
THE PAINTING WAS DONE BY THE FIRST HIGH COMMISSIONER OF INDEPENDENT TANGANYIKA IN THE UNITED KINGDOM, AMBASSADOR SAM NTIRO.
THE HAND OVER CEREMONY TOOK PLACE AT MR. MARSHALL'S RESIDENCE IN BATH, UNITED KINGDOM ON THURSDAY, THE 16TH OCTOBER 2008.
MR. KILUMANGA EXPRESSED APPRECIATION FOR THE ARTWORK AND PROMISSED TO DISPLAY THE 'INVALUABLE PIECE OF WORK' AT THE MISSION'S BOARD ROOM FOR EVERYONE TO ADMIRE THE TRUE HISTORIC FRIENDSHIP BETWEEN TANZANIA AND THE UNITED KINGDOM
Ndugu Michuzi, shukrani sana kwa hii taarifa. Marehemu Profesa Sam Ntiro alikuwa maarufu sana katika uwanja wa sanaa, akiwa amewafundisha wengi kule Makerere. Kazi zake ziko sehemu mbali mbali duniani, kuanzia majumbani mwa watu hadi katika taasisi maarufu. Mchango wake katika kuitangaza Tanzania ni mkubwa sana. Unastahili kutafitiwa, kuhifadhiwa na kujulikana miongoni mwa Watanzania. Namkumbuka Profesa Ntiro kwa namna ya pekee kwa vile alinifundisha pale Chuo Kikuu Dar, na pia tulikutana Chuo Kikuu cha Wisconsin, miaka ya mwanzo ya themanini na kitu, alipokuja kwa miezi kadhaa na mimi nikiwa nasoma pale.
ReplyDelete