Kutoka shoto: Ustadh Makoe, Maalim Abdallah (Mwenyekiti wa ZAWA), Idris Zahran (Ofisa wa habari na mawasiliano Ubalozini UK), Mohammed Zahran (Katibu wa East African Education), Saleh Jaber (Mwenyekiti wa Zenjydar Community Association), Ustadh Issa, Ustadh Khamis Faki (Mwenyekiti msaidizi East African Education Foundation), Salum Abdallah na wajumbe wengine waliohudhuria katika hafla ya baraza la Eid London 2008.
Kutoka shoto: Bwana Idris Zahran, Abuu Faraj (Mwenyekiti TZUK Association), Saleh Jaber (Mwenyekiti Zenjydar Community Association), Ustadh Nassor Haroub (Mwenyekiti East African Education Foundation) na Abdallah Maka.

Baadhi ya jumuia za East London zilihudhuria kwenye baraza la Eid ambalo limefanyika tarehe 11/10/2008. Baraza la Eid limeandaliwa na jumuia ya ZAWA ikishirikiana na East African Education Foundation na TZUK Association na Ubalozi wa Tanzania nchini UK.
Hii ni mara ya pili baraza la Eid kufanyika tangu mwaka 2007 na kusimamiwa rasmi na Maalim Abdallah.
Katika hafla hiyo, mgeni wa heshima bwana Idris Zahran ambaye aliwakilisha Ubalozi wa Tanzania nchini UK alipata fursa ya kukaribisha wote waliohudhuria na kuleta salamu za Mheshimiwa balozi Mwanaidi Maajar Sinare za Eid Mubarak.
Vilevile bwana Idris alisema, Mheshimiwa balozi anaanzisha mpango wa kukutana na wote wenye jambo lolote ambalo wangependelea kuongelea na Mheshimiwa katika kuleta maendeleo. Mpango huo ambao utakuwa kila siku ya Alhamisi, itakuwa ni siku maalumu kwa yoyote atakayependelea kukutana na mheshimiwa balozi Mwanaidi Maajar.
Picha na Ustadh Khalfan kwa niaba ya Zenjydar Community Association.
--
Zenjydar Community Association
www.zenjydar.co.uk

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ice Ice Baby! nakuonaa!
    umezeeka lakini!

    ReplyDelete
  2. huyu Saleh JABIR NDIO MUASISI WA BONGO FLAVA ANGEKUWA NA HAKI ZA COPYRIGHT ANGEKUWA TAJIRI MKUBWA SANA(INTERLECTUAL PROPERTY LAW),

    KWANI NDIO MBUNIFU WA MTINDO HUU.ALIKUWA NA KIBAO CHA ICE ICE BABY,SALEH JABIR KARAP KAWA CHUNGU,KITU KIMENIKAA ROHONI,LEO HII WAMEKUJA WATU WANASEMA WAO NDIO WAASISI WAKATI UKWELI UNAJULIKANA ILIUWA NI SALEH JABIR NA KIJANA BLACK MOSES WATOTO WA AL HARAMAIN SCHOOL KATI KATI YA JIJI.

    NAAMINI MITHUPU UNAIJUA HISTORIA HII KWA VILE NI MTOTO WA MJINI TULIKUWA WOTE YMCA UKITUPIGA PICHA. NA HATA SALEH JABIR ALIPOKUWA AKIFANYA MAMBO YAKE NEW AFRICA HOTEL.

    NASEMA HUYU NDIYE MUASISI SI MR.TWO ANAJIPAKAZIA KUWA NI MUASISI. NADHANI WAKATI HUO ALIKUWA BADO YUKO MBEYA HAJAJA DAR.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...