Na Irene Bwire, Nambia
BANDARI ya Dar es Salaam iko hatarini kupoteza wateja wa nchi zisizo na bandari kama haitamaliza tatizo la msongamano wa mizigo bandarini.
Hayo yamebainika jana wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipotembelea Mamlaka ya Bandari Namibia (NAMPORT) katika bandari ya Walvis Bay iliyopo Namibia na kuelezwa mpango wa bandari hiyo kuhudumia nchi zote za SADC ifikapo mwaka 2015.
Meneja Mauzo wa bandari hiyo, Bw. Elias Mwenyo alimweleza Waziri Mkuu kwamba mamlaka hiyo ya bandari iliyoanzishwa mwaka 1994 imepata hadhi ya kimataifa na kuweza kutoa huduma kwa nchi za Amerika Kusini, Amerika Kaskazini, Afrika Magharibi, Ulaya na Asia.
Alisema mwanzoni bandari hiyo ilikuwa ni uchochoro tu wa kuupitisha bidhaa lakini sasa inahudumia nchi za Zambia, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Botswana, na Zimbabwe ambazo hazina bandari.
“Urahisi wa mawasiliano ya barabara, reli na ndege kwenda nchi za SADC umetuwezesha kuhudumia nchi hizo tunakatisha jangwa la Kalahari badala ya kwenda Durban au Capetown, Afrika Kusini na hivyo kuokoa siku saba hadi 11 za mizigo kukaa njiani,” alisema.
Alipoulizwa na Waziri Mkuu Pinda ni muda gani meli zinatumia kukaa majini tangu zinapofika hadi kutia nanga bandarini hapo, Bw. Mwenyo alisema hakuna meli zinazokawizwa kwa sababu wanapopewa notisi ya saa 72 kabla meli haijafika maeneo ya kwao wanaanza maandalizi ya kuipokea na hivyo kuwa tayari kuzihudumia pindi tu zinapofika.
Alisema bandari hiyo ambayo haijawahi kupoteza mzigo hata mmoja ina uwezo wa kuhudumia tani milioni nne za mizigo kwa mwaka na uwezo wa kupokea meli za mizigo 350 kwa mwezi. Pia ina vitengo vya kukarabati meli zinapoharibika tofauti na zamani zilipokuwa zikilazimika kupelekwa Cape Town, Afrika Kusini.
Taarifa hizi zimekuja wakati Rais Jakaya Kikwete amemwagiza Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa ampe jibu la siku kamili za mtu kusubiri mzigo bandarini na kumtaka apunguze siku hizo kutoka siku 23 za sasa hadi 10.
Taarifa ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ambayo alisomewa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga Septemba 24, mwaka huu, inasema bandari za mwambao ambazo ni Dar es Salaam, Tanga na Mtwara zina uwezo wa kuhudumia tani milioni 11 kwa mwaka lakini katika mwaka 2007/8 ziliweza kuhudumia tani milioni 6.2 ambayo ni sawa na asilimia 58 ya uwezo wa bandari.
“Shehena ya kontena katika kipindi hiki ilikuwa makontena 325,000 ambayo ni asilimia 30 juu ya uwezo wa kitengo [WINDOWS-1252?]hicho,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Waziri Mkuu kesho (Ijumaa) atakutana na Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia na baadaye kutembelea mradi wa maji wa Goreangab ulioko eneo la Katutura na mchana anatajiwa kuondoka Namibia kurejea nchini.

mnaona wenzenu wanavyofanya kazi ticts sio nyie kujisifia tu kila wakati sema mnabebwa na wakubwa ndio maana
ReplyDeletewaache waendelee kupiga usingizi tu bandar kama za tanga ,mtwara kwa nini hazipanuliwi kuweza kupunguza huo msongamano wa kijinga wao ni dar tu wakat bandar kama ya mtwara ndio ina kina kirefu,tanga ndio tupu watu wanalala tu wao kaz ni uwizi tu ndio wanaujua tushacoka tushachoka
ReplyDeleteHata mimi ntahama kupitishia mizigo yangu kwenye bandari ya Dar es salaam, wenzao walivyoita bandari salama sijui hawakuelewa maana yake?. Waache walale usingizi yaani mpaka na Watanzania watakapoanza kupitia mizigo yao Kenya, Mozambique (si daraja la umoja litajengwa hivi karibuni) wao ndio wataamka usingizini. Sijui wanataka kitu gani hawa watu kuuchezea mkono unaokulisha! Ngoja kuwe kweupee hakuna wateja, na hiyo mikodi yao, miticts na tabia za kuweka mizigo ya watu muda mrefu ili walipwe pesa za mzigo kukaa humo! Na usumbufu usio na kichwa wala miguu.
ReplyDeleteHalafu utendaji wa kazi mbovu wakiulizwa eti ni shirika la umma si mali yangu, wakikosa mishahara ya kujilipa hawatakawia kuandamana. Ngoja ifilisike halafu tuone kama mtasema kwani mali yangu!
Kiboko yao iko njiani, 'Bandari Lala' inaitwa sasa na si 'Bandari Salama'
Kenya kulivyotokea machafuko ya kisiasa, bandari yao ya mombasa watu waliacha kutumia na kutumia bandari yetu ya dar.Badala ya Tanzania kuteck advantage kwa hilo, lakini badala yake walikuwa wanalalamika eti bandari imefurika mizigo so they cant handle it.Kwa nini Tanga au Mtwara zisitumike kwenye emergency kama hizo.
ReplyDeleteSawa kabisa mimi napenda ifungwe kabisa tujue vitu tunavileta kutoka mombasa kwa sababu mafisadi halisi wamejaa, wanachojua ni kuunda mbinu za ufanisi kwenye rushwa kila siku eti long roooom, umeshasikia wapi duniani siku hizi mizigo inachukua muda, vichwa vyao ni kufikiria kufanya hali iwe ngumu ili wapate rushwa zaidi, waziri kawambwa atapata pata presha ya bure fagia wote anzisha kampuni mpya.Nyingine ni dar airport na border posts.
ReplyDeleteWizi na kazi ni vitu viwili tofauti wao waache wafanye kazi yet sisi tunapata faida kubwa kwani mizigo tukichelewesha storage charge inatutosha
ReplyDeleteVitu vingi baada ya kuboresha mtu anakuja kujiweka katikati sasa hao tics wanafanya nini x=zaidi ya kupeana ulaji tuu
I think our government is forgetting about the fundamentals of economic development. Our port authority just realizes, JUST REALIZE, what competitors are doing, now; Just now? It is a shame, not only to the port authority, but to the government as a whole. It is within our National Security interest to know what other countries are doing economically so as we can compete. One thing they don’t know is, Namibia is just the beginning, this is just one country, there is more to this than they know. I knew what was happening since January of 2008, and they just found out? May be the question is, how did I find out about this? The answer is very simple news; we have to read my fellow Tanzanians. It was on the African Report magazine edition of January – July, 2008. This is what was said;
ReplyDelete“Mozambique’s strategic Central and Northern ports of Beira and Nacala are about to undergo substantial upgrading at a cost of $900 million, according to the transportation minister Paulo Zucula. A tendering process is about to begin, and the project will be partly financed through concessions to modernize and manage the ports. Roads and railways linking the ports to the neighboring landlocked states of Zimbabwe, Zambia and Malawi, will also be upgraded as part of Mozambique’s ambition to be the transport hub for the SADC region. The government’s plan is to rehabilitate the transportation system linking Beira to coal mines and other mineral extraction sites. The anticipated investment is $500 million for Beira and $400 million for Nacala”