Na Mwandishi wetu, Mbeya
Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuanza ziara ya siku 10 ya mkoa wa mbeya ambapo anatarajiwa kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya zote saba za mkoa huo wa kusini nyanda za juu.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. John Mwakipesile amewaomba wakazi wa mkoa huu kujitokeza kwa wingi kumpokea JK ambaye anazuru Mbeya kwa mara ya kwanza toka achaguliwe kuwa rais Desemba 2005.
Mr. Mwakipesile ameviambia vyombo vya habari leo kwamba JK atalala katika kila makao makuu ya wilaya katika ziara hiyo, mbali na kukaguia miradi na kuhutubia wananchi
Mr. Mwakipesile ameviambia vyombo vya habari leo kwamba JK atalala katika kila makao makuu ya wilaya katika ziara hiyo, mbali na kukaguia miradi na kuhutubia wananchi
Kwa mujibu wa Mh. Mwakipesile, akishawasili kesho na kuapata ripoti ya mkoa Ikulu ndogo ya Mbeya, ataelekea Mwakaleli katika wilaya ya Rungwe ambako atazi ndua kiwanda kipya cha chai na baadaye atahutubia wananchi.
Amesema siku itayofuata ataelekea Kyela kabla mya kuvuka kuelekea Ileje na Chunya. Okotoba 13 atakagua kituo cha ukulima cha Uyole na baadaye mchana ataweka jiwe la msingi katika Mbeya City Hostels inayojengwa. Kisha ataruka kwenda Tanga kwenye sherehe za kuzima mwenge.
Shughuli zingine za maendeleo atakazozindua ni kuzindua tawi la benki la CRDB la Mbozi, Saccos ya kijiji cha Ilembo pamoja na kukagua hospitali teule ya wilata ya Mbeya huko Ifilisi, sehemu za Mbalizi. Pia atakagua ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe.
Other major functions include inaugurating the Mbozi CRDB Bank, opening the Ilembo Village savings and Credit Cooperative Society(SACCOS) in Mbeya Rural district, inspecting the Mbeya district select hospital at Ifisi in Mbalizi and making a brief inspection of the Songwe International airport currently under construction.
The president will wind up his tour on October 18, this year.
Balozi Michuzi,kuna gazeti moja la kiswahili la kila wiki(Toleo la leo jumatano),limeandika habari fulani siyo nzuri kuhusu hii ziara.Tunaomba ulinzi uimarishwe sana rais wetu asije kupata bugudha yoyote huko Mbeya.Wengine wanasema rais hatulii Ikulu,mimi nasema hapana, huyu jamaa anafanya kazi bwana.Au wadau mnasemaje?(uchokozi)
ReplyDeleteWADAU NAOMBA MAWAZO YENU, KWANINI MAJIMBO AMBAYO CCM INAONA ITASHINDWA KWENYE UCHAGUZI WA UBUNGE POLISI NA TUME YA UCHAGUZI HUWA WANADAI KUWA YANA VURUGU! HII TULIONA WAKATI WA UCHAGUZI TEMEKE CCM DHIDI YA MREMA, AMBAPO RAISI WA WAKATI HUO ALITANGAZA KUWA KUNA VURUGU KUBWA WAKATI HAIKUWA KWELI. MATOKEO YA UCHAGUZI HUO YALITANGAZWA SAA NANE ZA USIKU BAADA YA VUTA NIKUVUTE KUBWA SANA.
ReplyDeleteSafi,kuna wakati niliona maoni katika gazeti fulani kuwa watu wa mbeya wanacomplain kuwa raisi hajawahi kufanya ziara mbeya toka achaguliwe naona sasa watafurahi, kumbe raisi huwa anasoma maoni na kuyafanyia kazi .Keep it Up mr.President
ReplyDeleteJamani mimi ni mkazi wa Mbeya. Matatizo yote ya Mbeya in RC Mwakipesile. Miaka 3 sasa hakuna maendeleo yote ni malmbano ya siasa tu.Rais angefika Mbeya siku nyingi lakini kila akitaka kuja Mwakipesile anamkataza eti Mwandosya ataandaa watu kumzomea!!!
ReplyDeleteZiara hii kuna watu wamehojiwa eti wanataka kuharibu msafara wa Rais kwa kumpiga mawe au kuvuruga msafara!!! Hivi kweli mwandosya na akili zake anaweza kufanya kitu kama hiki? Mbona JK alimpa uwaziri kama hawapendani??Gazeti la Raia mwema limeeleza vizuri kuhusu Mwakipesile.
Tunahitaji maendeleo Mbeya siyo siasa za makundi yasiyo na mwelekeo,Mbeya ni kati ya mikoa inayozarisha chakula kingi na imetoa wasomi wengi katika nchi hii inawapasa kutumia nafasi hiyo ambayo Mungu amewakirimu kuufanya Mkoa wa Mbeya imara Kiuchumi na kuonyesha mfano kwa mikoa mingine.Hizi habari zinzovumishwa na wanasiasa hazitatufikisha mahala popote zaidi tunampa ibilisi nafasi ya kuharibu zaidi.Tunamtakia Rais Jakaya M Kikwete hekima na ukaguzi mwema wa maendeleo awapo Mbeya.Karibu Mbeya,Karibu Kaporogwe uone water fall nzuri na kijani kibichi kizuri,asante GT.
ReplyDelete