Habari ya kazi bwana michuzi?
Hongera kwa blog yako inasaidia kuelimisha na kuhabarisha watu. Tatizo langu ni moja nakerwa sana na shirika la umeme Tanesco.
Kabla hata hawajatangaza mgao wa umeme sisi wakazi wa Kijitonyama mpakani B tunashida ya umeme kwenye fezi moja na unajua nyumba zetu wengi zina fezi moja tu sio tatu.
Kila wanapokata tumekuwa tunawapigia simu wanasema tunashughulikia eti transfoma ya Queen of Sheba imeelemewa. Sasa kama imeelemewa watafute namna ya kurekebisha.
Lakini kwa kipindi hiki cha hivi karibuni wamezidi maana Jumamosi ya tarehe 4 Octoba 2008 walikata umeme wakaturudishia jumapili asubuhi, jumapili usiku wakakata tena wakarudisha usiku huo huo, jumatatu wakakata wakarudisha jumanne asubuhi, jumanne usiku wakakata tena na kurudisha jumatato asubuhi.
Jumatato usiku wakakata eneo kubwa na kurudisha usiku huo huo. Alhamisi usiku wakakata mpaka sasa navyoandika saa mbili ya asubuhi siku ya ijumaa haujarudi.Naomba msaada wa kuelewa.
Hivi kuna mgao wa usiku siku hizi? Maana kwa wiki tumeshalala giza mara tatu. Ninachoelewa walitangaza mgao wa mchana. Usiku ndio tunahitaji sana umeme sababu ya kiusalama na wengine wanajisomea.
Ni mimi mdau mkereketwa.
Mkazi wa kijitonyama Mpakani B.


Pole sana Mdau, suala lako nimelifowadi kwa wahusika ili muweze kushughulikiwa, tatizo linaweza kuwa ni load kubwa na hivyo yawezekana mwahitaji transfoma ya ziada; anyways mimi sio msemaji lakini ni mfanyakazi na nimeshaliwakilisha
ReplyDeleteMambo ya Tanesco kuonea wananchi...kama kawaida!
ReplyDeleteNafuu wapate mpinzani sasa maana wamezidi.
Wewe Bibi Umeme...kwa nini ujumbe wako ufuatiliwa angali mlalamikaji ameshapeleka hoja mara nyingi? Ina maana hawasikilizi wateja?
Public bodies Tanzania zahitaji kunyoshwa adabu.
Michuzi usibane comment!
anonymous nimekuelewa, na new electric act imeshapita na hivyo wapinzani wanaruhusiwa kuja na kuanza kuzalisha na kusambaza bidhaa hii adimu, tayari shirika la Artumas limeanza, na vilevile husomi magazeti, tuna customer care charter ambayo ikishapita inakuonyesha haki zako kama mteja na muda wa issue kufuatiliwa hadi kuwa closed.
ReplyDeletenaomba malalamiko yote myawakilishe info@tanesco.co.tz na kwa sala la kijitonyama, hiyo ni rm.knorth@tanesco.co.tz
wakatabahu
sasa nikuulize swali? Hiyo customer care charter ikishapishwa...na haki yangu isipofuatiliwa...ninaenda kwa nani kulalamika? Mahakama itaweza ku-uphold iyo charter?
ReplyDeleteAu ndo mnaleta yale mambo ya kudanganya watu wasign alafu kumbe huna nguvu yeyote ya kulalamika...tehehe.
Ngojea nikupe mfano:
"7.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (2), Serikali,
vyombo vyake vyote na watu wote au mamlaka yoyote yenye
kutekeleza madaraka ya utawala, madaraka ya kutunga sheria
au madaraka ya utoaji haki, watakuwa na jukumu na wajibu wa
kuzingatia, kutia maanani na kutekeleza masharti yote ya
Sehemu hii ya Sura hii.
(2) Masharti ya Sehemu hii ya Sura hii hayatatiliwa nguvu ya
kisheria na Mahakama yoyote. Mahakama yoyote nchini
haitakuwa na uwezo wa kuamua juu ya suala kama kutenda au
kukosa kutenda jambo kwa mtu au mahakama yoyote, au kama
sheria, au hukumu yoyote,inaambatana na masharti ya
Sehemu hii ya Sura hii."
Hichi ni kipande cha katiba ya Tanzania. Umeona...kudadeki...tehehehe. nadhani hapo utakuwa umepata point yangu...au sio? Yani huna nguvu yoyote ya kulalamika sehemu yoyote serikali isipofuata hayo masharti!
Usikute iyo charter yenu nayo iko ivyo ivyo tu!
Lakini kama mambo ndo hivyo basi ni safi sana...na ni improvement kubwa katika kuleta maendeleo. Safi Sana na Asante kwa kutupa habari.
Mimi sio kwamba nilikuwa nachukia Tanesco...lakini ni kwamba ilifika kipindi mambo hayakuwa kama yatakiwavyo kuendeshwa. Mlileta ubabe na kudhorora kwa service nzima. Na hali ifikiapo hapo...change definitely is needed! (nimeingiza sera kidogo za Obama hapo...tehehe)
Michuzi plz usinibanie
mtoto
Nashukuru sana bibi umeme kwa kulifikisha suala hili kwa wahusika na tulirudishiwa umeme siku ya ijumaa usiku na mpaka leo jumatatu bado upo. Nashukuru wameweza kutatua tatizo. Na siku nyingine nitatumia email ambayo umetupatia.
ReplyDeleteNi mimi mkazi wa k'nyama