chumba namba 301 ambacho msanii jose chameloene alikuwamo kabla ya kujirusha dirishani akiwa usingizini na kuvunjika miguu yake yote miwili
hoteli ya impala ya a-taun ambako msanii wa uganda jose chameleone alijirusha akiwa ndotoni usiku wa kuamkia jana. chumba alichokuwa ni hicho kilichowekwa alama ya mduara mwekundu

habari zimeinia sasa hivi toka a-taun na tanga zimethibitisha kuvunjika miguu yote miwili kwa msanii jose chameleone wa uganda katika hoteli ya kitali ya impala.

jose chameleone alikuwa amepanga chumba namba 301 kilicho ghorofa ya tatu katika hoteli ya impala na alipojirusha majira ya saa kumi na moja asubuhi ya jana jumamosi aliangukia balkoni ya mgawaha wa continental wa hoteli hiyo ulio ghorofa ya kwanza. ambapo ndio kusema alidondoka ghorofa mbili na kuvunjika miguu yote miwili.

habari zinasema kwamba mara alipoanguka jamaa walimzingira na kumdhania ni mwizi, hadi wafanyakazi wa hoteli waliomtambua walipowaita mapromota wake ambao walimpeleka hospitali ya aicc haraka haraka.

habari za uhakika zinasema jose chameleone aliyekuwa amefika a-taun kwa shoo iliyoandaliwa na kampuni ya sigara kwenye hoteli ya naura springs, ambako baada ya kumaliza shoo milango ya saa sita Ijumaa usiku alielekea kujirusha katika klabu ya mawingu na baadaye kumalizia kwenye ufunguzi wa disko jipya katika klabu ya colobus.

kwa mujibu wa gadna g. habash wa clouds 88.4fm ambaye alikuwa anaongozana naye kote huko, baada ya hapo jose chameleone ilikuwa aelekee tanga kwa ajili ya tamasha la fiesta kabla ya kukumbwa na maswahiba hayo.
gadna kaniambia kwamba jose chameleone hawezi tena kufanya onesho kwenye fiesta hapo tanga kwani madaktari wa hospitali ya aicc alikopelekwa walisema amevunjika miguu yake yote miwili. na inaonesha hatikuwa fiti kufanya maonesho kwa muda mrefu ujao wakati akiuguza miguu yake.

"jana alimpigia mkewe simu ambaye alikodi ndege chap chap toka kampala na kumchukua kumpeleka huko kwa matibabu katika hospitali ya Nsabya", amesema gadna. alisema muda wote jamaa alikuwa wa kawaida kabisa na hakuwa amepiga maji kama inavyoshukiwa.

hata hivyo gdna hakusema kwa nini has jose alijirusha, ila kuna habari zinasema kwamba msanii huyo ana matatizo ya muda mrefu ya kutembea akiwa amelala fofofo - kwa kiinglishi sleep walking.

wadau wa uganda wategemee habari za undani za mkasa wa jose chameleone kwenye magazeti ya kesho kwani habari hiyo inafuatiliwa sana, na hata globu hii ya jamii imepigiwa simu na wahariri kibao kutaka kujua kilichosibu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi hizi picha zako uwe unaweka label yaani michuzi blog hapa ndo nafasi ya kwenda commercial yaani 'kujitangaza' kwa jamii this is a good news other news papers watatumia hizi picha esp. ya hiyo hotel na wanatakiwa wanunue toka kwako. Use the opportunity Misupu

    ReplyDelete
  2. Sleep walking au mumemuendea bagamoyo msanii wa watu.....????? hahahahhah nilikua najua sleep walking inaisha mtu ukiwa 15 to 19 yrs old.

    Baada ya hapo anahitaji psychiatric counseling.

    ReplyDelete
  3. whaaaaat? that's some serious sleep walking!Checked my calender usikute ni april fools day?

    ReplyDelete
  4. Hakuna Bwagamoyo ama nini, "Bhang" tu hizo babaakee, wafanyamchezo na makitu ya kutoka naura!! mnacheza.

    ReplyDelete
  5. Pole sana bro. Chameleone.

    Michu, yaani sisi watu wa Forensiki, tungemchunguza sana mwenyewe kwanza. Pia kwa kuangalia hicho chumba alimolala tungeweza kuanza kudonoa kama ni kweli alilala kwenye hicho kitanda au la na kama kwenye kitanda walikuwepo zaidi ya mtu mmoja n.k Na kama ni hivyo huyo mtu / watu wengine nao wangesaidia upelelezi. Tukio kama hili haliwezi kuhitimishwa kiulahisi tu kuwa ni ugonjwa wake wa kutembea ndotoni. Je ni mara ngapi(ukubwani mwake) amesha tembea kihivyo. Je kama ni kweli Msanii huyu amepewa ushauri gani na Daktari wake maana anaweza kujihatarisha maisha na ya wengine.

    ReplyDelete
  6. kwa sisi wataalam wa mambo haya ni kuwa mwenye ugonjwa wa kuota ndoto za kutembea huwa hatakiwi kulala kwenye chumba cha ghorofani, na kama ikitokea kuwa kalala ghorofani ni lazima chumba hicho kiwe na kinga ya kumzia mtu huyo kutoka nje, either kwa dirisha la kioo au nondo, na sio rahisi mtu huyo akaota hadi akafungua milango au dirisha kisha akaendelea kuota hadi aanguke chini, kwa haraka hapo huyo jamaa alikuwa kala msuba saana, au alisukumwa nje na malaya, au palikuwa na ugomvi fulani kaamua kuruka chini mwenyewe!mimi nilikuwa naota natembea hadi nikiwa na miaka 23, ila mara nyingi nilikuwa nazinduka nikiwa bafuni au chooni, na ndo nilipewa masharti na daktari sehem za kulala napokuwa nje ya getto langu!

    ReplyDelete
  7. Mimi ni mwanga wa kutupwa.

    Hiyo sleep walking kwa kiafrika kinaitwa kuwanga usiku.Acheni kutumia kiingereza kutulaghai waafrika.

    Mtu akiamka usiku na kutembea ni mwanga mia kwa mia hicho kiingereza chenu cha sleep walking muishie nacho huko huko Uingereza na madarasa ya tuition zenu.

    Michuzi babaako hakukupeleka ujifunze kiingereza udanganye waswahili wenzio. Mtu kama mwanga mwite mwanga siyo ooH SLEEP WALKER anafanya sleep walking acha uwongo. Kawadanganye wakwezo Uganda siyo sisi tuliozaliwa na kukulia Bagamoyo kwa wanga.

    ReplyDelete
  8. Kama alikuwa anawanga Usiku, Arusha hapafai kabisa angeuliza wachawi Arusha au angepiga ramli Uganda kwanza.

    Arusha kuna Walokole wakali kama akina Mwakasege na wengineo ambao huwa wanatelemsha wanga kutoka angani kwa sala zao za kilokole.Usijaribu kuwanga usiku Arusha.

    Anga la Arusha linafaa tu kwa ndege za kimataifa lakini halifai kabisa kwa ndege za kichawi.Mwanga ukiruka usiku Arusha Mjini utashushwa ghafla usipotaka kutua.Wachawi wa Sumbawanga mpo hapo nimeshawatahadharisha.Anga la Uganda na Sumbawanga ni rahisi kuruka kiwanga kuliko anga la Arusha mjini kwa wale mnaopenda kusafiri kwa ndege za asili bila ruksa wala leseni ya mamlaka ya anga Tanzania.

    ReplyDelete
  9. Hizi ni bangi :) Msuba si mchezo jamani.

    ReplyDelete
  10. Bangi la Tanzania hatari.
    Ukilivuta usiku kabla ya kulala lazima usiku mtu ufanye sleep walking mwanangu.Hapo ubishi hakuna.
    Hotel ni vizuri wakipangisha mtu waulize kama huwa anavuta bangi au la ili wamweke chumba cha chini ili kumwepusha akianza sleep walking asije pitiliza dirishani na kupitiliza hadi chini akafa wakamkosa mteja wao mvuta bangi.

    ReplyDelete
  11. Waganda Hawavuti banghe wanavuta hizi gundi za viatu au petroli.. dah lakini kweli pale mdau, huyu jamaa!? mhn

    = = =
    Buffalo,
    New York

    ReplyDelete
  12. wabongo achane uzushi...mimi binafsi sidhani kama kuna utata na issue ya sleep walking. Kuna rafiki yangu alikufa tukiwa primary school kwa ugonjwa huu huu. Teremka kutoka ghorofani ivyo ivyo.
    Kwa kifupi kinachotokea ni kuwa unapokuwa umelala...ubongo unakata mawasiliano(connection) ya movement kusudi mtu usiweze ku-act out your dreams. Sasa watu wenye matatizo ya sleep walking ni kuwa ubongo wao haukati haya mawasiliano na mtu anaweza kuamka na kufanya vitu. Kuna watu wanaua kabisa wakiwa katika hii state ya sleep walking. Mkitaka reference ya cases zilizoshinda mahakamani niulize.
    Moja hii hapa: http://www.citynews.ca/news/news_4792.aspx
    nyingine:
    http://www.cnn.com/US/9905/25/sleepwalk.defense/


    mtoto

    ReplyDelete
  13. ....KUFUMANIWA,je? Inaweza kuwa sababu mojawapo ya mtu kuruka dirisha hasa kama mwenye mali amekuja na mtu SITA Miraba Minne! teh teh! Sleep walking, my A#$@$!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...