Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata ambaye hivi sasa yuko nchini Afrika ya Kusini ameendelea kupanda chati baada ya kunyakua tangazo katika jarida la True Love.
Flaviana ambaye anaonekana amevaa mavazi mawili tofauti ukurasa wa 73, ameweza kupatamkataba huu.
Akieleza mkataba huu wa kutangaza nguo Flaviana alieleza," Huu ni mkataba mmoja tu, na hivi punde narajia tangazo langu la televisheni pia lianze kuonekana hapa South Africa na bara la Afrika".
Flaviana hakuwa tayari kuzungumzia mkataba wake mwingine hadi itakapoonekana lakini alieleza wazi kuwa hivi sasa anaendelea kupata mialiko mingi ya kazi (casting).
Flaviana Matata aliwakilisha nchi yetu kwa mara ya kwanza katika mashindano ya Miss Universe nchini Mexico ambapo alifanikiwa kushika nafasi ya 6. Hivi sasa yuko nchini Afrika Kusini akifanya kazi ya uanamitindo.
Flag up sista, Mungu akusaidie ...
ReplyDeleteThis is great, hiyo contract ni nzuri na ni ngazi ya kuelekea juu zaidi. I also remember seeing Odemba in True Love enzi zake! Way to go Flaviana, sijui na wewe utabadilisha jina uitwe labda Viana ? kama Happy anaitwa Millen?
ReplyDeletewho are you kidding? why don't you, tell us the real deal? tell us the truth that although you get some auditions, jobs offers have been almost none!!!
ReplyDeleteKila la kheri Flaviani.
ReplyDeleteNaamini safari kwenye fani bado ndefu,hivyo fuata maelekezo ya wabunifu wako au walimu wako nakuhakikisha siku moja unafika mbali zaidi ya hapo.
Hongera sana.
Inawezekana..Go on
Hongera dada
ReplyDeleteMtoto mtanashati, binti wa kiafrika umependeza kichizi! Huyu mrembo ndo amefanya vitu vya maana siyo kama wale wanaobaki kujiuza mjini! Flavian mtoto aminia! Endelea na kazi yako nzuri upeperushe bendera!!!
ReplyDeleteLife is wonderful. Tuwakilishe vizuri sisi watanzania kokote uendako. Mungu akubariki. Be yourself and enjoy life.
ReplyDeleteDada nakukubali sana jinsi ulivyo. ILA tu naona unaelekea kule walipopotea wenzako. 1. Hiyo mikataba nani anakusimamia au ndio bora nitokee kwenye jarida la SA na kupanda ndege? Pili nenda shule sasa ya mitindo na ubunifu ili uweze kufaidika vizuri. Nina maana unaweza kusoma na kufanya kazi pia.
ReplyDeleteWatanzania tunaridhika na vitu vidogo ndio maana hatuendelei. Sasa pongezi nyiingi kwa tangazo moja tu la kutangaza boutique jamani??
ReplyDelete