Salum Mnuna akifungua shampeni katika sherehe za ushindi wa FC BONGO.Katika sherehe hizo kulikua pia na award ya mchezaji bora wa FC BONGO 2008 ambayo ilinyakuliwa na kijana wa miaka 18 Zakaria Kibona.
Pichani Zakaria mwenye kikombe mkononi na magongo ambae amefanyiwa operesheni ya goti hivi karibuni akipongezwa na Goshashi, na picha ingine wana FC BONGO wakila mduara kwa sanaaaaa na kujidai ile mbaya. ubingwa mtamu jamani, we acha tu!


hongera Fc Bongo, na mwakani mujitahidi mfanye tena.
ReplyDeleteHongereni sana wana FC Bongo kwa ushindi...mwakani jiandaeni tena kusheherekea ushindi mwingine..
ReplyDeleteNaona Bob ndio aliestahili kupata award ya mchezaji bora, kwa kweli bila ya bob isingekuwa rahisi. Zaka ndio mchezaji mzuri sana lakini hakucheza vizuri sana kama bob.
ReplyDeleteZaka amemshinda Bob kwa kura karibu 10, kwahiyo hayo ni maoni yako anon unayemzungumzia Bob. Km kucheza vizuri wachezaji wote walicheza vizuri na kushirikiana. Ila bahati mbaya kikombe cha mshindi kilikua kimoja tu. Wengi wape! Zaka ndo mshindi...
ReplyDeleteSafi hiyoooooo...ila msivimbe vichwa kwa ubingwa huo..hiyo inabidi iwe kama appetizer tu..Gud luck ktk plan zenu.
ReplyDeleteHongereni sana FC Bongo kwa maendeleo mliyoyapata. Jamani nawezaje kuagiza jezi kama zenu? Anayefahamu tafadhali weka info hapa.
ReplyDeleteWatu wa majungu mbona hatuoni maoni yao? au wameshafunyata?
ReplyDeleteNaona mukubwa Goshi,,muzee ya Musoma unawakirisha ufinini.
ReplyDeleteMajungu wamekoma ubishi hapo ,sio mchezo.
ReplyDeleteUnayeomba majungu yakiinjikwa utaweza kuyapika na kuyapakua?
ReplyDeleteJungu namba 1
Prevention Cup ndiyo nini?
Lengo na Madhumuni yake ni nini?
Jungu namba 2
Nani mwandalizi wa Prevention Cup?
Rais wa Prevention Cup ni nani?
Makamu wake unamjua?
Katibu wake unamjua?
Mweka Hazina wake unamjua?
Wajumbe wa Kamati ya uandalizi wa Prevention Cup unawajua?
Je washiriki wa Prevention Cup wanajua?
Jungu namba 3
Nani anayewakilisha timu kwenye vikao vya maandalizi ya Prevention Cup?
Jungu namba 4
Nani mdhamini au wadhamini wa Prevention Cup?
Je washiriki wa Prevention Cup wanajua?
Kiasi gani cha fedha kimapato na matumizi kinatumika kuandaa Prevention Cup?
Je washiriki wa Prevention Cup wanakijua?
Mashindano ya Prevention Cup yana bima/insurance?
Kama yana bima/insurance ni aina gani ya bima yaliyo nayo na kiasi gani mshiriki atakayeumia anastahili kulipwa?
Wachezaji waliopata kuumia kwenye Prevention Cup wamewahi kulipwa bima?
Waandaaji, wasimamizi, marefari na linesmen wanalipwa au wanajitolea?
Kama wanalipwa wanalipwa kiasi gani?
Jungu namba 4
Zaidi ya kikombe na medali kuna tuzo nyingine yoyote ya fedha?
Kama ipo ni kiasi gani na nani anayepewa?
Majungu ndiyo hayo, ukishindwa kuyapika na kuyapakua utadhihirisha kwamba hizi methali za Kiingereza na Kiswahili zinazosema Fools are the tools of wise au Wajinga ndiyo waliwao ni kweli.
wee annon 10.04 ulietoa aya majungu una matatizo unaitaji msaada upesi,,,kwi kwi tih tih thi
ReplyDeleteMAJUNGUUUUUZZZZZZZZZ,
ReplyDeleteUNAYASEMA HAYO MAANA YAKE NINI?, kuwakatatisha tamaa wenzio au?.
Hivi huyu majungu mbona hatumuoni hadharani akiyasema hayo?
ReplyDeleteHaya majungu au facts?
ReplyDeleteAnon 11:43
Wewe unaona haya majungu yana lengo la kukatisha tamaa wengine au?
Anon 11:46
Kwani hapa yaliposemwa majungu haya ni faraghani au hadharani?
SIKILIZENI: Watanzania wenzetu mnaokaa nje ya bongo, tunawapenda sana, kiasi kikubwa kibinafsi mimi huwa nawaona kama wajanja, mmetoka. SASA:tunapoona mnafanya vitu vya kujishoo, misifa, kujifagilia, usanii na uongo mwingi mkiambatanisha na picha kutuonyesha mko sehemu fulani mnatanua, na huku si kweli, kujipachika archievement na success na status ambazo hamna mimi nawaona washamba kinona na mnacheza na maisha.Njooni bongo muone tulivyo fanaya mambo aibu! nyie namkubali ANON aliwapa FACTS ambazo mnaziita majungu hapo juu.
ReplyDeleteNi vile tu post zetu nyingi ANABANA MITHUPU kuzitoa., kwani anaye ana kasumba hiyo hiyo ya misifa.
fala huyo majungu, alijifanya amezimika siku ya fainali tulipochukua kombe kwa kuona aibu. Umati wote wa wabongo ukimsanifu yeye.
ReplyDeleteKaka michuzi naomba nitoe maoni na usiyabanie. Mimi ni mdau ambaye nimesoma maoni yote toka mwanzo hadi. Naomba niseme kwamba huyu majungu siyo fala bali mshamba mshamba fulani. Huku Europe kuna washamba washamba fulani wanachukulia mambo very serious. Halafu kuna watoto wa mjini wao wanachukulia mambo kama funny tu wanakutana wanaenjoy kila mtu anachukua hamsini zake.
ReplyDeleteKwa ushauri tu majungu usichukulie mambo very serious yaani take it easy ndiyo utaenjoy kuwa na watoto wa mjini. Yaani usiwe serious sana na kutaka sana mambo yawe straight forward. Ukiliona jambo kama ni shame, sham au scam unaliignore that way you will make your life happier and make a lot of friends. Ni hayo tu.
Sister fulani Helsinki.