Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Utabiri wa kp ni kweli kabisa. Kwa mwenendo wa siasa za kileo kama si za kisanii kibarua cha akina sheikh Yahya Hussein kimeanza kupungua thamani kwa sababu utabiri umerahisishwa.

    ReplyDelete
  2. Nahisi utabiri wa Kipanya utatimia.

    ReplyDelete
  3. EU YATAKA MAFISADI WASHITAKIWE

    2008-10-10 13:34:22
    Na Muhibu Said


    Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), umeitaka serikali iwashitaki mafisadi wanaoiba fedha za umma, ukisema kuwa hatua hiyo ndio njia pekee ya kukomesha ufisadi nchini.

    Akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalum mara baada ya kuzindua maonyesho ya filamu za EU, katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam jana, Kiongozi wa Umoja huo nchini, Jacques Champagne de Labriolle, alisema hawaungi mkono ufisadi kwa vile unakwamisha maendeleo ya nchi.

    ``Tunaunga mkono hatua zinazochukuliwa na serikali katika kukabiliana na ufisadi. Lakini lazima kuwe na ufuatiliaji wa kesi za ufisadi, kwani ufisadi ni wizi wa kuchukua fedha kutoka kwenye eneo la maendeleo na kuweka kwenye mfuko binafsi. Hili hatuliungi mkono kabisa. Lazima tabia hiyo (ufisadi) idhibitiwe na iendelee kukemewa,`` alisema de Labriolle.

    Hata hivyo, de Labriolle, ambaye pia ni Balozi wa Ufaransa nchini, alisema suala hilo anaiachia serikali na mahakama kushughulikia na kuongeza kuwa wataendelea kuunga mkono pale serikali itakapofanya vizuri katika kushughulikia mambo mbalimbali, ikiwamo kukomesha ufisadi.

    ``Ujumbe huu uwe unarudiwa kila wakati, kwani hivi sasa tuko katika karne ya 21, mambo mengi yameshafanyika huko nyuma, hivyo hakuna haja ya kurudi huko. Hivi sasa wananchi wanataka kujua matumizi ya fedha za umma,`` alisema de Labriolle.

    Kauli hiyo imetolewa na EU, kukiwa na mjadala mkubwa nchini unaohusu ufisadi, ukiwamo wa wizi wa Sh. bilioni 133 zilizothibitika kuchotwa na mafisadi kwenye Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

    Agosti 18, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alipokea rasmi ripoti ya uchunguzi wa upotevu wa fedha hizo, aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Timu iliyokuwa inafanya uchunguzi huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Johnson Mwanyika.

    Wengine, wanaounda timu hiyo, ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Dk. Edward Hoseah.

    Agosti 21, mwaka huu, akilihutubia Bunge, Rais Kikwete alisema hadi wakati huo, watu waliochota fedha kwenye EPA, walikuwa wamerejesha zaidi ya Sh. bilioni 60 na akawapa muda hadi kufikia Oktoba 30, mwaka huu wawe wamerejesha fedha hizo, vinginevyo, watafikishwa mahakamani kuanzia Novemba mosi.

    Ufisadi mwingine, unahusu mkataba wa zabuni ya kufua umeme wa dharura kwa gesi megawati 100, uliofanywa kati ya Tanesco na Kampuni hewa ya Richmond ya nchini Marekani.

    Ufisadi huo, ulidhihirika baada ya kampuni hiyo kushindwa kuwasilisha kwa wakati mitambo ya kuzalisha umeme huo.

    Bunge liliunda kamati ya kuchunguza na kuthibitika kwamba zabuni hiyo ilikiuka sheria.

    Sakata hilo ilisababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na kuvunjika kwa Baraza la Mawaziri, Februari mwaka huu.

    Hivi sasa, serikali inaendelea na uchunguzi dhidi ya Dk. Hosea na Mwanyika, kutokana na kuhusishwa kwao na kashfa ya Richmond. Katika mkumbo huo, pia yumo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja na maofisa wengine kadhaa wa Serikali na Tanesco.

    Wakati huo huo, jana askari wa Jeshi la Polisi, wakiwamo wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) waliojiandaa kwa zana mbalimbali, ikiwamo mabomu ya machozi na bunduki za risasi za moto, waliweka ulinzi katika ofisi ndogo za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizoko Barabara ya Lumumba, jijini Dar es Salaam wakati wa maandamano ya Chama cha Wananchi (CUF).

    Maandamano hayo yaliyoongozwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Makamu Mwenyekiti, Machano Khamis Machano na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad, yaliandaliwa kwa lengo la kuishinikiza serikali iwataje na kuwafikisha mahakamani mafisadi waliochota fedha katika EPA.

    Askari hao waliimarisha ulinzi katika ofisi hizo za CCM, baada ya waandamanaji waliokuwa wakizomea na kutoa maneno ya kejeli dhidi ya chama hicho na serikali kwa madai ya kukumbatia ufisadi na mafisadi, kufika katika eneo ziliko ofisi hizo walipokuwa wakienda katika viwanja vya Mnazi Mmoja, yalikohitimishwa maandamano hayo.
    Hata hivyo, askari hao waliondoka katika ofisi hizo, baada ya waandamanaji kupita kwa amani katika eneo hilo.

    SOURCE: Nipashe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...