado hujapata fursa ya kumuona hakikisha shows zake zilizobakia hazikukosi ili na wewe ushuhudie na ukubali umahiri wa mwanamuziki wetu huyu kutoka Nyumbani.


OCTOBER 4- NYATI LOUNGE JERSEY CITY N.J. (East Africans wote wa Philly, New york na up north mnakaribishwa)

OCTOBER 11- JAZZ NICKS CLUB- ESSEX, MD. (BALTIMORE)

OCTOBER 18 KANSAS CITY,KS. (Covering the midwest area)

OCTOBER 24 HOUSTON, TX (it's definetly going down)

OCTOBER 25 ATLANTA, GANOVEMBER 01 BOSTON, MA


Kwa maelezo zaidi ingia
alikibausa.com
aksanteni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. free TID? kama mtu amekosea lazima atumikie adhabu iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama hizo..

    ReplyDelete
  2. wanakupa ushauri mbaya'FREE TID'campaign,achana na mambo hayo

    ReplyDelete
  3. Wewe Ali Kiba najua unafanya show nzuri na nakufagilia, ila kama unaona aliyofanya TID ni mazuri kwa jamii basi nitakuona hauna maana.
    Sheria lazima itumike kwa kila mtu hata kama ni celeb.
    sio kwamba kwasababu TID ni celeb ndio afanye mambo yakipuuzi.

    Hata huko marekani ukifanya mambo ya kipuuzi pamoja na u celeb wako unawekwa ndani.

    Kwahi Ali Kiba sijui kilichokushawishi uvaa hio T-shirt ni kwa sababu gani.
    Najua bado ni kijana mdogo na watu wengi watakutumia kwa udogo wako lakini nawewe uwe unafunguka macho na kufikiria kwamba unakua, usitumiwe kihovyo hovyo. kama ule mfano wa kufanya show mwezi wa ramadhan.

    ReplyDelete
  4. Hebu wacheni comment za ajabu kumtisha Ali! Kuna mabazazi wangapi hapo Tz wanafanya mambo ya ajabu na bado wanatembea uraiani? Wafungeni hao mafisadi kwanza. Ovyooooooooooooo!

    ReplyDelete
  5. free TID? kampeni nyengine bwana! nani atawasikiliza? mimi huwa nacheka sana pale mtu anapokuja na ujanja wa kutengeneza pesa za haraka na akawapata watu mbumbu wa kununua anachokiuza. Naamini hata huyo TID hanufaiki na mauzo ya t-shirt hizo seuze kunufaika na kampeni.

    ReplyDelete
  6. hivi TID kafungwa?kafanya nini kwani?

    ReplyDelete
  7. Haya mfungo wa Ramadhan umekwisha,Kijana sasa unaruhusiwa kufanya maovu yooooooooooooooote utakayo.mmmmh.

    ReplyDelete
  8. MIMI NADHANI MNALIANGALIA JUUJUU TU SUALA LA T.I.D. NA KABLA SIJAENDELEA,NAMWUNGA MKONO ALIKIBA.
    "FREE T.I.D" IS A CALL, IT IS A CRY FOR JUSTICE, IT IS BASED ON SOMETHING FISHY THAT HAPPENED DURING TID'S TRIAL.
    THE JUDGE CONDEMNED TID TO PRISON WITHOUT AN OPPORTUNITY FOR FINE!
    YOU DONT NEED TO BE A ROCKET SCIENTIST TO KNOW THAT THE RULING WAS INFLUENCED BY CORRUPTION.
    "FREE TID"....WAY TO GO!
    Mdau
    Japan

    ReplyDelete
  9. NOTHING WRONG WITH ALI KIBA AND FREE TID. Kama angekuwa mtu wako wa karibu,ndg au rafiki, ungeunga mkono pia. so AK, dont worry pipo will TALK ANYWAY----Mimi nasema Free huyo Jamaa aje atupe Burudani ya Muziki, because the guy is GUD.

    ReplyDelete
  10. Kwani jamani wat hapnd???!!!eti kaka michuzi,tuelezee basi sio wote ambao tunajua

    ReplyDelete
  11. Michuzi umebana comment yangu hapo itoe bwana maana watu wanamfikiria vibaya TID wa watu acha wajue ukweli bwana........

    Mdau kino Klein

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...