Mbeya wapongeza sera sahihi za ubinafsishaji
Na Mwandishi Maalum,
Tukuyu, Rungwe, Mbeya
UMOJA wa Wakulima Wadogo wa Chai wa Rungwe (RSTGA), Wilayani Rungwe, Mkoani Mbeya umeipongeza Serikali kwa kubuni sera sahihi ya ubinafsishaji, yenye maono (vision) na manufaa kwa wananchi wa kawaida.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa RSTGA, Mchungaji Uswege Mwakalinga wakati anawasilisha shughuli za umoja wake kabla ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua Kiwanda cha Chai cha Mwakaleli, Wilayani Rungwe kilichokarabatiwa upya.
Mchungaji Mwakalinga amemwambia Rais Kikwete kwenye eneo la kiwanda hicho katika eneo la Rungwe Mashariki kwenye siku yake ya pili ya ziara ya Mkoa wa Mbeya:
"Tunaishukuru Serikali kwa kubuni sera yake sahihi ya ubinafsishaji, wenye maono ya mbali na wenye maslahi makubwa kwa wananchi wa kawaida. Huko nyumba, baadhi yetu, kama walivyo baadhi ya watu, tulikuwa na maoni kuwa ubinafsishaji ni sera ya ovyo," amesema Mchungaji huyo na kuongeza: "Kumbe tulikosea. Sisi katika RSTGA sasa tunajua fika faida za sera ya ubinafsishaji, sasa tunajua kuwa hii ni sera ya maana sana," amesema Mchungaji Mwakalinga.
Baada ya kuwa amesikia maneno hayo, Rais Kikwete ameingilia kati na kusema: "Ninakushukuru sana, kwa angalau kuisifia sera hii lakini pia kwa kukiri kuwa ni sera sahihi na yenye maono ya mbali,"
Rais Kikwete alikuwa katika eneo hilo la Mwakaleli kufungua kiwanda cha chai cha Mwakaleli ambalo limekarabatiwa rasmi upya kufuatia sekta binafsi kuingia katika uendeshaji wa kiwanda hicho.
RSTGA kinaendesha kiwanda hicho kwa ushirikiano wa ubia wa TATEPA, umoja huo wa wakulima ukiwa unamiliki asilimia 25 na TATEPA ikiwa inamiliki asilimia 75.
Kwa pamoja taasisi hizo mbili zimeunda kampuni ya Wakulima Tea Company Limited ambayo inaendesha kiwanda hicho na kingine cha chai wilayani Rungwe.
Kabla ya kuwasili kufungua kiwanda hicho, Rais Kikwete amepokea taarifa ya utendaji ya Wilaya ya Rungwe katika eneo la Rufingo, ambako amefungua pia jengo la SACCOS la wanachama wa chama cha kukopa na kuweka katika eneo hilo, na pia kuzungumza na wananchi.
Kabla ya kufika Rufingo, Rais amesimama kwa muda katika eneo la Mwanjelwa, nje kidogo ya mji wa Mbeya, ambako amesikiliza kilio cha wananchi kuhusu ajira.
Pia amesimama katika kijiji cha Ntokela ambako ameelezwa shida ya maji na ukosefu wa matuta kwenye barabara inayopita katika kijiji hicho ili kupunguza ajali katika barabara hiyo kuu ya lami kutoka Mbeya mjini kwenda Tukuyu.
Rais pia amelazimika kusimama mara mbili mjini Kiwira kutokana na wingi wa watu, na ameahidi kuangalia upya bei za bati na saruji baada ya wananchi wa eneo hilo kuwa wamemlalamikia kuhusu bei kubwa ya vifaa vya ujenzi.
Pia wamemlalamikia kuhusu pembejeo. Katika eneo la Kimo-Magereza, Rais Kikwete amesikiliza malalamiko ya wananchi kuhusu shida ya maji, shida ambayo imekuwa inarudiwa na wananchi wa Mkoa wa Mbeya tokea kuwasili katika mkoa huo Alhamisi, Oktoba 9, 2008.


JK na Bi Salma jamani wanapenda watoto kha, Utasikia wamemchukua Mungu awabariki
ReplyDeleteJamani pole mama yetu,niliskia ulikuwa unaumwa mafua ukaenda pharmacy huko America,pole sana natumaini unaendelea vizuri.Next time ukienda tena mama chukua mgonjwa mmoja wa Moyo ukamtupe India tu nae manake nao wapate ahueni.Nafkiri utafanyia kazi ushauri wangu shosti au sio?wapo wengi wanahitaji kwenda kutibiwa ila uwezo unasumbua so jaribu kuwakumbuka angalau nawe upate swawabu kwa Mungu.Ni hayo tu Michuzi me sio muosha kinywa ila ulikuwa ni ujumbe kwa shosti wangu na mama yetu.
ReplyDeleteChapa Kazi Kikwqete,ila mimi nina wacwac kama unapata muda wa kutosha kupumzika.
ReplyDeleteWakazi wa wilaya ya Rungwe na Mbeya kwa ujumla tunamshukuru sana JK kwa kufika huko.Ziara inatuondolea vimaneno maneno kuwa watu wa huko hatumpendi JK.JK ni wetu sote na tulimchgua , tena Mbeya kea kura nyingi kuliko wanaojikomba kwake sasa hivi.Sasa hivi washindwe na kulegea!!!
ReplyDeleteVile vile take note Bw.Michuzi hakuna mji wa Rungwe ila wilaya.
Nimesahau ki2 michuzi.Utatu-update mpambano wa Stars na Cape verde.Usisahau.
ReplyDeleteMbeya wamzonga Rais Kikwete kwa kelele za kupinga ufisadi
ReplyDeleteNa Brandy Nelson,Mbeya
RAIS Jakaya Kikwete jana alianza ziara yake ya kwanza mkoani Mbeya tangu aingie Ikulu, kwa maelfu ya watu kusimama barabarani kuuzuia msafara wake huku wakipiga kalele za kumtaka awashughulikie mafisadi kwa madai kuwa, ufisadi ni chanzo cha maisha magumu.
Wananchi hao walitanda barabarani kwenye maeneo ya Mwanjelwa jijini hapa na kuuzuia msafara wake hadi polisi waliposalimu amri na msafara kusimama, lakini ilikuwa kazi ngumu kuwatuliza wananchi hao kwenye eneo hilo la biashara lililo na watu wengi wanaofanya biashara ndogondogo.
Wakati gari la Rais Kikwete likisimama na huku wasaidizi wake wakiandaa taratibu za mkuu huyo wa nchi kuzungumza na wananchi, kelele zilitanda eneo hilo, wengi wao wakipiga kelele kuwalaani mafisadi na tatizo la ajira.
Rais Kikwete alijitokeza kwa kutumia dirisha la juu ya gari na kuanza kuwasalimia wananchi, lakini hakukuwa na masikilizano pamoja na kutumia kipaza sauti kutokana na kelele nyingi zilizokuwa zikipigwa na wananchi hao walioonekana kuwa na jazba.
"Mafisadi!.. ajira... maisha magumu." ni baadhi ya maneno yaliyokuwa yakitolewa na wananchi hao ambao mkoa wao unategemea kilimo cha mpunga, ndizi, kahawa, viazi na chai.
Baada ya kuona hakuna maelewano, Rais Kikwete alimuomba kiongozi wa eneo hilo atoe malalamiko ya wananchi hao na akajitokeza mtu aliyeitwa God Haule, ambaye alijitambulisha kama katibu wa soko.
Katibu huyo alisema kuwa, kilio chao ni pamoja na maisha magumu ambayo alisema yanasababishwa na ufisadi na kwamba, vijana wengi hawana ajira na hivyo kuishi maisha ya shida.
Haule alisema kuwa vijana wengi hawana ajira na kinachowaumiza zaidi ni kuona viongozi ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi, wanaendelea kukaa madarakani bila ya kuwachukulia hatua yoyote.
Pamoja na maelezo ya kiongozi wa wananchi hao, wengi wao wakiwa ni vijana, waliendeleza kelele zao kiasi cha eneo hilo kuonekana kuwa lina vurugu kutokana na kutosikilizana.